Barbados

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Barbados

Barbados ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi takriban 430 km kaskazini - mashariki kwa Venezuela (Amerika Kusini).

Nchi jirani za karibu kuvukia bahari ni Saint Lucia na Saint Vincent upande wa magharibi, Trinidad na Tobago upande wa kusini na Grenada upande wa kusini-magharibi.

Barbados ni kisiwa cha Antili Ndogo. Kwa urefu kinafikia km 34 na kwa upana 23.

Wakazi ni 277,821, na kwa asilimia 91 wana asili ya Afrika, 4% ya Ulaya, 1% ya India.

Lugha rasmi ni Kiingereza, ingawa wakazi wengi kabisa wanaongea kwa kawaida aina ya Krioli inayoitwa Kibajan.

Upande wa dini, 75.6% ni Wakristo, hasa Waanglikana (23.9%) na Wapentekoste (19.5%). Dini nyingine kwa pamoja zinafikia 3%, kwa kuwa 21% hawana dini yoyote.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Barbados kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.