Maryland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maryland
Mahali pa Maryland katika Marekani
Mahali pa Maryland katika Marekani

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Annapolis
Eneo
 - Jimbo 32,133 km²
 - Bara 25,314 km² 
 - Maji 6,819 km² 
Tovuti: http://www.maryland.gov/
Ramani ya Maryland

Maryland ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko kwenye pwani la Atlantiki upande wa mashariki ya Marekani bara. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, West Virginia, Delaware, Virginia na mkoa wa shirikisho la Washington DC.

Hori la Chesapeake linagawa eneo la jimbo kwa pande mbili. Mji mkuu ni Annapolis na mji mkubwa ni Baltimore. Kwa miji mingine, angalia orodha ya miji.

Iliundwa kama koloni ya Ungereza mwaka 1634 na mkabaila Lord Baltimore aliyetumia jina la Maryland kwa heshima ya mke wa mfalme Charles I. Baltimore aliyetoka Ueire alitafuta hasa mahali kwa ajili ya Wakatoliki wasiokubaliwa katika koloni nyingine za Uingereza. Maryland ilikuwa koloni ya kwanza yenye sheria iliyokubali madhehebu yote ya kikristo.

Mji mkuu wa Washington DC ulijengwa kwenye eneo lililotengwa na eneo la Mayrland kando la mto Potomac. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani 1861-1865 Maryland ilikaa upande wa Maungano.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Majimbo ya Marekani

AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming

Flag USA template.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maryland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.