Kosta Rika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kosta Rika
Ramani ya Kosta Rika.

Kosta Rika (kwa Kihispania: Costa Rica, yaani Pwani Tajiri) ni nchi ya Amerika ya Kati.

Imepakana na Nikaragua na Panama; kuna pwani ya Pasifiki upande wa magharibi na pwani ya Bahari ya Karibi upande wa mashariki.

Kosta Rika ilikuwa nchi ya kwanza duniani ya kufuta jeshi lake kikatiba. Pia inaongoza kwa kuhifadhi mazingira.

Mji mkuu ni San José.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kufika kwa Wahispania katika karne ya 16, nchi ilikaliwa na Waindio wachache.

Mwaka 1821 koloni hilo lilijiunga na ghasia ya maeneo mengine ya Amerika ya Kati dhidi ya utawala wa Hispania.

Mwanzoni nchi hizo ndogo zilijiunga na Meksiko lakini baada ya miaka miwili zilianzisha "Shirikisho la Amerika ya Kati" lililokwisha mwaka 1839.

Tangu mwaka 1847 Kosta Rika imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.

Mwaka 1948 kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo viliwahi kwisha. Mwaka uliofuata nchi ilifuta kabisa jeshi hadi leo[1][2][3].

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi (65.8%) wana asili ya Ulaya, mbali ya machotara Wazungu-Waindio (13.65%) na wahamiaji wenye asili yoyote (9.03%). Waindio, ambao ndio wakazi asili, ni 2.4% tu.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.

Upande va dini, walio wengi ni wafuasi wa Yesu katika Kanisa Katoliki (70.5%: ndiyo dini rasmi) au madhehebu ya Uprotestanti (13.08%). Nje ya Ukristo, unaongoza Ubuddha (2.3%).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. El Espíritu del 48. "Abolición del Ejército" (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 9 March 2008.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Costa Rica". World Desk Reference. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 February 2008. Iliwekwa mnamo 9 June 2009.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. "Costa Rica". Uppsala University. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-10. Iliwekwa mnamo 9 June 2009.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kosta Rika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.