St. Pierre na Miquelon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Saint Pierre and Miquelon)
Saint-Pierre et Miquelon
Bendera ya Saint-Pierre na Miquelon Nembo la Saint-Pierre na Miquelon
Wito: A mare labor (Kazi kutoka bahari)
Lugha rasmi Kifaransa
Mji Mkuu St. Pierre
Rais wa Halmashauri Kuu Stéphane Artano
Mkuu wa Mkoa (Préfet) Albert Dupuy
Eeno
 – Jumla
 – % maji

 242 km²
 0.0%
Idadi ya wakazi
 – Jumla (2011)

 6,080
Pesa Euro (€;EUR)
Jamla la pato la eneo
(Wanazaa kiasi gani cha mali kwa mwaka)
$48.3 Millioni
Kanda la saa UTC-3
Simu ya eneo 508 ¹
Intaneti TLD .pm
1. 0508 kutoka Ufaransa bara.
Stpierremap.png
Miquelon
Ramani

Saint-Pierre na Miquelon ni funguvisiwa na eneo la ng'ambo la Ufaransa (kwa Kifaransa "Collectivité d'outre mer") karibu na pwani ya Kanada katika bahari ya Atlantiki.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Funguvisiwa iko karibu na jimbo la Newfoundland ya Kanada.

Visiwa vikubwa zaidi ni Saint-Pierre (km² 26), Miquelon (km² 110), Langlade (km² 91) halafu kuna visiwa vingine vidogo. Jumla la eneo ni km² 242 lenye wakazi 6,080, hasa kisiwani Saint-Pierre (5,456).

Karibu wote wanaongea Kifaransa na ni waamini wa Kanisa Katoliki.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Visiwa vimetembelewa na wavuvi kutoka Ulaya tangu karne ya 15.

Inaaminiwa ya kwamba makazi ya kwanza ya kudumu ya wavuvi Wafaransa yalianzishwa katika karne ya 17.

Tangu vita ya miaka saba visiwa hivi vilikuwa mabaki pekee ya koloni la Kanada ya Kifaransa.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi umetegemea tangu mwanzo uvuvi. Siku hizi kuna pia utalii.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa visiwa ni raia wa Ufaransa. Huchagua bunge lao lenye watu 19. Bunge la eneo linamchagua mwakilishi mmoja katika bunge la kitaifa la Ufaransa.

Saint-Pierre na Miquelon si sehemu ya Eneo la forodha la Ulaya.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.