Wakatoliki wa Kale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kanisa kuu la Mt. Gertrude huko Utrecht, Uholanzi. Ni mama wa makanisa yote ya Wakatoliki wa Kale.

Wakatoliki wa Kale ni jina linalotumika kujumlisha Wakristo wa Magharibi ambao wametengana na Askofu wa Roma hasa baada ya Mtaguso wa kwanza wa Vatikano (1869-1870) kutangaza dogma ya Papa kutoweza kukosea anapotamka rasmi jambo fulani kama fundisho la kudumu moja kwa moja.

Wakristo hao walijipatia uaskofu halisi katika mlolongo wa Mitume kupitia Askofu wa Utrecht mwaka 1873, na baada ya hapo waliusambaza kwa madhehebu mengi, ambayo mengine kwa sasa hayana ushirika nao.

Imani na liturujia zao zinafanana na zile za Kanisa Katoliki, lakini taratibu zimekwenda mbali.

Baadhi ya Makanisa ya namna hiyo yanaunda "Umoja wa Utrecht" ulioanzishwa mwaka 1889 na kuwa na waamini 115,000 duniani mwaka 2013.

ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakatoliki wa Kale kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.