Plato

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sanamu ya kichwa cha Plato

Plato (Kigiriki: Platon) alikuwa kati ya wanafalsafa muhimu zaidi wa Ugiriki ya Kale. Aliishi kati ya 427 KK hadi 347 KK. Alikuwa mwanafunzi wa Sokrates na mwalimu wa Aristoteles.

Alibuni mawazo mengi yenye maana hadi leo. Wanafalsafa wa kisasa wamesema ya kwamba falsafa yote inamtegemea Plato.

Aliandika mafundisho yake kwa umbo la majadiliano - yaani watu wawili au zaidi wanajadili mawazo wakikubaliana au kutokubaliana. Kwa njia hii Plato alipenda kueleza fikra zake.

Mara nyingi Sokrates ni msemaji mkuu katika majadaliano ya Plato. Huonyeshwa akiwauliza watu juu yale wanachoamini akiendelea kuuliza maswali kama mawaza yao yanalingana na mantiki. Haieleweki ni kiasi gani ya kwamba Plato alitumia kweli mafundisho ya Sokrates mwenyewe au kama alimtumia zaidi kwa njia ya kifasihi akieleza fikra zake Plato kupitia mdomo wa Sokrates wa majadiliano.

Kati ya maandiko muhimu ya Plato ni "Politeia" yaani "kuhusu dola".

Dhana na vitu[hariri | hariri chanzo]

Katika falsafa ya Plato kuna tofauti muhimu kati ya dhana na kitu. Dunia ya kweli ni dunia ya dhana. Vitu ni

(inaendelea)