Saint-Barth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Saint Barthélemy)
Ramani ikionyesha St. Barth kati ya Saint Martin na St Kitts.
Pwani ya St. Barth.

Saint-Barth (jina rasmi la Kifaransa ni Collectivité territoriale de Saint-Barthélemy) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa.[1] Jina la awali lilikuwa Ouanalao, halafu likapewa jina la Mtume Bartholomayo.[2] St. Barth ni kisiwa chenye asili ya volkeno ambacho kipo kati ya Saint Martin na St. Kitts.[3]

Ukubwa wake ni kilometa mraba 25.

Kuanzia mwaka 2003 hakipo tena chini ya Guadeloupe.

Wakazi ni 9,035 (kadirio la Januari 2011).

Makao makuu yako Gustavia, ilipo bandari kuu ya kisiwa.

Lugha na utamaduni ni vya Kifaransa hasa, kwa kuwa wakazi wengi wana asili hiyo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. The World Fact Book. Government. CIA Fact Book. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-29. Iliwekwa mnamo 8 January 2011.
  2. R. P. Raymond BRETON. Dictionnaire caraïbe-françois, Auxerre, Chez Gilles Bouquet, 1665.
  3. The World Fact Book. Geography. CIA Fact Book. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-29. Iliwekwa mnamo 8 January 2011.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Historia na biolojia
Taarifa za jumla
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Saint-Barth kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Coordinates: 17°54′N 62°50′W / 17.900°N 62.833°W / 17.900; -62.833