Kigiriki
|
Kigiriki (pia: Kiyunani) ni lugha ya Kihindi-Kiulaya inayotumiwa hasa nchini Ugiriki. Maandishi yake yamejulikana tangu miaka 3500 iliyopita. Hakuna lugha nyingine duniani inayozungumzwa hadi leo yenye historia ndefu kuliko hii, isipokuwa Kichina.
Kigiriki ni muhimu sana kwa utamaduni wa kisasa kwa sababu ya kutoa michango mingi kwa lugha ya sayansi, teknolojia na utamaduni. Fikra nyingi muhimu zilionekana mara ya kwanza kwa Kigiriki na falsafa iliyojadiliwa na kuandikwa kwa lugha hii. Istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kigiriki.
Alfabeti ya Kigiriki ilikuwa msingi wa alfabeti nyingine mbili, za Kilatini na Kisirili, pia kwa miandiko ya abijadi kama herufi za Kiarabu au za Kiebrania. Kiswahili huandikwa leo kwa herufi za Kilatini.
Kati ya maandiko muhimu ya Kigiriki ni yale ya wanafalsafa kama Plato na Aristoteles na pia baadhi ya maandiko ya Biblia ya Kikristo (Agano Jipya pamoja na Deuterokanoni), mbali ya tafsiri ya kwanza ya Biblia ya Kiebrania maarufu kwa jina la Septuaginta (karne ya 2 KK).
Kati ya karne ya 3 KK hadi karne ya 6 BK Kigiriki kilikuwa lugha ya kimataifa katika eneo kubwa la kandokando ya bahari ya Mediteranea pamoja na Mashariki ya Kati.
Lugha imeendelea kubadilika kisarufi, kimatamshi na pia kimsamiati. Hivyo Kigiriki cha kale kimekwisha, hakizungumzwi tena na watu, lakini bado kinafundishwa katika shule na vyuo vingi, hasa Ulaya.
Leo hii katika nchi ya Ugiriki kuna lugha ya Kigiriki Kipya kinachoendela kuandikwa kwa herufi zilezile.
Ulingano wa Kigiriki cha Kale na cha Kisasa
[hariri | hariri chanzo]Kigiriki cha Kisasa | Kigiriki cha Kale |
---|---|
1 Στην αρχή ήταν ο Λόγος, και ο Λόγος ήταν προς τον Θεό(ν), και Θεός ήταν ο Λόγος. | 1 Ἐν ἀρχῇ ἦν ὁ Λόγος, καὶ ὁ Λόγος ἦν πρὸς τὸν Θεόν, καὶ Θεὸς ἦν ὁ Λόγος. |
/stin ar'khi 'itan o 'logos ke o 'logos 'itan pros ton thi'o ke thi'os 'itan o 'logos/ | /en ar'khe en o logos kaí o lógos en prós tón the'on kaí the'os en o lógos/ |
Kwa Kiswahili: Hapo mwanzo, kulikuwa na Neno; naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. (Injili ya Yohane, 1,1) |
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- makala za OLAC kuhusu Kigiriki Ilihifadhiwa 29 Juni 2015 kwenye Wayback Machine.
- lugha ya Kigiriki katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/ell
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kigiriki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |