Dogma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Neno dogma linatumika hasa kumaanisha fundisho la imani lisiloweza kukanushwa na wafuasi wa dini fulani. Linaweza kutumika pia kwa maana isiyo ya kidini.

Asili ya neno[hariri | hariri chanzo]

Dogma ni leno la Kigiriki (δογμα, dògma) linalotokana na kitenzi δοκω, doko. Maana zake zilikuwa tatu:

1. rai;

2. wazo, fundisho la falsafa au dini;

3. uamuzi, tamko.

Ndiyo sababu "dogma ya Kanisa" inamaanisha tamko lililotolewa na Mtaguso au Papa kumalizia mjadala kuhusu fundisho fulani baada ya kuthibitisha ufunuo wa Mungu unasema nini juu ya hilo.

Baada ya hapo, mwamini anayekataa dogma anahesabiwa kuwa mzushi na kutengwa na Kanisa.