Hawaii
Hawaii | |||
| |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Honolulu | ||
Eneo | |||
- Jumla | 28,311 km² | ||
- Kavu | 16,635 km² | ||
- Maji | 11,677 km² | ||
Tovuti: http://www.hawaii.gov/ |
Hawaii (kwa Kihawaii: Mokuʻāina o Hawaiʻi) ni funguvisiwa la bahari ya Pasifiki ambalo ni jimbo la Marekani, pia ni jina la kisiwa chake kikubwa.
Hawaii ilikuwa ufalme wa Wapolinesia, ikawa koloni la Marekani]] katika karne ya 19 na imekuwa jimbo la Marekani tangu tarehe 21 Agosti 1959.
Mji mkuu ni Honolulu kwenye kisiwa cha Oahu.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Funguvisiwa la Hawaii lina jumla ya visiwa 137 vyenye eneo la kilomita za mraba 16,649 za nchi kavu. Visiwa vilivyo vingi ni vidogo, havikaliwi na watu.
Visiwa vikubwa, kuanzia magharibi kwenda mashariki, ni:
Visiwa vyote vina asili ya kivolkeno. Mlima Mauna Kea ni volkeno ndefu kabisa duniani yenye kimo cha mita 4201 juu ya UB lakini inaanza chini ya bahari katika kina cha mita 5,000, hivyo kimo cha jumla ni zaidi ya mita 9,000. Volkeno ya pili ni Mauna Loa yenye masi kubwa zaidi. Mauna Loa ni volkeno hai kwenye kisiwa kikuu cha Hawaii, pamoja na mlima Kilauea.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Hawaii ilikaliwa na Wapolynesia waliofika kwa mitumbwi yao mikubwa. Jamii zao zilitawaliwa na familia za makabaila zilizotazamiwa kuwa za juu kuliko watu wa kawaida. Tabaka la pili la juu lilikuwa lile la makuhani.
Kati ya miaka 1781 na 1811 Kamehameha I alifaulu kuunganisha visiwa vyote chini ya utawala wake akawa mfalme wa kwanza wa Hawaii yote.
Katika miaka ya karne ya 19 iliyofuata wageni kutoka Marekani na Ulaya walianza kujenga makazi visiwani. Uchumi wa kisasa ulianzishwa kwa mashamba ya miwa na uvuvi.
Mwaka wa 1842 Marekani ikatambua ufalme wa Hawaii kama nchi huru ya kujitegemea.
Athira ya wafanyabiashara matajiri Wazungu ikakua. Kwa njia ya ghasia wakamlazimisha mfalme Kalakaua mwaka 1887 kukubali katiba iliyowapa haki ya kupiga kura matajiri pekee. Mwaka uleule Marekani ilipewa haki ya kutawala kituo cha kijeshi cha Pearl Harbour.
Malkia Liliuokalani († 1917) alijaribu mwaka 1893 kufuta katiba na kurudisha mamlaka ya wafalme lakini alipinduliwa na wenye mashamba makubwa waliosaidiwa na wanajeshi wa Marekani, na jamhuri ya Hawaii ikatangazwa.
Wakati wa Vita ya Marekani dhidi Hispania serikali ya Marekani iliamua kutwaa Hawaii na kuitangaza kuwa mali ya Marekani. Baadaye visiwa vilitawaliwa kama koloni na baadaye kama eneo la kitaifa la Marekani.
Marekani iliingia katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa shambulio la Japani dhidi ya manowari za Marekani katika bandari ya Pearl Harbour tarehe 7 Desemba 1941.
Tarehe 21 Agosti 1959 Hawaii imekuwa jimbo kamili la Marekani.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Wakazi wake ni 1,419,561 (2014), kati yao 10% ni Wahawaii asili; wengi zaidi ni Wazungu, machotara wa aina mbalimbali, Wafilipino, Wajapani n.k.
Lugha rasmi ni Kiingereza, inayozungumwa nyumbani na 75% ya wakazi, na Kihawaii.
Upande wa dini, wengi ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki, likifuatwa na Wamormoni. Lakini Waprotestanti kwa jumla ni wengi zaidi.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Niʻihau sq mi 70 (km2 180)
-
Kauaʻi sq mi 552.3 (km2 1 430)
-
Oʻahu sq mi 598 (km2 1 550)
-
Maui sq mi 727.3 (km2 1 884)
-
Molokaʻi sq mi 260 (km2 670)
-
Lānaʻi sq mi 140.5 (km2 364)
-
Kahoʻolawe sq mi 44.6 (km2 116)
-
Hawaiʻi sq mi 4 028.2 (km2 10 433)
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Bushnell, O. A. The Gifts of Civilization: Germs and Genocide in Hawaiʻi. Honolulu: University of Hawaii Press, 1993.
- Holmes, T. Michael. The Specter of Communism in Hawaiʻi. Honolulu: University of Hawaii Press, 1994.
- Russ Jr., William Adam. The Hawaiian Republic (1894-98) and Its Struggle to Win Annexation. Selinsgrove, PA: Susquehanna University Press, 1961.
- Schamel, Wynell and Charles E. Schamel. "The 1897 Petition Against the Annexation of Hawaiʻi." Social Education 63, 7 (November/December 1999): 402–408.
- Stokes, John F.G. "Spaniard and the Sweet Potato in Hawaiʻi and Hawaiian-American Contacts." American Anthropologist, New Series, vol. 34, no. 4 (1932) pp. 594–600.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Official website
- Hawaii State Guide from the Library of Congress
- Hawaii katika Open Directory Project
- Hawaiʻi State Fact Sheet from the U.S. Department of Agriculture
- USGS real-time, geographic, and other scientific resources of HawaiiIlihifadhiwa 19 Desemba 2011 kwenye Wayback Machine.
- Energy Data & Statistics for Hawaii Ilihifadhiwa 9 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.
- Satellite image of Hawaiian Islands Ilihifadhiwa 4 Aprili 2004 kwenye Wayback Machine. at NASA's Earth Observatory
- Documents relating to Hawaii Statehood, Dwight D. Eisenhower Presidential Library Ilihifadhiwa 1 Aprili 2015 kwenye Wayback Machine.
- Happily a State, Forever an Island by The New York Times
- Hawaiʻi Then and Now – slideshow by Life magazine (Archived from the original Ilihifadhiwa 3 Novemba 2010 kwenye Wayback Machine. on November 3, 2010)
- Hawaiian Imprint Collection From the Rare Book and Special Collections Division at the Library of Congress
Majimbo ya Marekani |
---|
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hawaii kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |