Kihispania
Kihispania Español Castellano |
|
---|---|
Lugha | |
Asili | Uhispania Puerto Rico Argentina, Bolivia, Chile, Colombia, Costa Rica, Cuba, Jamuhuri ya Dominican , Ecuador, El Salvador, Guinea ya Ikweta, Guatemala, Honduras, Meksiko, Nicaragua, Panama, Paraguay, Peru, Uruguay, na Venezuela. |
Wasemaji |
L1 : 500 Milioni |
Familia za lugha | Kihindi-Kiulaya Kilatini |
Aina za Awali | Kilatini ya kawaida Kihispania cha Kale |
Mfumo wa kuandika | Kilatini |
Nambari za Msimbo | |
ISO 639-1 | es |
ISO 639-2 | spa |
Glottolog | stan1288 |
![]() Lugha ya Kwanza kwa wengi Lugha Rasmi au Lugha ya Pili Asilimia 20% kwenda juu |
Kihispania (español) au Kicastilia (castellano) ni lugha ya Kiromansi kutoka familia ya lugha za Kihindi-Kiulaya, ambayo ilitokana na Kilatini cha Kawaida kilichozungumzwa katika Rasi ya Iberia huko Ulaya. Leo hii, ni lugha ya kimataifa yenye takriban wasemaji wa asili milioni 484, hasa katika Amerika na Hispania, na takriban milioni 558 wakiwemo wasemaji wa lugha ya pili. Kihispania ni lugha rasmi ya nchi 20, na pia ni moja ya lugha rasmi sita za Umoja wa Mataifa. Kihispania ni lugha ya pili duniani kwa idadi ya wasemaji wa asili baada ya Kichina cha Mandarin; lugha ya nne kwa idadi ya wasemaji duniani baada ya Kiingereza, Kichina cha Mandarin, na Hindustani (Kihindi-Kiurdu); na ndiyo lugha maarufu zaidi ya Kiromansi duniani. Nchi yenye idadi kubwa ya wasemaji wa asili ni Mexico.
Historia ya lugha
[hariri | hariri chanzo]Asili ya lugha hiyo ni katika nchi ya Uhispania (Ulaya kusini magharibi), lakini kutokana na historia ya ukoloni na ya biashara lugha hiyo imesambaa sana, hasa Amerika ya Kusini na ya Kati.
Lugha iliyozaa Kihispania ni Kilatini cha Waroma wa Kale waliotawala kwa muda mrefu Uhispania. Ndiyo sababu maneno yake yanatokana na Kilatini kwa asilimia 80, lakini pia na Kiarabu kwa asilimia 8.
Kati ya lugha za Kirumi Kihispania ni lugha ya kisasa ambayo ni karibu zaidi na lugha ya kale, isipokuwa Kisardinia na Kiitalia.
Nchi zinazotumia Kihispania kama lugha rasmi
[hariri | hariri chanzo]- Costa Rica
- Cuba
- El Salvador
- Jamhuri ya Dominika
- Guatemala
- Honduras
- Mexico
- Nicaragua
- Panama
- Puerto Rico
Afrika
[hariri | hariri chanzo]Nchi zenye wasemaji wengi wa Kihispania
[hariri | hariri chanzo]- Nchini Marekani Kihispania ni lugha ya pili baada ya Kiingereza hasa katika majimbo ya Kusini zilizokuwa zamani sehemu za Mexiko.
- Ufilipino kwa sababu ilikuwa koloni la Uhispania
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- makala za OLAC kuhusu Kihispania Ilihifadhiwa 12 Mei 2015 kwenye Wayback Machine.
- lugha ya Kihispania katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/spa
- Free SPANISH LANGUAGE course by email
- Ramani za Matamshi ya Lahaja ya Kihispania
- Lugha isiyo rasmi ya Kihispania
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Lugha za Kirumi
- Lugha za Hispania
- Lugha za Costa Rica
- Lugha za Cuba
- Lugha za El Salvador
- Lugha za Jamhuri ya Dominika
- Lugha za Guatemala
- Lugha za Honduras
- Lugha za Meksiko
- Lugha za Nicaragua
- Lugha za Panama
- Lugha za Puerto Rico
- Lugha za Argentina
- Lugha za Bolivia
- Lugha za Chile
- Lugha za Colombia
- Lugha za Ecuador
- Lugha za Guyana
- Lugha za Paraguay
- Lugha za Peru
- Lugha za Uruguay
- Lugha za Venezuela
- Lugha za Guinea ya Ikweta
- Lugha