Guam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Territory of Guam
Guåhan
Bendera ya Guam Nembo ya Guam
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Where America's Day Begins"
Wimbo wa taifa: Fanohge Chamoru
Lokeshen ya Guam
Mji mkuu Hagatna (Agana)
°′  °′ 
Kijiji Dededo
Lugha rasmi Kiingereza, Kichamoru
Serikali Eneo la ng'ambo la Marekani
Donald Trump
Felix Perez Camacho
Eneo la ng'ambo la Marekani
Koloni la Hispania
Koloni la Marekani
Eneo la ng'ambo la Marekani

1668
1898
1949
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
543.52 km² (ya 192)
‘‘(kidogo sana)’’
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
170,000 (ya 186)
307/km² (ya 37)
Fedha US Dollar (USD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
Chamorro Standard Time (UTC+10)
-- (UTC)
Intaneti TLD .gu
Kodi ya simu +1-671

-



Ramani ya Guam.

Guam (kwa Kichamoru: Guåhan) ni eneo la ng'ambo la Marekani (U.S. Territory of Guam) upande wa kusini wa funguvisiwa ya Mariana katika Bahari ya Pasifiki. Huhesabiwa kati ya visiwa vya Mikronesia.

Eneo la kisiwa hicho ni kilometa mraba 543.

Mji mkuu ni Hagåtña (Agana).

Uchumi wa Guam unategemea kituo cha kijeshi cha Marekani pamoja na utalii.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza wanaojulikana ni Wachamoru walihamia miaka 4,000 hivi iliyopita.

Tangu mwaka 1668 visiwa vya Mariana vilikuwa koloni la Hispania.

Baada ya vita ya Marekani dhidi Hispania Guam ikatwaliwa na Marekani. Visiwa vya upande wa Kaskazini vikauzwa kwa Ujerumani na kuwa Mariana ya Kaskazini.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kisiwa kikatwaliwa na Japani, lakini tarehe 21 Julai 1944 Waamerika walirudi na kuwafukuza Wajapani.

Mwaka 1949 kisiwa kilipewa hadhi ya Eneo la ng'ambo la Marekani, wakazi wake wakapewa uraia wa shirikisho hilo.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa 37.1% ya wakazi wote (159,358) ni Wachamoru, wakifuatwa na Wafilipino (26.3%). Wachamoru wengi zaidi wanaishi Marekani bara.

Upande wa dini, 85% ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.