Jumuiya ya Madola
Jumuiya ya Madola Common Wealth of nations (en) | |
---|---|
Mji mkubwa | New Delhi |
Lugha rasmi | Kiingereza |
• Mfalme | Charles III |
Wanachama | nchi 53 nchi 33 ndogo |
Historia | |
1583 -1997 | |
• Tangazo la Balfour | 19 Novemba 1926 |
• Sanamu ya Westminster | 11 Desemba 1931 |
• Tangazo la London | 28 Aprili 1949 |
Eneo | |
• Jumla | km2 ▲ 29,958,050 |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 2.7 Bilioni |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ▲ $13.1 Trilioni |
• Kwa kila mtu | ▲ $4,810 |
Tovuti rasmi: https://thecommonwealth.org | |
Jumuiya ya Madola (kwa Kiingereza Commonwealth of Nations) ni muungano wa nchi mbalimbali hasa Uingereza na nchi zilizokuwa koloni zake.Umoja huu umeanzishwa mw. 1926 kama "Jumuiya ya Kibritania" (British Commonwealth) na kupewa jina lake la sasa tangu 1949. Inafuatana na Milki ya Kiingereza ambayo ilikuwa dola kubwa kabisa katika historia ya dunia lakini maeneo yake yalianza kuachana baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kutokana na kudhoofishwa kwa Uingereza vitani na miendo ya kupigania uhuru katika nchi mbalimbali hasa Uhindi.
Leo zipatao asilimia 30 ya watu wote duniani (watu 1,800,000) huishi katika nchi wanachama za Jumuiya ya Madola. Nchi za jumuiya hii wenye wakazi wengi ni hasa Uhindi, Pakistan, Bangladesh na Nigeria. Kuna pia nchi ndogo sana kama Tuvalu yenye wakazi 11,000 pekee.
Nchi kadhaa zilisimamishwa uanachama au kuondoka kwa hiari zao. Mfano Tanganyika na Zanzibar ziliungana kwa hiyo hazipo tena lakini mpya ya Tanzania imekuwa nchi mwanachama. Vilevile Newfoundland iliondoka katika jumuiya baada ya kujiunga na Kanada kama jimbo.
Pakistan ilisimamishwa uanachama mara kadhaa kwa sababu serikali yake ilipinduliwa na wanajeshi walioanzisha serikali ya kijeshi. Imerudishwa tena.
Zimbabwe ilisimamishwa uanachama baada ya uchaguzi bandia 2002 ikaamua kujiondoa kabisa mwaka 2003.
Jamhuri ya Ueire iliamua mwaka 1949 kuacha viungo vyote na Uingereza ikajitangaza kuwa jamhuri isiyokubali athira ya nje kama hali ya malkia wa Uingereza kuwa mkuuw a dola hivyo ikaondoka katika jumuiya.
Afrika Kusini ilijiondoa 1961 kwa sababu ya upinzani wa jumuiya dhidi ya sheria za apartheid. Baada mwisho wa ubaguzi wa rangi nchi ilirudi katika jumuiya.
Fiji imesimamishwa mara kadhaa baada ya uasi wa kijeshi uliopindua serikali.
Muhtasari
[hariri | hariri chanzo]Jumuiya ya Madola ni ushirikiano wa hiari wa mataifa 56, mengi yao yakiwa yalikuwa sehemu ya Milki ya Britania hapo awali. Inahudumu kama jukwaa la kushirikiana katika masuala ya kimataifa kama vile biashara, elimu, haki za binadamu, na maendeleo endelevu. Ingawa haina mamlaka rasmi ya kisiasa juu ya wanachama wake, Jumuiya hii inakuza ushirikiano kupitia maadili ya pamoja kama demokrasia, utawala bora, na maendeleo ya kiuchumi. Jumuiya ya Madola inafanya kazi kupitia taasisi mbalimbali, zikiwemo "Sekretarieti"" ya Jumuiya ya Madola na Wakfu wa Jumuiya ya Madola, zinazosaidia utungaji sera, ujenzi wa uwezo, na kubadilishana tamaduni kati ya mataifa wanachama.
Moja ya sifa kuu za Jumuiya ya Madola ni uanachama wake wa mataifa mbalimbali, yaliyoko katika mabara tofauti, yakiwemo Afrika, Asia, Karibiani, Ulaya, na Pasifiki. Utofauti huu unatoa fursa za kubadilishana tamaduni na uchumi, na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa yenye mifumo tofauti ya kisiasa na kiuchumi. Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM), unaofanyika kila baada ya miaka miwili, ni jukwaa muhimu kwa viongozi kujadili changamoto za kimataifa na kuunda sera za pamoja. Zaidi ya hayo, Jumuiya ya Madola inahimiza ushiriki wa vijana, usawa wa kijinsia, na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ikiimarisha nafasi yake kama shirika linaloendeleza ushirikiano wa kimataifa na maendeleo.
Wanachama
[hariri | hariri chanzo]Ilijiunga | Nchi | Bara | Wakazi |
---|---|---|---|
1931 | Afrika Kusini | Afrika | 47,423,000 |
1981 | Antigua na Barbuda | Amerika ya Kati | 81,000 |
1931 | Australia | Oceania | 20,555,300 |
1973 | Bahamas | Amerika ya Kati | 323,000 |
1972 | Bangladesh | Asia | 148,384,000 |
1966 | Barbados | Amerika ya Kati | 279,000 |
1981 | Belize | Amerika ya Kati | 287,730 |
1966 | Botswana | Afrika | 1,765,000 |
1984 | Brunei | Asia | 374,000 |
1978 | Dominika | Amerika ya Kati | 79,000 |
1970 | Fiji | Oceania | 848,000 |
1965 | Gambia | Afrika | 1,517,000 |
1957 | Ghana | Afrika | 22,113,000 |
1974 | Grenada | Amerika ya Kati | 103,000 |
1966 | Guyana | South America | 751,000 |
1947 | India | Asia | 1,100,000,000 |
1962 | Jamaika | Amerika ya Kati | 2,651,000 |
1995 | Kamerun | Afrika | 16,322,000 |
1931 | Kanada | Amerika ya Kaskazini | 32,654,500 |
1963 | Kenya | Afrika | 34,256,000 |
1961 | Kipro | Ulaya | 818,200 |
1979 | Kiribati | Oceania | 99,000 |
1966 | Lesotho | Afrika | 1,795,000 |
1964 | Malawi | Afrika | 12,884,000 |
1957 | Malaysia | Asia | 27,356,000 |
1982 | Maldivi | Asia | 329,000 |
1964 | Malta | Ulaya | 402,668 |
1968 | Morisi | Afrika | 1,245,000 |
1995 | Msumbiji | Afrika | 19,792,000 |
1990 | Namibia | Afrika | 2,031,000 |
1968 | Nauru | Oceania | 14,000 |
1931 | New Zealand | Oceania | 4,147,972 |
1960 | Nigeria | Afrika | 132,796,000 |
1947 | Pakistan | Asia | 158,352,000 |
1975 | Papua Guinea Mpya | Oceania | 5,887,000 |
1983 | Saint Kitts na Nevis | Amerika ya Kati | 43,000 |
1979 | Saint Lucia | Amerika ya Kati | 161,000 |
1979 | Saint Vincent na Grenadini | Amerika ya Kati | 119,000 |
1970 | Samoa | Oceania | 185,000 |
1976 | Shelisheli | Afrika | 81,000 |
1961 | Sierra Leone | Afrika | 5,525,000 |
1965 | Singapur | Asia | 4,326,000 |
1978 | Solomon Islands | Oceania | 478,000 |
1948 | Sri Lanka | Asia | 20,743,000 |
1964 | Tanzania | Afrika | 50,329,000 |
1970 | Tonga | Oceania | 102,000 |
1962 | Trinidad na Tobago | Amerika ya Kati | 1,305,000 |
1978 | Tuvalu | Oceania | 10,000 |
1962 | Uganda | Afrika | 28,816,000 |
1931 | Ufalme wa Maungano (Uingereza) | Ulaya | 60,209,500 |
1968 | Uswazi | Afrika | 1,032,000 |
1980 | Vanuatu | Oceania | 211,000 |
1964 | Zambia | Afrika | 11,668,000 |
Nchi wanachama za zamani
[hariri | hariri chanzo]Ilijiunga | Nchi | Bara | Ilitoka |
---|---|---|---|
1931 | Ueire | Ulaya | 1949 |
1931 | Newfoundland | Amerika ya Kaskazini | 1949 |
1961 | Tanganyika | Afrika | 1964 |
1963 | Zanzibar | Afrika | 1964 |
1980 | Zimbabwe | Afrika | 2003 |