Pitcairn
Pitcairn ni kisiwa katika Pasifiki na pia jina la funguvisiwa ambalo ni eneo la ng'ambo la Uingereza pekee katika Pasifiki.
Makao makuu ni kijiji pekee cha Adamstown.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Pitcairn ni kisiwa chenye asili ya kivolkeno. Eneo lake ni km² 4.6 na idadi ya wakazi ni 46 tu, ambao wanazungumza Krioli maalumu ya Kiingereza na kuwa Waadventista Wasabato.
Visiwa vingine ni atolli za Oeno, Henderson na Ducie ambazo hazina wakazi. Watu walio karibu wako kwenye kisiwa cha Pasaka (km 2,000) na kwenye Polynesia ya Kifaransa (km 500).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Hakuna uhakika kuhusu wakazi na wageni wa Pitcairn kabla ya kugunduliwa na kijana Pitcairn kwenye jahazi ya Kiingereza mwaka 1767. Inaaminiwa ya kwamba Wapolinesia walikalia visiwa tangu karne kadhaa, lakini hakuna uhakika kama walikuwepo bado wakati wa kufika kwa Wahispania waliopita sehemu hizi katika karne ya 17. Kwa vyovyote Waingereza hawakukuta tena watu.
Tangu mwaka 1790 kisiwa kilikaliwa na waasi wa Bounty iliyokuwa jahazi ya Kiingereza ambamo ulitokea uasi wa mabaharia dhidi ya nahodha. Waasi waliamua kujificha kwa sababu waliogopa adhabu ya kifo kulingana na sheria za Uingereza za wakati ule. Wakazunguka bahari pamoja na wanawake wa Tahiti wakakuta Pitcairn wakajenga makazi yao kisiwani.
Mwaka 1838 kisiwa kilitangazwa kuwa koloni la Uingereza.
Mwaka 1856 watu wa Pitcairn walihamishiwa kisiwa cha Norfolk kwa sababu walikuwa wengi mno kulingana na udogo wa kisiwa hata wakaona njaa. Lakini familia tano waliamua kurudi tena na ndio mababu wa wakazi wa leo.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi unategemea hasa kilimo cha kijungujiko na misaada kutoka Uingereza. Mara chache kisiwa kinatembelewa na watalii.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- the cia gov factbook Ilihifadhiwa 25 Oktoba 2017 kwenye Wayback Machine.
- http://www.lareau.org/pitcairn2.gif Ilihifadhiwa 3 Julai 2007 kwenye Wayback Machine. Ramani
- http://www.government.pn/ Tovuti rasmi ya Pitcairn
- http://www.jncc.gov.uk/pdf/OT_Pitcairn.pdf Ilihifadhiwa 13 Oktoba 2010 kwenye Wayback Machine. Mimea na wanyama wa Pitcairn
- http://aob.oxfordjournals.org/cgi/content/abstract/92/1/31 Maua ya kisiwa
- http://library.puc.edu/pitcairn/pitcairn/index.shtml Habari za Pitcairn (Pacific Union College; englisch)
- http://www.koys.de/Pitcairn/ Pitcairn: picha
- http://onlinepitcairn.com/newslinks.htm Ilihifadhiwa 30 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. Blogu ya Mike Warren
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |