Eneo la ng'ambo la Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya maeneo ya ng'ambo ya Uingereza
(Eneo la Kiingereza kwenye Antaktika na Akrotiri na Dhekelia (Kupro) havionyeshwi)

Eneo la ng'ambo la Uingereza ni moja kati ya maeneo 14 ambayo ni chini ya serikali ya Uingereza lakini si sehemu za nchi.

Kwa Kiingereza yameitwa "British Overseas Territory" tangu sheria ya 2002 badala ya jina la awali "British dependent territory" yalivyoitwa tangu 1981. Kabla ya 1981 yaliitwa "koloni"

Hali ya maeneo haya ni tofauti na Jumuiya ya Madola ambayo ni jumuiya ya hiari ya koloni za zamani za Uingereza.

Mambo ya kisheria[hariri | hariri chanzo]

Kwa jumla wakazi wa maeneo ya ng'ambo ya Uingereza ni raia wa Uingereza wana haki kuhamia Uingereza penyewe. Kila eneo lina bunge lake na uhuru fulani wa kutunga sheria zake.

Visiwa vya mfereji wa Kiingereza (Jersey, Guernsey) na Isle of Man si maeneo ya ng'ambo ya Uingereza bali "maeneo chini ya taji la Uingereza".

Maeneo ya ng'ambo ya Uingereza[hariri | hariri chanzo]

Bendera Eneo Mahali Wito Eneo Wakazi Mji Mkuu
Flag of Anguilla.svg Anguilla Karibi Strength and Endurance 102 km²
(39.4 mi²)
12,8 The Valley
Flag of Bermuda.svg Bermuda Atlantiki Quo fata ferunt (Kilatini: "Pote heri inapotupeleka") 53.3 km²
(20.6 mi²)
64,482 Hamilton
Flag of the British Antarctic Territory.svg Eneo la Uingereza katika Antaktika Antarctica Research and discovery 1,709,400 km²
(666,000 mi²)
200 staff Rothera (kituo kikuu)
Flag of the Commissioner of the British Indian Ocean Territory.svg Eneo la Uingereza katika Bahari Hindi Bahari Hindi In tutela nostra Limuria (Kilatini: "Tumekabidhiwa Limuria") 60 km²
(23 mi²)
3,200 military and staff Diego Garcia (kituo cha kijeshi)
Coat of arms of the British Virgin Islands.svg Visiwa vya Virgin vya Uingereza Karibi Vigilate (Kilatini: "Mwe macho!") 153 km²
(59 mi²)
21,73 Road Town
Coat of arms of the Cayman Islands.svg Visiwa vya Cayman Karibi He hath founded it upon the seas 260 km²
(100.4 mi²)
57,8 George Town
Flag of the Falkland Islands.svg Visiwa vya Falkland Atlantiki Desire the right 12,173 km²
(4,702 mi²)
2,967 Stanley
Gibraltar Ulaya ya Kusini Nulli expugnabilis hosti (Kilatini: "Haishindwi na adui yeyote") 6.5 km²
(2.5 mi²)
27,776 Gibraltar
Coat of arms of Montserrat.svg Montserrat Karibi 102 km²
(39 mi²)
9 Plymouth
Coat of arms of the Pitcairn Islands.svg Visiwa vya Pitcairn Pasifiki 43 km²
(17 mi²)
(all islands)
67 Adamstown
Flag of Saint Helena.svg Saint Helena (pamoja na Ascension na Tristan da Cunha)   Atlantiki Loyal and unshakeable 410 km²
(158 mi²)
(all islands)
6,563 Jamestown
Flag of South Georgia and the South Sandwich Islands.svg Visiwa vya South Georgia na South Sandwich Atlantiki Leo terram propriam protegat (Kilatini: "Simba alinda kwake") 3,903 km²
(1508 mi²)
11-26 staff King Edward Point/Grytviken
Flag of the United Kingdom.svg Akrotiri and Dhekelia (Kupro) Mediteraneo (Kupro) Dieu et mon droit (Kifaransa: "Mungu na haki yangu") 254 km²
(98 mi²)
wanajeshi 15,000 Episkopi Cantonment
Flag of the Turks and Caicos Islands.svg Visiwa vya Turks na Caicos Karibi One people, one nation, one destiny 430 km²
(166 mi²)
26,288 Cockburn Town

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]