Visiwa vya Falkland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
'
Bendera ya Visiwa vya Falkland (Falkland Islands, Malvinas) Nembo ya Visiwa vya Falkland (Falkland Islands, Malvinas)
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Desire the right"
Wimbo wa taifa: "God Save the Queen"
Lokeshen ya Visiwa vya Falkland (Falkland Islands, Malvinas)
Mji mkuu Stanley
51°42′ S 57°51′ W
Mji mkubwa nchini Stanley
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Eneo la ng'ambo la Uingereza
Queen Elizabeth II
Eneo la ng'ambo la Uingereza
Siku ya uhuru (Ushindi juu ya Argentina)
14 Juni 1982
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
12,173 km² (162)
0
Idadi ya watu
 - Julai 2008 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
3,140 [1] (217)
0.26/km² (240)
Fedha Falkland Islands pound (FKP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-4)
(UTC-3)
Intaneti TLD .fk
Kodi ya simu +500Christchurch Cathedral, Stanley
Nyumba ya mkulima nyikani za Falkland

Visiwa vya Falkland (Kiingereza: Falkland Islands au Kihispania Islas Malvinas) ni funguvisiwa katika bahari ya Atlantiki ya kusini takriban 450 km mbele ya pwani la Argentina.

Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza linalodaiwa na Argentina kama sehemu yake.

Funguvisiwa ina takriban visiwa 200. Viwili ambavyo ni vikubwa ni Falkland Magharibi na Falkland Mashariki na kila kimoja huwa na eneo la takriban 6,000 km². Mwinuko mkubwa ni mlima wa Mount Usborne (Kihispania: Cerro Alberdi) mwenye 708 mita juu ya uwiano wa bahari.

Hali ya hewa ni baridi na kuna mvua nyingi. Halijoto ya wastani ni 5 °C pekee. Kwa sababu hii mimea ni hasa manyasi; kutokana na baridi miti haizidi kimo cha mita 1.

Idadi ya wakazi haizidi 3,000 na wote hao ni Waingereza wanaosema Kiingereza. Wanajipatia riziki yao kwa uvuvi na ufugaji wa kondoo. Mji wa pekee ambao ni pia makao makuu ya utawala ni Port Stanley kwenye kisiwa cha mashariki mwenye wakazi 2100. Pamoja na wakazi kuna wanajeshi Waingereza 1,500. Barabara ya lami ya pekee kisiwani inayounganisha Stanley na kituo cha kijeshi kwa umbali wa kilomita 50.

Argentina inadai ya kwamba visiwa ni eneo lake na 1982 jeshi la Argentina ilivamia visiwa vikuu. Uingereza ilijibu kivita ikapeleka wanajeshi huko na baada ya vita fupi ya wiki 6 Argentia ilishindwa; takriban wanajeshi 1000 waliuawa.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Falkland Islands (Islas Malvinas). CIA. Iliwekwa mnamo 2010-03-05.