Maandishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mitindo ya maandishi duniani
buluu: alfabeti ya Kilatini; kibichi: alfabeti ya Kiarabu; nyekundu: Kikirili; njano: mwandiko wa Kichina; kichungwa: miandiko ya Kihindi

Maandishi (pia: mwandiko) ni tendo la kushika sauti za lugha kwa njia ya alama zinazoandikwa.

Mitindo ya miandiko[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya maandishi duniani inatumia alfabeti mbalimbali na kati yao alfabeti ya Kilatini imesambaa zaidi ikifuatwa na alfabeti ya Kiarabu na alfabeti ya Kikirili.

Asia ya Mashariki imeendelea kutumia maandishi yake ya alama zinazoonyesha neno lote badala ya herufi tu. Mtindo wa kutumia alama kwa neno lote ulitumiwa pia katika tamaduni za Misri ya Kale au Meksiko ya Kale.

Miandiko ya Uhindi inayotokana na mwandiko wa Brahmi hutumia miandiko mbalimbali inayoonyesha silabi. Hata lugha za Ethiopia hufuata mtindo wa kufanana nayo.

Sanamu ya mwandishi (Misri ya Kale)

Historia ya maandishi[hariri | hariri chanzo]

Hakuna uhakika maandishi yalianza lini na wapi duniani. Wataalamu wengi huona ya kwamba Sumer katika Mesopotamia ilikuwa na maandishi ya kwanza duniani.

Wengine huona ya kwamba sanaa ya kuandika ilianzishwa na watu mbalimbali kwa nyakati tofauti katika pande mbalimbali za dunia. Si rahisi kuwa na uhakika kwa sababu maandishi yenyewe hudumu kwa muda tu kutegemeana na mata na vifaa vilivyotumiwa.

Maandishi kwenye mawe magumu tena penye hali ya hewa yabisi hukaa miaka maelfu. Kwa njia hii tuna ushuhuda wa maandishi ya mapema hasa kutoka nchi kama Mesopotamia, Misri, Bara Hindi na China. Lakini hatuwezi kukana uwezekano wa maandishi yaliyotumia mata kama magome ya miti yanayooza haraka hasa katika mazingira penye mvua nyingi.

Watu waliandika juu ya miamba, matofali, bao za nta, kitambaa, ubaoni au mabati ya metali mbalimbali. Mainka wa Peru walitumia mwandiko wa mafundo kwenye kamba.

Kati ya mata zote za kutunza maandishi ni hasa karatasi inayotumiwa zaidi. Ilibuniwa China inapojulikana mnamo mwaka 100 BK na kusambaa polepole Asia halafu Ulaya.

Siki hizi maandishi ya elektronia yameanza kusambaa pamoja na matumizi ya tarakilishi na mtandao.


Tazama pia[hariri | hariri chanzo]