Nenda kwa yaliyomo

Virginia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Virginia
Virginia

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Richmond
Eneo
 - Jumla 110,785 km²
 - Kavu 102,548 km² 
 - Maji 8,236 km² 
Tovuti:  http://www.virginia.gov/
Ramani ya Virginia

Virginia ni jimbo (commonwealth) la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika mashariki ya Marekani bara. Imepakana na West Virginia, Maryland na mkoa wa shirikisho la Washington D.C. upande wa kaskazini, North Carolina na Tennessee upande wa kusini halafu Kentucky na West Virginia upande wa magharibi. Upande wa mashariki ni bahari ya Atlantiki pamoja na hori ya Chesapeake.

Mji mkuu ni Richmond (Virginia) na mji mkubwa ni Virginia Beach.

Virginia ilikuwa koloni ya Uingereza tangu kuanzishwa kwa mji wa Jamestown (Virginia) mwaka 1607. Jina la "Virginia" lamaanisha "kibikira" kwa heshima ya malkia Elizabeth I ambaye hakuolewa. Mwaka 1788 ilikuwa jimbo la kujitawala la nchi mpya ya Marekani ni moja kati ya majimbo 13 yaliyoanzisha Marekani.

Jimbo la West Virginia iliwahi kuwa sehemu ya Virginia. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani Virginia iliondoka katika maungano ya madola ya Marekani ikajiunga na waasi wengine katika Shirikisho la Marekani. Wakati ule wilaya kwenye magharibi ya jimbo zilijitenga na kuwa jimbo jipya lililobaki upande wa maungano hata baada ya mwisho wa vita.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Majimbo ya Marekani

AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming

Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Virginia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.