Elizabeth II wa Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Elisabeth II 2006

Elisabeth II ni malkia wa Uingereza (au Ufalme wa Muungano) tangu 1952. Alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor tar. 21 Aprili 1926 mjini London kama mtoto wa kwanza wa mfalme Georg VI na Elizabeth Bowes-Lyon.

Kama mkuu wa Jumuiya ya Madola yeye ni pia mkuu wa dola wa nchi zifuatazo n´dani ya jumuiya hii:

Alitangazwa kuwa malkia tar. 6 Februari 1952 mara moja baada ya kifo cha babake George VI. Wakati ule alikuwa akitembelea Kenya iliyokuwa bado koloni ya Uingereza akatembelea milima ya Aberdares.

Alipokea taji katika ibada rasmi tar. 2 Juni 1953 kwenye kanisa la Westminster Abbey.

Katika nchi zote anaposhika cheo hana mamlaka ya kiserikali anatawala kama mfalme wa kikatiba katika muundo wa serikali ya kibunge.