Nenda kwa yaliyomo

Samoa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malo Sa'oloto Tuto'atasi o Samoa
Independent State of Samoa
Bendera ya Samoa Nembo ya Samoa
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Fa'avae i le Atua Samoa
(Samoan: "Samoa is founded on God")
Wimbo wa taifa: The Banner of Freedom
Lokeshen ya Samoa
Mji mkuu Apia
13°35′ S 172°20′ W
Mji mkubwa nchini Apia
Lugha rasmi Samoan, Kiingereza
Serikali Parliamentary democracy
Malietoa Tanumafili II
Uhuru
Tarehe
1 Januari 1962
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
2,842 km² (174 ya)
0.3%
Idadi ya watu
 - Julai 2012 kadirio
 - 2006 sensa
 - Msongamano wa watu
 
194,320 (166)
179,186
63.2/km² (126 ya)
Fedha Tala (WST)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-11)
(UTC)
Intaneti TLD .ws
Kodi ya simu +685

-Bendi ya Polisi ya Samoa

Samoa ni nchi ya visiwani ya Polynesia katika Pasifiki ya kusini yenye wakazi 176,710 (2001 sensa). Nchi huru ya Samoa ni sehemu ya magharibi ya funguvisiwa ya Samoa. Sehemu ya mashariki iko chini ya Marekani.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]
Ramani ya Samoa

Eneo lake ni visiwa tisa (au kumi kama kisiwa kidogo sana kinahesabiwa humo), jumla ni kilomita za mraba 2,934. Visiwa viwili vikubwa vya Upolu (km² 1,118) na Savai'i (km² 1,708) vina asilimia 96 za eneo lote. Kuna bado visiwa viwili vidogo vya Manono na Apolima vyenye wakazi, halafu visiwa vingine visivyokaliwa na watu.

Mji mkuu wa Apia uko Upolu.

Mahali pa juu ni mlima Mauga Silisili mwenye kimo cha mita 1,858.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Samoa ilikaliwa na Waaustronesia tangu miaka 3,000 iliyopita.

Mzungu wa kwanza alifika mwaka 1722.

Ilikuwa ufalme wa kujitegemea kabisa hadi mwaka 1889. Mwaka ule uliwekwa chini ya ulinzi wa nchi tatu: Uingereza, Ujerumani na Marekani.

Baada ya kifo cha mfalme 1898 kulitokea fitina juu ya mrithi wake na nchi za nje zilingia kati. Mkataba wa Pande Tatu wa mwaka 1899 uligawa funguvisiwa ya Samoa kati ya Ujerumani na Marekani. Sehemu ya magharibi ikawa "Samoa ya Kijerumani".

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia visiwa vilitekwa na New Zealand vikabaki chini ya nchi hiyo kama maeneo yaliyokabidhiwa na Shirikisho la Mataifa na baada ya 1945 na Umoja wa Mataifa kwa jina la "Samoa ya Magharibi".

Uhuru ulipatikana mwaka 1962.

Lugha na Dini

[hariri | hariri chanzo]

Wakazi ni 194,320, karibu wote wakiwa wametokana na wakazi asili.

Kuna lugha mbili tu ambazo huzungumzwa nchini Samoa, zote mbili zikiwa lugha rasmi, yaani Kiingereza na Kisamoa.

Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo, wengi wakiwa Waprotestanti, hasa Wakalvini (31.8%), wakifuatwa na Wakatoliki (19.4%).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.