Guatemala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Guatemala


Guatemala (pia Gwatemala; kutoka lugha ya Kinahuatl Cuauhtēmallān, "kwenye miti mingi") ni nchi ya Amerika ya Kati. Inapakana na Bahari ya Pasifiki upande wa Magharibi, na Atlantiki upande wa Mashariki, tena na nchi za Mexiko, Belize, Honduras na El Salvador.

Kanisa la San Andrés Xecul.

Eneo lake ni km2 108,889 ambamo wanaishi watu 17,980,803 (2023).

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi (56%) ni machotara waliotokana na Waindio na Wazungu au watu wenye asili ya Ulaya tu. Waindio wenyewe ni 43.4%.

Lugha rasmi na inayotumika zaidi (69.9%) ni Kihispania, lakini zipo pia nyingine 23 za wakazi asili.

Upande wa dini, wakazi wengi ni wafuasi wa Yesu katika Kanisa Katoliki (45%) na madhehebu mengine ya Ukristo, hasa ya Uprotestanti (42%). Asilimia 11 hawana dini.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guatemala kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.