Dominica

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kisiwa cha Dominica
Dominica


Ramani ya Dominica.

Dominica (pia Dominika) ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi. Haitakiwi kuchanganywa na Jamhuri ya Dominika ambayo ni nchi nyingine katika Karibi.

Nchi ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola, lakini ni jamhuri.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina limetokana na lugha ya Kilatini na linamaanisha „Jumapili“ kwa sababu Kristoforo Kolumbus alifika huko mara ya kwanza siku ya Jumapili tarehe 3 Novemba 1493.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kina urefu wa km 46.4 na upana wa km 25.6; eneo lake ni km² 746.

Mlima mkubwa ni volkeno ya Morne Diablotins yenye kima cha m 1,447 juu ya UB.

Kuna misitu mingi na maeneo ya kuhifadhiwa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Dominica ilikuwa kati ya visiwa vya mwisho katika Karibi vilivyotekwa na Wazungu kutokana na utetezi mkali wa wenyeji Waindio. Ni pia mahali pa mwisho ambako bado wako Wakaribi (3,000) waliopotea penginepo kwenye visiwa vya Karibi.

Tabia ya kisiwa kuwa na milima mingi ilifanya isionekane ni mahali pazuri pa kilimo ya mashamba makubwa. Hivyo mataifa yaliyounda makoloni kwa muda mrefu hayakuvutwa kulipa gharama za kupeleka wanajeshi wengi kisiwani waliohitajika kukandamiza Waindio.

Hispania iliacha majaribio ya kuteka kisiwa katika karne ya 16.

Uingereza ilijaribu kuunda utawala wake juu ya kisiwa mwaka 1627 ikaacha.

Mwaka 1635 Ufaransa ilipeleka bendera yake Dominica lakini ikaacha pia.

Tangu mwaka 1748 Uingereza na Ufaransa walipatana ya kwamba kisiwa kitakuwa eneo lisilotawaliwa na upande mmoja.

Katika miaka iliyofuata walowezi wachache Wafaransa walianzisha mashamba na mji wa Roseau.

Baada ya vita ya miaka saba Uingereza ulichukua utawala wa kisiwa na kupeleka huko walowezi pamoja na watumwa kutoka Afrika. Waindio walirudishwa polepole katika maeneo ya milimani.

Uhuru ulipatikana tarehe 3 Novemba 1978.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Miji mikubwa zaidi kisiwani ni:

  • 1. Roseau: wakazi 16,571
  • 2. Portsmouth: wakazi 3,633
  • 3. Marigot: wakazi 2,669
  • 4. Berekua: wakazi 2,608
  • 5. Mahaut: wakazi 2,369
  • 6. Saint Joseph: wakazi 2,184

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa wakazi 75% wana asili ya Afrika na 19.2% ni machotara.

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wengine wanazungumza Krioli zinazotegemea Kifaransa au Kiiingereza.

Upande wa dini, 80% ni Wakatoliki, 10-12% ni madhehebu ya Kisabato, 3% wanafuata dini za jadi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Dominica kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.