Wamethodisti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wamethodisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanaozingatia mafundisho ya John Wesley ambaye katikati ya karne ya 18 alianzisha uamsho katika ushirika wa Anglikana akisaidiana na mdogo wake Charles na George Whitefield.

Mapema makleri wengi wa Anglikana walijiunga nao wakaitwa Methodists.

Ni baada ya kifo cha John Wesley tu kwamba wao wakawa madhehebu ya kujitegemea.

Kupitia umisionari wa nguvu Umethodisti ulienea katika Dola la Uingereza, Marekani na kwingine.

Kwa sasa wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 70 duniani kote.

Karibu jumuia zao zote zinaunda pamoja kiungo cha mashauriano kinachoitwa World Methodist Council, chenye makao makuu huko Lake Junaluska, North Carolina, Marekani.

Hata hivyo Umethodisti una tofauti kubwa ndani yake upande wa mafundisho, ibada n.k.