Nenda kwa yaliyomo

Antigua na Barbuda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Antigua and Barbuda
Bendera ya Antigua na Barbuda Nembo ya Antigua na Barbuda
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Each Endeavouring, All Achieving (Jaribu kila kitu, Faulu kila kitu)
Wimbo wa taifa: Fair Antigua, We Salute Thee (Antigua mzuri twakusalimu)
Wimbo wa kifalme: God Save the Queen1
Lokeshen ya Antigua na Barbuda
Mji mkuu Saint John's
17°7′ N 61°51′ W
Mji mkubwa nchini Saint John's
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Ufalme wa Kikatiba
Charles III wa Uingereza
Rodney Williams
Gaston Browne
Uhuru
kutoka Uingereza

1 Novemba 1981
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
440 km² (ya 182)
--
Idadi ya watu
 - 2020 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
100,772 (ya 182)
186/km² (57)
Fedha East Caribbean dollar (XCD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
AST (UTC-4)
ADT (UTC-3)
Intaneti TLD .ag
Kodi ya simu +268

-

1 God Save The Queen ni kama wimbo la taifa lakini hutumiwa tu kwenye nafasi za kifalme.


Ramani ya Antigua na Barbuda
Bandari ya maboti Antigua

Antigua na Barbuda ni nchi ya visiwani ya Amerika kwenye bahari ya Karibi. Ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola.

Inaundwa na visiwa viwili vya Antigua na Barbuda vinavyokaliwa na watu pamoja na visiwa vingine vidogo kama cha Redonda visivyo na wakazi.

Antigua na Barbuda ni sehemu ya funguvisiwa la Antili Ndogo pamoja na Guadeloupe, Dominica, Martinique, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadini, Barbados, Grenada, Trinidad na Tobago upande wa kusini halafu Montserrat, Saint Kitts na Nevis, Saint Barthélemy, Saint Martin na Anguilla upande wa magharibi.

Idadi ya wakazi ni watu 100,772 (2020). Wengi wao hukaa Antigua. Barbuda ina watu 1,638 tu.

Walio wengi sana (91 %) wametokana na watumwa kutoka Afrika waliopelekwa hapa wakati wa ukoloni, lakini kuna mchanganyiko mkubwa wa damu.

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wengi wanazungumza Krioli na 10,000 hivi Kihispania, hasa wahamiaji.

Upande wa dini, 92.7% ni Wakristo, hasa Waanglikana (17.6%), wakifuatwa na Waadventista Wasabato, Wapentekoste, Wamoravian, Wamethodisti, Wakatoliki, Wabaptisti n.k. Wengine ni Rastafari (3.6%), Baha'i (1.1%) n.k.

Nchi hufuata utaratibu wa ufalme wa Kikatiba. Mkuu wa dola ni mfalme Charles III wa Uingereza anayewakilishwa na Gavana Mkuu.

Serikali imo mikononi mwa waziri mkuu anayetegemea kura za bunge.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Antigua na Barbuda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.