Tarakilishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Tarakilishi au Kompyuta ni mashine inayopokea habari na kuzishughulikia kulingana na kanuni za programu inayopewa. Inafuata hatua za mantiki katika kazi hii.

Yaliyomo

Historia ya Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Tarakilishi inatafsiriwa na hatua za kimaendeleo ya Tarakilishi. Ni hatua ambazo Tarakilishi imepitia toka aina ya kizamani hadi aina ya kisasa. Hatua hizi zinachukuliwa kama vizazi vya Tarakilishi.

Kimsingi Tarakilishi ni kifaa chochote kinachomsaidia binadamu kufanya hesabu. Zipo Tarakilishi za aina mbili, Tarakilishi ambazo ni Analojia (ya umakanika) na Tarakilishi ambazo ni Dijitali (ya elektroniki).

Hatua kabla ya vizazi vya Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Tarakilishi za Analojia (hazitumii umeme) ndizo ambazo zilianza kabla ya Tarakilishi za Dijitali (zinatumia umeme).

Tarakilishi za Analojia ni vifaa vinavyosaidia kufanya hesabu vikiendeshwa kwa mtangamano wa moja kwa moja na vidole. Mifano ya Tarakilishi hizi ni kama vile Fito za Kuhesabia, Fimbo za Hesabu, na kadhalika.

Calculi kilikuwa kifaa kitumikacho kuhifadhi hesabu. Vitu kama Pia, Tufe Mfinyanzi, na kadhalika vinafungwa kwenye kopo kuwakilisha hesabu pengine ya wanyama wafugwao au nafaka.

Suanpan (Namba zinazowakilishwa kwenye Abakusi hii ni 6,302,715,408)

Abakusi ni aina nyingine ya Tarakilishi analojia, ambayo ni kibao maalum chenye shanga zilizovikwa kwenye fito kinachotumika kusaidia hesabu za kujumlisha na kutoa.

Kila Tarakilishi, kwa namna tofautitofauti, inahimili kitendo cha Pembejeo, Mchakato, na Zao. Yaani, kila Tarakilishi inaweza kupokea data (habari), kufanya mchakato na kutoa majibu ya zile habari zilizochakatwa katika mtindo wa taarifa.

Kitendo Pembejeo-Mchakato-Zao (Input-Process-Output) cha Abakusi kwa kawaida kabisa ni tendo la kusogeza shanga mahali kupya (pembejeo), Kuhesabu zile shanga zilizojitenga na nyingine (mchakato), na kuziona shanga jinsi ambavyo zimejitenga na nyingine ni Zao.

Mifano mingine ya Tarakilishi analojia ambazo zilitengenezwa kitaalamu zaidi, ni kama vile Automata na Programmable cart, hizi zilitengenezwa na Shujaa wa Alexandria miaka ya 10 – 70 Baada ya Kristo (AD).

Planisphere ilivumbuliwa na Abū Rayhān al-Bīrūnī miaka ya 1000 Baada ya Kristo (AD).

Kulikuwa na Tarakilishi analojia ambazo ziliundwa kwa sababu ya kufanya hesabu za falaki, ni kama zifuatazo, Antikythera mechanism na astrolabe kutoka Ugiriki wa kale miaka ya 100150 Kabla ya Kristo.

Equatorium na Universal Latitude-independent Astrolabe zilivumbuliwa na Abū Ishāq Ibrāhīm al-Zarqālī mnamo 1015 baada ya Kristo.

Seti ya majedwali kokotozi ya John Napier kutoka miaka ya 1680

Astronomical Clock Tower ilivumbuliwa na Su Song miaka ya 1090 BK wakati wa kipindi cha utawala wa kinasaba wa mfalme Song.

John Napier alihitaji kufanya mahesabu mengi ya kuzidisha wakati akitengeneza Chati ya Logi ya kwanza. Katika kipindi hicho akavumbua Tarakilishi analojia iitwayo Napier’s Bones. Napier’s Bones ipo kama Abakusi lakini hii ilitumika kufanya hesabu za kuzidisha na kugawanya.

Rula Mtelezo (Slide rule) ilivumbuliwa mwaka 1620. Hii ni Tarakilishi analojia iwezeshayo hesabu za kuzidisha na kuganya zifanyike kwa wepesi na haraka zaidi ukilinganisha na ilivyokuwa hapo nyuma. Hapa namba halisi zinawakilishwa kama umbali au nafasi baina ya vituo viwili katika mstari mnyofu. Rula Mtelezo ilikua ikitumiwa na vizazi vya wahandisi na wataalamu wa hesabu mpaka kilipokuja kuvumbuliwa Kikokotoo cha Mfukoni.

Muonekano nyuma ya Pascal's calculator. Pascal alivumbua huu mtambo mwaka 1642.

Mwaka 1645, Blaise Pascal, msomi kutoka Ufaransa, alivumbua Kikokotoo analojia na kukipa jina Pascal’s Calculator au Pascaline. Hiki ni chombo cha kufanyia hesabu, ambacho alikitengeneza kwa ajili ya kumsaidia baba yake katika kazi za hesabu, lakini hakikuwa na sifa bora kama ilivyotakiwa.

Mnamo 1672, Gottfried Wilhelm von Leibniz alivumbua Kikokotoo analojia kiitwayo Stepped Reckoner. Pia ndie mvumbuzi wa Mche Duara wenye gia nyingi zilizopangiliwa kitaalamu ambao ulikuja kupata umaarufu kwa kutumika zaidi katika miundo ya Tarakilishi analojia zilizofuata. Stepped Reckoner ni maboresho ya Pascaline ambapo sasa ikawa inafanya hesabu za kuzidisha na kugawanya moja kwa moja.

Miaka ya 1820 Charles Xavier Thomas de Colmar alivumbua Kikokotoo analojia kiitwacho Thomas Arithmometer, ambacho kilizalishwa na kuuzwa kwa wingi zaidi. Thomas Arithmometer kilikuwa sehemu kubwa ya kazi ya Leibniz.

Mwaka 1903, Ryōichi Yazu wa Japani aliiweka dhahiri Yazu Arithmometer. Hiki ni Kikokotoo analojia kilichotumia Mche Duara mmoja wenye gia ishirini na mbili (22), ambacho kilifanya hesabu mchanganyo katika mpango wa namba wa kizio cha pili na wa kizio cha tano. Hizi hesabu ni mashuhuri kwa watumiaji wa Soroban (Abakusi ya Kijapani).

Kikokotoo Curta kinaweza pia kufanya hesabu za kuzidisha na kugawanya.

Vikokotoo analojia kama vile Addiator yenye kufanya hesabu za kizio cha kumi, Comptometer, Monroe, Curta na Addo-X zilitumika mpaka miaka ya 1970.

Kikokotoo cha mezani cha kwanza kabisa kilichotumia umeme kilikuwa cha Uingereza kilichoitwa ANITA MK.VII

Mwezi Juni 1963 Friden aliitambulisha Tarakilishi ya kazi-nne EC-130. Ilitumia transista katika muundo wake na ilikuwa na skrini ya inchi 15 yenye uwezo wa kuonesha mpaka tarakimu kumi na tatu (13).

Tarakilishi toleo EC-132 iliweza kufanya hesabu za Kipeo cha Pili pamoja na hesabu zitumiazo Namba Tegemezi zitumikazo katika hesabu za kinyume katika kuzidisha.

Mwaka 1965, Maabara za Wang zilitengeneza Kikokotoo cha mezani kilichoitwa LOCI-2. Kikokotoo hiki kilitumia transista katika muundo wake na kiliweza kuonesha mpaka tarakimu kumi katika skrini yake. LOCI-2 iliweza kufanya hesabu za Logi.

Teknolojia ya Panchi Kadi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1801 Joseph-Marie Jacquard alitengeneza Kitanda Cha Mfumi ambapo bombwe iliyokuwa ikifumwa iliongozwa na Panchi Kadi.

Mfululizo wa Kadi unaweza kubadilishwa bila kubadilisha mfumo mzima wa umakanika wa Kitanda Cha Mfumi. Hii ilikua ni hatua muhimu ya mafanikio katika uandishi wa programu.

Mtambo wa hesabu kutoka IBM utumiao panchi kadi, ulipigwa picha mwaka 1936

Charles Babbage mara nyingi anafikiriwa kama mwasisi wa vifaa vya Tarakilishi za kisasa. Mwanzoni mwa miaka ya 1810 Babbage alipata maono ya hesabu za namba na chati zitakazofanywa kimashine.

Kuifanya ndoto yake kuwa kweli, Babbage akabuni Kikokotoo cha kufanya hesabu za namba zenye mpaka nafasi za desimali nane (8).

Kutokana na mafanikio ya wazo lake hili, mwaka 1830 Babbage akaweka mpango wa kuunda machine ambayo ingetumia panchi kadi kuchakata hesabu za sayansi ya namba.

Machine hii ingeweza kutunza namba katika vizio maalum vya kumbukumbu, na kungekua na aina flani ya uongozi mwandamano. Hii inamaanisha kwamba utendaji kazi mmoja ungefanyika kabla ya mwingine kwa namna ambayo mtambo ungerudisha majibu pasipo kushindwa. Mtambo huu ukaja kujulikana kama Analytical Engine, ambayo ni uwakilishi wa kweli wa vifaa vya Tarakilishi za sasa.

Charles Babbage aliunda mtambo wa kwanza ujulikanao kwa jina la Difference Engine mwaka 1833. aliendelea na ubunifu wake hadi mwaka 1837 ndipo akaiunda Analytical Engine.

Analytical Engine ilikua ni Tarakilishi ya Madhumuni-ya-Ujumla yenye kuweza kufuata utaratibu wa mfuatano wa mambo ya kutekeleza, iliyotumia panchi kadi na injini ya mvuke kwa ajili ya nguvu ya uendeshaji.

Ada Lovelace (Augusta Ada Byron) mtoto wa mwinyi Byron wa London Uingereza, anaaminika kama mwasisi wa uandishi wa programu za Tarakilishi na anachukuliwa kama mtu mwenye kipaji halisi cha hesabu.

Ada Lovelace alianza kufanya kazi na Charles Babbage kama msaidizi wakati Babbage akiunda Analytical Engine. Katika kipindi chake cha kazi na Babbage, Ada Lovelace akawa mbunifu wa kwanza wa seti za maelekezo ya kihesabu ambayo lazima yafuatwe katika mpango imara (hasa na Tarakilishi) ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo flani la hesabu.

Zaidi, katika kufanya kazi na Babbage, kulipelekea Ada Locelace kubashiri Tarakilishi za baadae ambazo sio tu zingefanya hesabu za namba, bali pia kuzifanyia kazi alama, ziwe za hesabu au la.

Mtambo ambao ulitumia sehemu kubwa ya muundo wa Difference Engine uliundwa mwaka 1843 na Per George Scheutz akiwa na mtoto wake wa kiume aitwae Edward. Mtambo huu uliuzwa kwa serikali za Uingereza na Marekani, ulitumika mahsusi kuzalisha chati za logi.

Mwaka 1909, muhasibu kutoka Dublin Ireland, Percy Ludgate, peke yake aliunda Tarakilishi ya umakanika yenye kuweza kutumia programu.

Mwishoni mwa miaka ya 1880, muamerika Herman Hollerith akabuni kifaa cha kutunzia data ambacho baadae kinaweza kusomwa na mtambo. Baada ya majaribio ya awali na mikanda ya karatasi kutofanikiwa, akaamua kutumia panchi Kadi.

Kuzitengeneza Panchi Kadi Herman Hollerith akabuni Mtambo wa Kuorodhesha (Tabulator) na mtambo uitwao Key Punch.

Tarakilishi analojia zilizoendelea[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya vita kuu ya pili ya Dunia Tarakilishi analojia za umakanika na umeme zilionekana kuwa ni kazi iliyo katika “hali ya ustadi”.

Tarakilishi analojia ziliweza kutumika katika tatuzi za matatizo magumu kwa kutumia Tabia mishabaha. Hii ni faida mojawapo dhidi ya Tarakilishi dijitali ambazo haziwezi.

Tarakilishi analojia za umakanika zilitumia hesabu za hali nyingine za asili, kama vile uhamisho wa nishati, momenta, na kadhalika kutengeneza idadi za kifanani (data).

Kwa mfano Tarakilishi iliyotumia maji kama idadi ya kifanani (data), ilikuwa ni Water Integrator iliyoundwa mwaka 1928.

Kwa kutumia mkondo na kizio cha nguvu ya umeme, Tarakilishi analojia za umeme ziliumba Hali za Asili kua kama idadi ya kifanani. Kwa mfano Mallock Machine ilioundwa mwaka 1941.

Tarakilishi Planimeter ilitumia umbali kama idadi ya kifanani.

Tofauti na Tarakilishi dijitali za kisasa, Tarakilishi analojia hazikuweza kubadilika kiurahisi kupokea mazingira mapya. Zilihitaji kufungwa upya waya kwa kutumia mikono ili kuzibadilisha kutoka kufanyia kazi tatizo moja kwenda lingine.

Mkokotoo wa dijitali ya ki-elektroniki wa mwanzoni[hariri | hariri chanzo]

Enzi ya ukokotozi wa kisasa ilianza kabla, na wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia.

Kwanza kabisa vifaa vya elektromakanika, kama vile rilei, vilitumika.

Mwezi wa kumi na moja mwaka 1937 George Stibitz alivumbua kikokotoo kilichotumia rilei kilichoitwa Model K. Hiki ndicho kikokotoo cha kwanza kufanya kazi kwa mfumo wa namba jozi. K inasimama kama Meza ya Jikoni ambapo ndipo alipokiungia kikokotoo hiki.

Hata hivyo, vifaa vya sakiti za elektroniki vikatumika mbadala ya vile vilivyolingana navyo vya elektromakanika, hivyo hesabu za dijitali zikachukua nafasi ya hesabu za analojia.

Mwaka 1936, jalada la Alan Turing lilithibisha kwa kiasi kikubwa kuwa kishawishi katika swala zima la ukokotozi na sayansi ya Tarakilishi.

Turing alitoa maana ya Tarakilishi ya kazi zote ambayo ingetekeleza maelekezo ya programu iliyotunzwa kwenye mkanda. Muundo huu ukaja kuitwa Mashine ya Turing.

Mashine ya Turing ilikuwa na hifadhi ndogo sana.

Tarakilishi za kisasa zinaitwa kama Turing kamilifu, ambapo ni kama kusema uwezo wake wa kutekeleza seti za maelekezo ya kihesabu upo sawa kabisa na Mashine ya kazi zote ya Turing.

Palikuwa na mikondo mitatu iliyoenda sambamba ya uundaji wa Tarakilishi enzi za kipindi cha vita kuu ya pili ya Dunia.

Ya kwanza ilikua kazi ya Wajerumani, Konrad Zuse, kifupi Z1 mwaka 1938.

Pili ilikua uundaji wa usiri wa Tarakilishi iitwayo Colossus, nchini Uingereza mwaka 1943.

Mkondo wa tatu ulikua ni uundaji wa Tarakilishi ziitwazo ENIAC na EDVAC. Tarakilishi hizi ziliundwa na Eckert pamoja na Mauchly. Tarakilishi hizi zilitangazwa kwa mapana.

Teknolojia hii ilipelekea [kupitia Turing na wengine] kuundwa kwa Tarakilishi elektroniki ya kwanza ya kibiashara nchini Marekani.

Tarakilishi ya kwanza Duniani kutunza programu ilikua inaitwa Manchester, jina la utani Mtoto. Iliundwa na Frederic C. Williams, Tom Kilburn na Geoff Tootill, katika Chuo Kikuu cha Manchester kiitwacho Victoria, na kuanza kutumia programu yake ya kwanza tarehe 21, mwezi wa sita mwaka 1948.

Leibniz alielezea mfumo wa namba jozi (kiambato kikuu cha Tarakilishi zote za kisasa), hata hivyo hadi miaka ya 1940, miundo mingi iliyofuatia (Ikiwamo mitambo alioiunda Charles Babbage miaka ya 1822, pia hata ENIAC ya mwaka 1945), ilitumia msingi wa mfumo wa namba desimali.

Pete kihesabio cha ENIAC kiliigiza utendaji kazi wa tairi ya tarakimu ya mtambo makanika wa kujumlishia.

Tarakilishi ya elektroniki (Dijitali)[hariri | hariri chanzo]

Tunaingiza Habari (Pembejeo), Tarakilishi inachakata kwa njia ya elektroniki kulingana na maelekezo yapatikanayo katika programu inayotumika kwa muda huo, na kutoa matokeo (Zao).

Tarakilishi za elektroniki zina uwezo wa kufanya kiwango kikubwa cha hesabu na mikokotoo kwa muda mchache.

Kwa kweli tunatumia Tarakilishi kuchakata Picha, Sauti, Maandishi, na vitu vingine ambavyo havipo katika jinsi ya namba. Lakini vyote hivi vinategemea msingi wa hesabu za namba. Michoro, Sauti, na kadhalika ni namba ambazo zimetafsiriwa ndani ya mtambo.

Katika Tarakilishi za dijitali namba hizi ni Moja (1) na Sifuri (0), zinazowakilisha hali kuu mbili za umeme, aidha umeme umewaka (1) au umeme umezima (0). Huu ndio mfumo wa namba jozi utumikao na vifaa vya dijitali.

Kwa maneno mengine kila Picha, kila Mlio, na kila andishi linakua na kanuni jozi husika. Uunganishaji usio na mwisho wa hizi Moja (1) na Sifuri (0) ndio unatengeneza maelekezo yanayopatikana kwenye programu.

Vizazi vya Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Kwa ujumla Tarakilishi zinaweza kuwekwa katika makundi manne ya hatua za kimaendeleo.

Kila kundi liliishia kwa kipindi cha muda flani, na kila kundi lilitupa Tarakilishi ambayo aidha ni mpya na iliyoboreshwa, au maboresho flani kwa Tarakilishi iliopo.

Kizazi cha Kwanza cha Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Kundi hili lilianza miaka ya 1940 hadi miaka ya 1950. Tarakilishi ya elektroniki ya kwanza ilikua inatumia Taa Ombwe katika muundo wake. Kutokana na Taa Ombwe Tarakilishi hizi zikawa zinatoa joto jingi.

Tarakilishi za kipindi hiki zilikua kubwa sana na changamani. Pia zilitumia kiasi kikubwa sana cha umeme.

Tarakilishi hizi zilifanya kazi pole pole sana na ziliweza kufanya kazi moja tu kwa muda. Hazikua zikitumia Mfumo tendaji. Gharama za awali na endeshaji zilikua ni kubwa.

ENIAC ilikuwa ni kifaa cha kwanza cha elektroniki ambacho ni Turing-kamilifu, ambayo ilifanya kokotozi za mwendo wa mitupo ya makombora angani kwa jeshi la Marekani

Tarakilishi ya kwanza ya elektroniki ya Madhumuni-ya-Ujumla iliitwa ENIAC (Electronic Numerical Integrator And Computer).

ENIAC ilikuwa na ukubwa wa mita za mraba 167, uzito wa tani 27, na ilitumia umeme wa kilowati 150. Ilikuwa na maelfu ya Taa Ombwe, dayodi fuwele, rilei, kikinzanishi, na kapasita katika muundo wake.

Tarakilishi ya kwanza ya elektroniki isiyo ya Madhumuni-ya-Ujumla iliitwa ABC (Attanasof-Berry Computer).

Tarakilishi nyingine za enzi hii zifananazo na hizi ni pamoja na Z3 za Ujerumani, Tarakilishi ziitwazo Colossus ambazo zilikua kumi, LEO, Harvard Mark1, na UNIVAC zote za Uingereza.

Upunguzaji ukubwa wa umbo[hariri | hariri chanzo]

Tofauti na ENIAC iliyotumia mtindo wa mchakato sambamba, EDVAC (Electronic Discrete Variable Automatic Computer) ambayo ni mrithi wa ENIAC, ilitumia Bongo kuu kimoja. Muundo huu ulikua rahisi na ulitumika kufanikisha wimbi la upunguzaji ukubwa wa umbo.


Kizazi cha Pili cha Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Kundi hili ni la zile Tarakilishi zilizotumika miaka ya 1955 hadi 1960.

Kuanzia miaka ya 1955 na kuendelea, transista zilichukua nafasi ya Taa Ombwe katika muundo mzima wa Tarakilishi, hivyo Tarakilishi zikapungua ukubwa wa umbo, gharama za awali na endeshaji zikapungua ukilinganisha na kundi la kwanza.

Tarakilishi zikatumia umeme mdogo zaidi hivyo na joto likapungua pia.

Kasi ya utendaji kazi ikaongezeka zaidi ukilinganisha na Tarakilishi za Kizazi cha kwanza.

Diski za kutunzia data ziliweza kuhifadhi makumi ya mamilioni ya herufi na tarakimu.

Tarakilishi ya kwanza iliyotumia transista iliundwa katika Chuo Kikuu cha Manchester mwaka 1953.

Tarakilishi iliyopata umaarufu sana ambayo ilitumia transista katika muundo wake iliitwa IBM 1401.

Mwaka 1956, kampuni ya IBM (International Business Machine) iliunda diski ngumu ya kwanza iitwayo IBM 350 RAMAC.

Kizazi cha Tatu cha Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya 1960 na kuendelea ilishuhudia uvumbuzi wa Sakiti changamano (IC) ambapo Jack St. Clair Kilby na Robert Noyce, kwa kutumia udongo wa silikoni (ambao ni Nusu-kipitishi cha umeme) waliwezesha vifaa vya elektroniki kama vile transista, dayodi, na kadhalika kufungamanishwa kwa idadi kubwa katika kisilikoni kimoja.

Sakiti changamano (IC) ikachukua nafasi ya transista katika muundo wa Tarakilishi, hivyo Tarakilishi zikazidi kupungua ukubwa wa umbo ukilinganisha na za kizazi kilichopita.

Kasi ya utendaji kazi ikazidi kuongezeka zaidi.

Tarakilishi zikatumia umeme mchache zaidi hivyo joto likapungua pia.

Sakiti changamano (IC) ni ndogo kwa umbo na zinatengenezeka kwa ufanisi zaidi. Kwa sababu hii Mikroprosesa ikavumbuliwa.

Utambulisho wa Sakiti Changamano kwenye Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Kitendo cha Tarakilishi kutumia Sakiti changamano (IC) kilikua cha taratibu, hivyo Tarakilishi za Kizazi cha Pili ziliendelea kutumika.

Kwanza zikaja Tarakilishi Dogo (mini computer) ambazo bado zilitegemea matumizi ya transista.

Kisha zikaja Tarakilishi Dogo chotara (hybrid mini computer) ambazo zilitumia transista na Sakiti changamano (IC) kwa pamoja. Mfano wa Tarakilishi hizi ni kutoka kampuni ya IBM, System/360.

IBM System/360 zilikua ni ndogo zaidi kiumbo na bei rahisi ukilinganisha na Tarakilishi za kundi la Kwanza na la Pili. Ambazo ziliitwa Kiunzikuu (Mainframe).

Kizazi cha Nne cha Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Hili ni kundi la Tarakilishi zilizotumika kuanzia miaka ya 1971 mpaka sasa.

Tarakilishi hizi zinatumia Mikroprosesa badala ya Sakiti changamano (IC) hivyo zimepungua zaidi ukubwa wa umbo.

Mikroprosesa ni mfungamanisho wa maelfu ya Sakiti changamano (IC) zilizotambulishwa kipindi cha Kizazi cha Tatu, katika kisilikoni kimoja.

Ujio wa Mikroprosesa ukazaa mabadiliko ya Mikrokompyuta, ambazo zikaja kujulikana kama Tarakilishi Binafsi.

Kizazi cha Kwanza cha Tarakilishi Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Tarakilishi hizi ni zile zilizokua zikitumika katikati ya miaka ya 1971 na 1976.

Mwanzoni Mikrokompyuta zilikua ni mkusanyiko wa ajabu, mara nyingi zilikuja katika mtindo wa vifaa. Kimsingi nyingi zilikua ni maboksi yenye taa na swichi nyingi.

Zilitumika kipekee na wahandisi na wapendeleaji walioelewa mfumo jozi.

Kizazi cha Pili cha Tarakilishi Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Hizi ni Tarakilishi zilizotumika kuanzia mwaka 1977 mpaka sasa.

Mikrokompyuta zakawa rahisi kuzitumia na kufanya idadi kubwa ya hadhira iweze kuzipata.

Kwa kufanana, zinakuja zikiwa na Kibao mbonyezo, Kipanya, na skrini. Au pia unaweza kuzifunga kwenye televisheni.

Tarakilishi hizi zinakimu uwakilishaji muono wa maandishi na namba kwenye skrini.

Kifupisho[hariri | hariri chanzo]

Katika historia ya vifaa kokotozi,

Kizazi cha Tano cha Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Huu ni mradi ulioanzishwa mwaka 1982 na Wizara ya Viwanda na Biashara za Kimataifa ya Japani kutengeneza Tarakilishi ambayo iwe na uwezo kama wa Tarakilishikuu (Super Computer), na kutoa jukwaa kwa maendeleo ya baadaye ya Akili bandia. Ndipo mradi huu ukaitwa Mradi wa Mifumo ya Tarakilishi za Kizazi cha Tano.

Mradi huu ulilenga kuitengeneza Tarakilishi hiyo kwa kipindi cha miaka 10, ambapo baada ya hapo mradi ungefikirika kumalizika na uwekezaji ungeanzishwa katika mradi mpya wa “Kizazi cha Sita”.

Upo mgawanyiko wa maoni kuhusu matokeo yake; aidha mradi haukuwa na mafanikio au jambo hili lilikuwa mbele ya wakati wake.

Pale ambapo vizazi vya Tarakilishi vilivyopita vilizingatia kuongeza idadi ya elementi zenye mantiki kwenye Bongo kuu moja, Kizazi cha tano katika kipindi chake kiliaminika badala yake kugeukia uongezaji wa idadi ya Bongo kuu kwenye Tarakilishi moja ili kuongeza utendaji.

Kuzaliwa kwa Tarakilishi[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya miaka ya 1920, Tarakilishi walikuwa ni Makarani binadamu.ambao walifanya mikokotoo. Kawaida walikua chini ya uongozi wa Mwanafizikia.

Maelfu wengi wa Tarakirishi waliajiriwa maeneo ya biashara, serikalini, na idara za tafiti.

Wengi wa Tarakilishi walikua ni wanawake, na walitambulika wana digrii ya Kalkulasi. Baadhi walifanya hesabu za kifalaki kwa ajili ya kalenda.

Baada ya miaka ya 1920, msemo Mtambo kokotoaji ukamaanisha mtambo wowote ambao unafanya kazi ya Tarakilishi binadamu, hususani zile ambazo zinafuatana na taratibu za utendaji za tasnifu ya Church-Turing.

Tasnifu ya Church-Turing[hariri | hariri chanzo]

Tasnifu inaeleza kwamba, mbinu ya hisabati inaleta matokeo pale ikiweza kuwekwa kama orodha ya maelekezo yanayoweza kufuatwa na Karani binadamu kwa penseli na karatasi, kwa muda wote unaohitajika, na pasipo ubunifu au utambuzi.

Mitambo ambayo ilikokotoa kwa kutumia thamani endelevu ilitambulika kama aina ya analojia.

Mitambo hii ya analojia ilitumia vyombo vya mitambo ambavyo viliwakilisha idadi za namba endelevu, kama vile pembe ya mzunguko wa mpini au utofauti kwenye nguvu ya umeme.

Vifaa vya mitambo ya dijitali, kwa kupingana na analojia, viliweza kuonyesha hali ya uthamani wa namba na kutunza kila tarakimu binafsi.

Vifaa vya mitambo ya dijitali vilitumia difference engines au rilei kabla ya uvumbuzi wa vifaa vya hifadhi ya ndani.

Msemo Mtambo kokotoaji taratibu ukaanza kupotea mwishoni mwa miaka ya 1940, na kubaki Tarakilishi pale ambapo mwanzo wa kishindo wa Mitambo dijitali ya elektroniki ulipozoeleka.

Tarakilishi hizi ziliweza kufanya ukokotoaji ambao awali ulifanywa na karani binadamu.

Kwa sababu thamani zinazotunzwa na mitambo ya dijitali hazikuwekewa mipaka na tabia asili kama vifaa vya analojia, Tarakilishi mantiki, kwa msingi wa vifaa vya dijitali, iliweza kufanya chochote ambacho kiliweza kuelezewa kama “makanika halisi.”

Mtambo wa nadharia wa Turing, uliobuniwa na Alan, ni kifaa cha kubuni kilichoongelewa kinadharia ili kusoma tabia za vifaa kama hivyo.

Maana ya kompyuta[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kupokea na kukusanya taarifa (Data), kufanyia kazi na kutoa matokea ya kazi hiyo na namna ilivyoendeshwa, pamoja na kutoa matokeo ya kitu kilichofanyika, yaani kinachoonekana (Information)kwa haraka.

Tofauti ya data na habari (information)[hariri | hariri chanzo]

Data[hariri | hariri chanzo]

Ni ibara ya taarifa au maelezo, na inaweza kuonekana katika sura ya maandishi, michoro, picha, namba, alama, nembo, sauti au lugha ya maandishi, au sauti pamoja na picha.

Habari (Information)[hariri | hariri chanzo]

Ni kazi inayotokana na taarifa au maelezo (Data) baada ya kwisha kupangiliwa na kufanyiwa kazi kisha kutoa matokeo kamili ya kazi hiyo, pamoja na kuleta kitu chenye kufahamika na chenye faida.

Sifa za kompyuta[hariri | hariri chanzo]

Wepesi[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta inafanya kazi kwa wepesi wa hali ya juu kiasi kwamba unaweza kutafuta kitu kwa muda wa sekunde chache tu, kitu ambacho kama utakitafuta kupitia chombo chengine unaweza kuchukuwa wakati mrefu mpaka kukipata na pengine usikipate, kwa mfano unaweza kufanya hesabu ngumu kwa muda mchache kuliko kutumia akili yako. Pia unaweza kutafuta somo lolote kupitia internet kwa kutumia muda mfupi kulipata somo hilo kuliko ungetumia marejeo ya vitabu vya kuchapishwa.

Ubora[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta inafanya kazi kwa ubora zaidi bila kuonyesha udhaifu na makosa ya aina yoyote, na kama itabainika ya kwamba kuna makosa yametendeka kwenye kazi yako kompyuta kabla ya kuendelea kufanya kazi inakuonyesha kwamba upo katika makosa na kukutaka mara moja kurekebisha makosa hayo kwa kukuletea tangazo lenye sehemu kadhaa za kuchagua, ima kuendelea na kazi yako kama ilivyo au kufanya marekebisho ya kazi yako, kwa mfano unapotafuta kitu kutoka kwenye kompyuta, kompyuta kabla ya kutekeleza amri hiyo inakuletea tangazo na kukuuliza ya kwamba ni kweli una uhakika wa kutaka kufuta kitu hicho au umefanya hivyo bila kukusudia?

Pia kompyuta imekuandalia kila kitu unachotaka kukifanya ndani yake kutegemea na malengo yako mwenyewe.

Pia kompyuta inazingatiwa ni mwalimu au muelekezaji (Instructor), kwani inakuelekeza jinsi gani unaweza kufanya kazi yako kwa ukamilifu.pia ndani ya kompyuta kuna kitu kinachoitwa kisaidizi (help)mbacho kinatumika kwa ajili ya kufanya utafiti wa kitu fulani ili kufahamu matumizi na njia zake.

Uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu[hariri | hariri chanzo]

Miongoni mwa mambo muhimu ndani ya kompyuta ni kupatikana sehemu kubwa ya kuhifadhia vitu kwa amani na bila kupotea vitu hivyo.

Aina za matumizi ya kompyuta[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya kompyuta yanatofautiana kutokana na malengo na makusudio ya mtumiaji mwenyewe, na matumizi ya kompyuta yamegawanyika katika sehemu kuu mbili.

Matumizi ya jumla[hariri | hariri chanzo]

Kuna kompyuta zilizoandaliwa kwa ajili ya matumizi yote ambayo mtumiaji anaweza kutumia kutegemea na malengo yake binafsi, kwa mfano mhasibu anaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kufanyia kazi zake za uhasibu (hesabu). pia mwanasayansi, fundi, mwalimu na mwanafunzi, wote hao wanaweza kutumia kompyuta kwa malengo yao tofauti.

Matumizi maalumu[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta hizi zimeandaliwa kwa ajili ya malengo maalumu tu, kama zile kompyuta zilizoandaliwa kwa ajili ya kuchorea moyo na kupigia picha za X-ray, ambazo ni vigumu kwa mtu mwengine kuzitumia kwa ajili ya kufanyia kazi zake binafsi ambazo zina tofautiana na hizo za hospitalini.

Aina za kompyuta[hariri | hariri chanzo]

Tarakilishi na sehemu zake.

Kuna aina kuu tatu za kompyuta, nazo ni kama ifuatavyo:-

Kompyuta Dijitali[hariri | hariri chanzo]

Ni kompyuta zinazotumika kwa ajili ya kufanyia hesabu pamoja na kazi za kutumia akili.

Kompyuta Analogu[hariri | hariri chanzo]

Ni kompyuta zinazotumika kwa ajili ya kupokea taarifa (Data) kama zile za kusomea hali ya hewa, kupimia mishipa ya damu na kupimia kiwango cha chumvi kwenye maji.

Kompyuta Mahuluti (Hybrid Computers)[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta hizi zinafanana na zile zilizotangulia kutajwa hapo mwanzo, nazo zinatumika kwa ajili ya kutafutia taarifa (Data) kutoka kwa binadamu moja kwa moja na kupitia mandishi na vipimo.

Aina za Tarakilishi dijitali[hariri | hariri chanzo]

Tarakilishi inaweza kuainishwa kulingana na madaraja yafuatayo:

 • Ukubwa wa umbo
 • Dhumuni, na
 • Utendaji kazi

Kwa kutumia msingi wa ukubwa wa umbo, tarakilishi zinaweza kuwekwa katika makundi yafuatayo:

Tarakilishikuu (Super Computer):[hariri | hariri chanzo]

Tarakilishi hii inashughulikia kiwango kikubwa kabisa cha hesabu za sayansi.

Inahifadhiwa katika chumba chenye mfumo poza maalum ambao unaunganisha uyoyozwaji hewa na kimiminiko poza.

Tarakilishikuu za miaka ya 1970 zilitumia prosesa chache. Katika miaka ya 1990, zikatokea mashine zitumiazo maelfu ya prosesa. Hadi mwishoni mwa karne ya 20 Tarakilishikuu zitumiazo makumi elfu ya prosesa zikawa ni kawaida. Tarakilishi za karne ya 21 zinaweza kutumia prosesa zaidi ya 100,000 (baadhi zikitumia vizio vyenye kuonesha kwa picha) zikiunganishwa na miungo kasi.

Hadi mwezi Juni wa mwaka 2013, Tarakilishikuu iitwayo Tianhe-2 ya Uchina, ndiyo yenye kasi kubwa zaidi duniani kwa 33.86 petaFLOPS (FLoating Point Operations Per Second).

Tarakilishikuu Blue Gene/P iliyopo Maabara ya Kitaifa ya Argonne

Tarakilishikuu iitwayo Blue Gene/P iliyopo Maabara ya Kitaifa ya Argone inaendesha zaidi ya prosesa 250,000, ikitumia uyoyozwaji hewa wa kawaida wa kituo cha data, ina makundi 72 ya makabati yanayounganishwa na mtandao nuru wa kasi kubwa.

Mifumo ya Tarakilishi zitumiazo jumla kubwa ya prosesa kwa kawaida zinatumia moja ya njia mbili: Njia mojawapo (kwa mfano, kwenye ukokotozi msambao) idadi kubwa ya Tarakilishi peke (kwa mfano, Tarakilishi mpakato [laptop]) zinasambazwa kwenye mtandao (kwa mfano, intaneti) na kutenga kiasi au muda wote kutatua tatizo fulani kwa pamoja; kila Tarakilishi inapokea na kukamilisha kazi nyingi ndogo ndogo, na kutoa ripoti ya matokeo kwa Tarakilishikuu ambayo inaunganisha matokeo ya kazi kutoka Tarakilishi zote kuwa utatuzi wa jumla.

Katika njia nyingine, idadi kubwa ya prosesa zilizoteuliwa zinawekwa kwa ujirani mkubwa kabisa (kwa mfano, kwenye Konga tarakilishi); hii inaokoa muda mwingi kuhamisha data kuzunguka pande zote na inafanya urahisi kwa prosesa kufanya kazi pamoja (kuliko katika kazi zilizotenganishwa), kwa mfano katika usanifumuundo Wavu na Hayipakyubu.

Matumizi ya prosesa zenye-kokwa-nyingi ikiunganishwa na uwekaji-chini-ya-makao-makuu ni mwelekeo unaoibuka; mtu anaweza kufikiria hiki kitu kama konga dogo (prosesa zenye-kokwa-nyingi katika smatifoni, tableti, tarakilishi mpakato na kadhalika) ambalo kwa pamoja linategemea na kuchangia kwenye kundi.

Tarakilishikuu inachukua nafasi muhimu katika sayansi ya mkokotoo, na zinatumika kwa mapana kwenye kazi makini za mkokotoo katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na makanika ya kwanta, utabiri wa hali ya hewa, tafiti za tabia nchi, chunguzi za mafuta na gesi, fanyizo za molekuli (ukokotozi wa maumbile na tabia za michanganyiko ya kemikali, makromolekuli za biolojia, polima, na fuwele), na uigaji wa Asili (kama vile uigaji wa nyakati za mwanzo za ulimwengu, erodainamiki za ndege na vyombo vya anga, ulipuaji wa silaha za nyuklia, na mchanganyiko wa nyuklia).

Pote pote katika historia ya Tarakilishikuu, zimekuwa muhimu katika nyanja ya kukabili Elimu ya mficho.

Kipimo cha utendaji wa Tarakilishikuu[hariri | hariri chanzo]

Kwa ujumla Tarakilishikuu imelenga katika upeo wa ukokotozi uwezo kuliko ukokotozi ujazo.

Ukokotozi uwezo hasa unafikiriwa kwamba ni kutumia uwezo wa mwisho wa ukokotozi kutatua tatizo moja kubwa katika kiwango kifupi cha muda.

Mara nyingi mfumo uwezo unaweza kutatua tatizo lenye ukubwa au ugumu ambao hakuna Tarakilishi nyingine inayoweza. Kwa mfano, matumizi magumu sana ya uigaji hali ya hewa.

Kwa kupingana na hili, ukokotozi ujazo moja kwa moja unafikirika kutumia nguvu ya Tarakilishi yenye athari madhubuti za gharama kwa ajili ya kutatua kiwango kidogo cha matatizo makubwa au kiwango kikubwa cha matatizo madogomadogo. Kwa mfano, maombi ya watumiaji wengi kwenye databezi au nywila. Miundo ya mashine zitumikazo kusaidia watumiaji wengi kama utaratibu wa kazi za kila siku zinaweza kuwa na ukubwa mwingi lakini hazifikiriwi moja kwa moja kama Tarakilishikuu, ikichukuliwa kwamba hazitatui tatizo moja kubwa na gumu sana.

Kasi za juu za Tarakilishikuu. Kasi kwenye alamakipimamwendo zaidi ya miaka 60.

Kwa ujumla, kasi za Tarakilishikuu zinapimwa na kuwekwa alama teule kwa FLOPS (Floating Point Operations Per Second), na si kwa mbadala wa MIPS; ni kwamba, hii ni “Instructions per second” kama inavyohusika na Tarakilishi za madhumuni-ya-jumla. Vipimo hivi kwa kawaida vinatumika kwa pamoja na viambishi awali vya SI kama vile Tera-, ikiunganishwa katika kifupisho “TFLOPS” (1012 FLOPS, inatamkwa teraflops), au peta-, ikiunganishwa kwenye kifupisho “PFLOPS” (1015 FLOPS, inatamkwa petaflops). Kwa “Kipimopeta” Tarakilishikuu zinaweza kuchakata kwadrilioni moja (milioni kwa kipawa cha nne (Uingereza) au milioni kwa kipawa cha tano (Marekani)) (1015) (1000 trilioni) FLOPS. “Kipimoexa” ni kuwa ukokotozi tendaji upo kwenye nafasi ya exaflops. Exaflop ni kwintilioni moja (1018) FLOPS (teraflops milioni moja).

Si namba moja inayoweza kutoa picha ya utendaji mzima wa mifumo ya Tarakilishi, hata hivyo lengo la alama teule ya Linpark ni kukadiria ni kwa kasi ipi Tarakilishi inaweza kutatua matatizo ya namba na hii inatumika kwa mapana zaidi katika tasinia. Vipimo vya FLOPS ni eidha vimedondolewa kulingana na nadharia ya utendaji wa kiwango mbadiliko cha prosesa (kizalishwacho kutoka ainisho la mtengenezaji wa prosesa na kuonyeshwa kama “Rpeak” katika orodha ya TOP500) ambacho kiujumla hakipatikani wakati wa kufanya kazi halisi, au uelewa patikanifu, uzalishwao kutokana na alama teule za LINPARK na kuonyeshwa kama “Rmax” katika orodha ya TOP500. Alama teule za LINPARK hasa hasa zinatekeleza changanuzi za LU ya solo kubwa. Utendaji wa LINPARK unatoa ishara kiasi ya utendaji kwa baadhi ya matatizo ya dunia halisi, lakini si lazima ifananie na masharti ya utendaji kazi ya Tarakilishikuu nyingi nyinginezo, ambapo kwa mfano zinaweza kuhitaji zaidi kiwango kikubwa cha uwezo wa vizio vya kutunzia kumbukumbu, au zinaweza kuhitaji utendaji bora wa ukokotozi wa namba kamili, au zinaweza kutaka utendaji wa juu wa mifumo ya I/O ili kupata viwango vya juu vya utendaji.

Orodha ya TOP500[hariri | hariri chanzo]

Chati ya pai inayoonyesha ushiriki wa nchi kutumia Tarakilishikuu mpaka Novemba 2015

Tangu mwaka 1993, Tarakilishikuu zenye kasi kubwa zimekuwa zikiwekewa safu katika orodha iitwayo TOP500.

Orodha hii inaonyesha Tarakilishikuu yenye kasi iliyopo katika muda wowote unaotakiwa.

Orodha ya TOP500 inaonyesha Tarakilishikuu yenye kasi iliyopo ni ile ambayo nchi nyingi duniani kote zinashiriki kuitumia.

Mradi wa TOP500 unaweka safu na maelezo ya mifumo ya Tarakilishi 500 zenye nguvu zaidi duniani.

Mradi ulianzishwa mwaka 1993 na unachapisha orodha iliyokuwa ya kisasa ya Tarakilishikuu mara mbili kwa mwaka.

Orodha ya kwanza ya kisasa mara zote inatukia na Mkutano wa Kimataifa wa Ukokotozimkuu mwezi Juni. Na ya pili huwakilishwa mwezi Novemba katika Mkutano wa Ukokotozimkuu wa ACM/IEEE. Mradi huu umelenga kutoa msingi wa kutumainiwa wa ufuatiliaji na ugunduaji mielekeo ya ukokotozi wa kasi ya juu na kuweka safu katika misingi ya HPL. Ni utekelezaji unaowezekanika wa utendaji wa hali ya juu wa alama teule ya LINPARK ulioandikwa kwenye fortran ya Tarakilishi za distributed-memory.

Orodha ya TOP500 inakusanywa na Jack Dongara wa Chuo kikuu cha Tennessee, knoxville, Erich Strohmaier na Horst Simon wa Maabara ya Kitaifa ya NERSC/Lawrence Berkeley (na, kutoka 1993 mpaka kifo chake mwaka 2014, Hans Meuer wa Chuo kikuu cha Mannheim, Ujerumani.)

Ifuatayo ni orodha ya hivi karibuni ya Tarakilishi ambayo inapatikana juu kabisa ya orodha ya TOP500, na “kasi ya juu” inapatikana kama makadirio ya “Rmax

Tarakilishi 20 za juu duniani hadi Juni 2013
Mwaka Tarakilishikuu Kasi ya juu
(Rmax)
Mahali
2013 NUDT Tianhe-2 33.86 PFLOPS Guangzhou, Uchina
2012 Cray Titan 17.59 PFLOPS Oak Ridge, U.S.
2012 IBM Sequoia 17.17 PFLOPS Livermore, U.S.
2011 Fujitsu Tarakilishi K 10.51 PFLOPS Kobe, Japani
2010 Tianhe-IA 2.566 PFLOPS Tianjin, Uchina
2009 Cray Jaguar 1.759 PFLOPS Oak Ridge, U.S.
2008 IBM Roadrunner 1.026 PFLOPS Los Alamos, U.S.
1.105 PFLOPS

Historia ya Tarakilishikuu[hariri | hariri chanzo]

Historia ya ukokotozi mkubwa sana inarudi nyuma hadi miaka ya 1960 wakati mfululizo wa tarakilishi katika Control Data Corporation (CDC) ulibuniwa na Seymour Cray kutumia ubunifu vumbuzi na usambamba ili kufanikisha kufikia kilele cha ukokotoaji bora.

Tarakilishi CDC6600 iliyoachiwa mwaka 1964 inafikirika kuwa ndiyo Tarakilishikuu ya kwanza.

Cray alihama CDC mwaka 1972 na kwenda kuunda kampuni yake. Miaka minne baadaye, aliwasilisha Tarakilishi iitwayo Cray-1 iliyokua na kasi ya 80MHz mwaka 1976, na ikawa moja ya Tarakilishikuu yenye mafanikio sana katika historia ya Tarakilishi.

Tarakilishi Cray-2 iliachiwa mwaka 1985 ambayo ilikua ni tarakilishi ya prosesa 8 yenye kutumia kimiminiko poza na mfumo poza wa maji yanayosukumwa kwa nguvu ya shinikizo kupoza vihunzi huru vyake wakati ikitumika.

Cray-2 ilifanya kazi kwa kasi ya 1.9gigaflops ikawa Tarakilishi yenye kasi kubwa duniani hadi mwaka 1990.

Cray-1 imetunzwa katika jumba la makumbusho la Deutsches-

Wakati tarakilishikuu za miaka ya 1980 zikitumia prosesa chache tu, miaka ya 1990, mashine zilizotumia maelfu ya prosesa zikaanza kuonekana kote Marekani na Japani, na kuweka rekodi mpya za utendaji wa mkokotoo.

Tarakilishikuu iitwayo Numerical Wind Tunnel kutoka kampuni ya Fujitsu ilitumia prosesa za Vekta 166 na kujiweka nafasi ya juu mwaka 1994 kwa kasi ya juu ya 1.7gigaflops kwa prosesa.

Intel Paragon inawezekana ilikuwa na prosesa za Intel i860 kuanzia 1000 hadi 4000 katika umbo mbalimbali, na kutambulika kuwa ndiyo na kasi zaidi duniani mwaka 1993. Paragon ilikuwa ni mashine ya MIMD ambayo inaunganisha prosesa kupitia wavu wa vimbe mbili wenye kasi kubwa, ulioruhusu kazi zifanyike katika chomozo tofauti, kwa kuwasiliana kupitia Kipengee cha Upitishaji Jumbe.

SR2201 ilipata utendaji wa juu wa 600 megaflops mwaka 1996 kwa kutumia prosesa 2048 zilizounganishwa kupitia mtandao wa mwamba wa vimbe tatu wenye kasi.

Matumizi ya nishati na mbinu za kudhibiti joto kwa Tarakilishikuu[hariri | hariri chanzo]

Tarakilishikuu hasa inatumia kiwango kikubwa cha nguvu ya umeme, na takribani kiwango chote hiki kinageuzwa kuwa joto, inahitaji upoozaji. Kwa mfano Tianhe-1A inatumia megawati 4.04 za umeme.

Gharama za kuwasha na kupoza mashine zinaweza kuwa kubwa, kwa mfano megawati 4, katika bei ya dola 0.10 kwa kilowati, ni jumla ya dola 400 kwa saa au dola milioni 3.5 kwa mwaka.

Mbinu za udhibiti joto ni suala kubwa kwenye vifaa vya elektroniki vyenye sehemu nyingi, na linaathiri mifumo ya Tarakilishi yenye nguvu sana kwa namna tofautitofauti. Nguvu ya Mpango wa Joto na Mtapanyo wa Nguvu ya CPU vilitoa kwa ukokotozi-mkubwasana kuzipita zile mbinu za kizamani za upoozeshaji Tarakilishi.

Uwekaji wa maelfu ya prosesa pamoja bila kuzuilika unazalisha kiwango kikubwa cha msongamano wa joto ambao unatakiwa ushughulikiwe. Cray-2 ilipoozwa kwa kimiminiko poza na mfumo poza wa maji yanayosukumwa kwa nguvu ya shinikizo kupoza vihunzi huru vyake wakati ikitumika. Hata hivyo njia hii ya upoozeshaji kwa kutumia kimiminiko haikua sahihi kiutendaji kwa mifumo ya kabati-nyingi zitumiazo prosesa zisizo-kwenye-rafu, na katika System X, mfumo maalum wa upoozeshaji unaohusisha uyoyozwaji hewa na kimiminiko poza ulianzishwa kwa mwungano na kampuni ya Liebert.

Katika mfumo wa Blue Gene, IBM kwa makusudi kabisa walitumia prosesa za nguvu ya chini ili kushughulikia msongamano wa joto. Kwa upande mwingine, Power775 kutoka IBM, iliyoachiwa mwaka 2011, ina elementi zilizowekwa karibu sana ambazo zinahitaji upoozeshaji wa kutumia maji. Mfumo wa Aquasar kutoka IBM kwa upande mwingine unatumia upoozeshaji wa kutumia maji moto ili kufanikisha ufanisi wa nishati. Maji yanatumiwa pia kupasha majengo.

Ufanisi wa nishati wa mifumo ya tarakilishi kwa jumla unapimwa kimbadala na “FLOPS kugawanya kwa wati”. Mwaka 2008, Roadrunner kutoka IBM ilifanya kazi kwa 376 MFLOPS/wati. Mwezi Novemba mwaka 2010, Blue Gene/Q ilifikia 1684 MFLOPS/wati. Mwezi Juni wa 2011, sehemu 2 za juu kwenye orodha ya Green500 zilishikwa na mashine za Blue Gene, za New York (kila moja ikifikia 2097 MFLOPS/wati), ambapo konga DEGIMA ya Nagasaki ikichukua nafasi ya tatu ikiwa na 1375 MFLOPS/wati.

Matumizi ya tarakilishikuu[hariri | hariri chanzo]

Hatua za matumizi ya tarakilishikuu zinaweza kuwekwa kwa kifupi katika jedwali lifuatalo:

Muongo Matumizi na Tarakilishi husika
1970s Utabiri wa hali ya hewa, tafita za erodainamiki (Cray-1).[1]
1980s Changanuzi za Probabilistiki,[2] Ufanyizaji kinga za mnururisho[3] (CDC Cyber).
1990s Mabavu ya uvumbuzi wa maneno ya siri (EFF DES cracker).[4]
2000s Uigaji majaribio ya nyuklia wa 3D kama mbadala wa utendaji kisheria wa mkataba wa kuzuia ueneaji wa silaha za nyuklia. (ASCI Q).[5]
2010s Uigaji elimumiendo ya molekuli (Tianhe-1A)[6]

Tarakilishi Blue Gene/P ya IBM imekua ikitumika kuigiza seli neva bandia katika ulinganifu wa makadirio ya asilimia moja ya tabaka la nje ya ubongo wa binadamu.

Utabiri wa hali ya hewa wa kisasa pia unategemea tarakilishikuu. Idara ya Taifa ya Usimamiaji masuala ya Bahari na Hewa inatumia tarakilishikuu kuchakacha mamia ya mamilioni ya chunguzi kusaidia kufanya tabiri za hali ya hewa ziwe sahihi zaidi.

Mwaka 2011, changamoto na magumu katika kusukuma mgubiko wa matumizi ya tarakilishikuu viliwekewa msisitizo na kampuni ya IBM kutelekeza mradi wake wa tarakilishi Blue Waters ya kipimopeta.

Tafiti na mwelekeo wa kimaendeleo[hariri | hariri chanzo]

Mchoro wa vimbe 3 (3D) wa miunganiko ya Torus utumikao na mifumo kama vile Blue Gene, Cray XT3, n.k.

Kulingana na kasi ya sasa ya maendeleo, wataalamu wa tasnia wanakadiria kwamba kufikia mwaka 2018 tarakilishikuu zitafikia exaflops 1 (1021) (FLOPS kwintilioni moja). Wachina wameanza mipango wawe na tarakilishikuu ya exaflop 1 inayofanya kazi kufikia mwaka 2018 kwa kutumia usanifumuundo wa prosesa yenye kokwa nyingi za Intel MIC, ambayo ni itikio la kampuni ya Intel kwa mifumo ya GPU, SGI wamepanga kupata ongezeko la mara 500 katika utendaji kufikia 2018, ili waweze kupata exaflop moja. Sampuli za visilikoni vya MIC vyenye kokwa 32 ambavyo vinaunganisha vizio vya mchakato vekta na CPU ya kawaida zimekuwa zikipatikana. Serikali ya India pia imeanzisha lengo kwa tarakilishikuu kuwa na mfiko wa exaflop, ambalo wanatarajia kulifikia mwaka 2017.

Erik P. Benedictis wa maabara za taifa za Sandia ametoa nadharia kwamba tarakilishi ya zettaflop (1021) (FLOPS sextilioni moja) inahitajika ili kufanikisha ufanyizaji hali ya hewa kamili, ambayo inaweza kujumuisha mzunguko wa muda wa wiki mbili kiusahihi. Mifumo kama hii pengine inaweza kutengenezwa kwenye miaka ya 2030.

Tarakilishi kiunzikuu (Mainframe Computers)[hariri | hariri chanzo]

Tarakilishi kiunzikuu IBM System z9

--Sehemu hii inaweza kuwa na maelezo ya kiufundi zaidi na maneno mengine kukosa tafsiri ya Kiswahili kwa wasomaji wengi kuelewa. Tafadhali saidia kuboresha sehemu hii iweze kueleweka zaidi kwa wasomaji wa kawaida kwa kutoa tafsiri ya maneno yaliyotumika humu, au kutoa maelezo mepesi bila kuondoa maana halisi.-- Tarakilishi kiunzikuu ni tarakilishi ambazo kimsingi zinatumiwa na kampuni na mashirika ya serikali kwa matumizi makinifu, kuchakata data nyingi kama vile sensa, takwimu za viwanda na biashara, upangaji rasilimali za kazi, na uchakatuaji amali.

Mtajo huu kwa asili unanena kuhusu makabati makubwa yanayotunza Bongo kuu na Kizio kikuu cha kumbukumbu kwa tarakilishi za awali.

Baadaye, msemo huu ukatumika kubainisha mitambo yenye nguvu ya kibiashara dhidi ya ile yenye nguvu ndogo. Miundo mikubwa ya nyingi ya Mifumo ya Tarakilishi ilianzishwa miaka ya 1960, lakini ikaendelea kukua.

Tarakilishi kiunzikuu pia inajulikana kama “Chuma Kubwa (Big Iron)” ni ndogo na haina nguvu sana kama Tarakilishikuu katika uwezo wa ukokotoaji. Inahusika na utunzaji wa faili na kumbukumbu kubwa sana.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Miundo ya tarakilishi kiunzikuu ya kisasa kwa jumla inatafsiriwa kwa kasi ya mkokotoo kazi-moja (hasa inatafsiriwa kama kiasi cha MIPS au FLOPS katika suala la hesabu za kiwango mbadiliko), na zaidi kwa

 • Uhandisi wa ndani wa ziada na matokeo makubwa ya ulinzi na kutegemeka.
 • Upatanifu hasahasa ulio nyuma kimaendeleo na programu za zamani.
 • Vima vya matumizi ya juu ya mikokotoo na vifaa vya tarakilishi kuhimili idadi kubwa ya kazi katika muda fulani.

Uthabiti wao na kutegemeka vinawezesha hii mitambo kufanya kazi bila kukatizwa kwa vipindi virefu.

Uboreshaji wa programu kawaida unahitaji utengenezaji wa mfumo endeshi au sehemu zake, na hizi si vivuruga pale tu unapotumia vifaa vya kutengeneza hali ya kweli ambayo si bayana kama vile mfumo endeshi uitwao z/OS na mfumo endeshi uitwayo Parallel Sysplex zote za IBM, au Unisys ya XPCL, ambayo inahimili ushirikishaji wa kazi kubwa hivi kwamba mfumo mmoja unaweza kuchukua kazi za mwingine wakati unapokuwa unajiweka sawa.

Tarakilishi kiunzikuu zinatafsiriwa kwa upatikanaji mkubwa, moja ya sababu kubwa ya maisha marefu, wakati ambapo zenyewe hasa zinatumika katika matumizi ambayo zikiacha kutumika itakuwa gharama na ni janga kubwa. Huu msemo tegemezi, patikanivu, na inayohudumika (reliability, availability and serviceability = RAS) unatafsiri tabia za tarakilishi kiunzikuu.

Mipango na utekelezaji stahiki unahitajika ili kutumia hivi vitu, na kama utekelezaji hautakuwa sawa, unaweza kutumika kuzuia faida zipatikanazo. Kwa nyongeza, tarakilishi kiunzikuu zipo salama zaidi kuliko aina nyingine za tarakilishi: dhaifu za kanzi data za NIST National Institute of Standards and Technology, US-CERT, inawekea kima tarakilishi kiunzikuu za desturi kama vile Zseries za IBM, Unisys Dorado na Unisys Libra kama miongoni mwa zile ambazo zipo salama zaidi zikiwa na madhaifu machache madogomadogo zikilinganishwa na maelfu ya Vyeneo (Windows), Linux na Unix.

Mwishoni mwa miaka ya 1950, tarakilishi kiunzikuu nyingi zilikuwa hazina kipengee ingiliano kamilifu. Zilikubali kundi la panchi kadi, mikanda ya karatasi, au mikanda ya sumaku kuhamisha data na programu. Zilifanya kazi katika mtindo wa bechi kuhimili shughuli za nyuma ya ofisi kama vile tozo za wateja, na vituo ingiliano vinavyohimiliwa takribani maalum kwa matumizi zaidi kuliko uendelezaji wa programu. Vifaa kama Mashine chapa na Teleprinta vilikuwa pia viweko amrisho vya kawaida kwa waendeshaji mifumo mpaka miaka ya 1970, ingawaje kwa kiasi kikubwa vilipandikiziwa vibao mbonyezo na vifaa onyeshi.

Mwanzoni mwa miaka ya 1970, tarakilishi kiunzikuu nyingi zilipata kipengee muingiliano cha watumiaji na kufanya kazi kama tarakilishi inayotoa huduma kwa tarakilishi nyingine ndogo zilizoungwa nayo, zikihimili mamia ya watumiaji wakati huohuo pamoja na mchakatuo wa bechi. Watumiaji walipata fursa ya kuingia kwa kutumia vituo maalumu, au, baadaye, kwa kutumia tarakilishi binafsi zilizozatitiwa na programu igizaji vituo.

Kufikia miaka ya 1980, tarakilishi kiunzikuu nyingi zilihimili vituo vyenye hali ya upicha, na vituo igizaji, lakini si kipengee cha upicha cha watumiaji.

Mpango huu wa ukokotozi wa mtumiaji wa mwisho ulifikia mwelekeo tawala wa hali ya kupitwa na wakati miaka ya 1990 kutokana na ujio wa tarakilishi binafsi zilizokuwa na GUI.

Baada ya mwaka 2000, tarakilishi kiunzikuu nyingi za kisasa kwa kiasi au kabisa polepole zinaondoa ingio maarufu la vituo kwa watumiaji wa mwisho kufadhili kipengee cha watumiaji cha mtindo wa webu.

Kihistoria, tarakilishi kiunzikuu zilipata sehemu ya jina lake sababu ya ukubwa wake wa msingi, na kwa sababu ya mahitaji muhimu ya upashaji joto, upitishaji hewa safi, na uyoyozaji hewa (HVAC), na nguvu ya umeme; kimsingi imejiweka kama “mfumo mkuu” wa muundo msingi uliokusudiwa.

Mahitaji ya sanifu za muundo msingi wa juu kwa haraka sana yalipungua kati kati ya miaka ya 1990, kwa sanifu za tarakilishi kiunzikuu zenye CMOS kuchukua nafasi ya teknolojia ya zamani ya bipolar. IBM ilidai kwamba tarakilishi kiunzikuu zake mpya zinaweza kupunguza gharama ya nishati kwa ajili ya nguvu na upoozeshaji kwa vituo vya data, na pia zinaweza kupunguza mahitaji ya nafasi halisi zikilinganishwa na server farms.

Sifa[hariri | hariri chanzo]

Ndani ya Tarakilishi kiunzikuu IBM System Z9

Tarakilishi kiunzikuu za kisasa zinaweza kutumia namna nyingi tofauti za mifumo tendaji kwa pamoja. Hii mbinu ya mitambo ya kweli lakini si bayana inawezesha vitumika kutumika kama vile vipo kwenye taralikishi asili dhahiri. Katika dhima hii, kiunzikuu moja inaweza kuchukua nafasi ya huduma za vifaa tendaji vya hali ya juu na kuwa seva za kawaida.

Wakati tarakilishi kiunzikuu zinaasisi uwezo huu, zile hali zisizo bayana zinapatikana katika familia nyingi za mifumo ya tarakilishi, ingawa si moja kwa moja katika kiwango sawa au usawa wa usasa.

Tarakilishi iunzikuu zinaweza kuongeza au kufanyia mbadiliko moto uwezo wa mfumo bila kuvuruga utendaji wa mfumo, kwa udhahiri na uchembe wa viwango vya kisasa ambavyo si kawaida kupatikana kwenye tatuzi nyingi za seva. Tarakilishi viunzikuu za kisasa zikitambulisha IBM zSeries, seva za System z9 na System z10, zinatoa viwango viwili vya kweli isiyo bayana; migawanyo mantiki (LIPARs, kupitia nyenzo PR/SM) na mitambo isiyo bayana (kupitia mfumo tendaji Z/VM).

Wateja wengi wa Viunzikuu wanatumia mashine mbili, moja katika vituo data vyao vya msingi, na moja katika vituo data vya kutunzia nakili za kumbukumbu – kwa utendaji mzima, utendaji kiasi, au inayosubiria – kama ikitokea balaa itakayoathiri mjengo wa kwanza, jaribio, maendeleo, mafunzo, na kazi za uzalishaji wa vitumika na kanzidata zinazoweza kutumika kwenye mashine moja, isipokuwa kwa mahitaji makubwa sana ambapo uwezo wa mashine moja unaweza ukawa na mpaka.

Uwekaji kama huu wa Viunzikuu mbili unaweza kusaidia huduma za kibiashara endelevu, ukizuia kwa pamoja uhaba uliopangwa na ambao haukupangwa. Kiutendaji wateja wengi wanatumia Viunzikuu nyingi zilizounganishwa eidha kwa Sysplex sambamba na kushirikiana na DASD (katika mtazamo wa IBM), au kwa kushirikiana vihifadhi data vilivyo mbali kieneo vitolewavyo na EMC au Hitachi.

Viunzikuu zimeundwa kushughulika na wingi mkubwa wa input na output (I/O), na kutia mkazo mchakato wa kazi. Tangu mwishoni mwa miaka ya 1950, miundo ya Viunzikuu iliwekewa vifaa saidizi (vilivyoitwa mikanda au vichakata vya kiungoni) ambavyo vilisimamia vifaa vya I/O, vikiiacha huru CPU ihusike tu na vitunza kumbukumbu vyenye kasi kubwa.

Ni kawaida kwenye maduka ya Kiunzikuu kuhusika na kanzidata kubwa na mafaili. Mafaili yenye ukubwa wa Gigabyte mpaka terabyte si yasiyo ya kawaida. Ikilinganishwa na tarakilishi binafsi (PC), kwa kawaida Viunzikuu zina mara mia kwa maelfu ya vitunza data vitumikavyo, na vinaweza kufikiwa kwa kasi. Familia nyingine za seva pia zinapunguza kazi za I/O na kutilia mkazo mchakato wa kazi.

Mainframe return on investment (ROI), kama jukwaa lingine lolote la mchakato, ni tegemezi katika uwezo wake wa kupima, kuhimili kazi michanganyiko, upunguzaji gharama za leba, ufikishaji huduma usiopingika kwa matumizi muhimu ya kibiashara, na vipengele vingine kadhaa vya gharama vilivyopunguzwa hatari.

Mini Computers[hariri | hariri chanzo]

Aina hizi za kompyuta zilidhihiri katika kipindi cha miaka ya 60. Ni kompyuta zenye umbile dogo kuliko zile zilizotangulia kutajwa, na ni bora kwa kuunganishia kompyuta nyingine zinazotumika viwandani na ndani ya nchi.

Micro Computers[hariri | hariri chanzo]

Aina hii ya kompyuta inakusanya aina zifuatazo:

Kompyuta za Kibinafsi (PCs) ambazo ni maalumu kwa ajili ya matumizi ya mtu mmoja tu. Home Computers, Portable Computers: Nazo ni kompyuta za kubeba mkononi, ambazo zimegawanyika katika aina zifuatazo:

 • 1. Laptop.
 • 2. Notebook.
 • 3. Palmtop.

Kazi za msingi zinazofanyika ndani ya kompyuta[hariri | hariri chanzo]

 1. Kazi za uingizaji (Input).
 2. Kazi za uwendeshaji au ufanyishaji (Proccessing).
 3. Kazi za utoaji (Output).
 4. Kazi za kuhifadhi (Storage)

Matumizi ya kompyuta[hariri | hariri chanzo]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na kuendelea kwa elimu ya teknolojia imetusaidia sana kujifunza mambo mbali mbali kupitia kompyuta, ambapo unaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kuuliza maswali na kujibiwa kwa haraka tena kwa njia tofauti, pia unaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kielimu, pia unaweza kuandaa vipindi mbali mbali vya masomo na kufundishia elimu tofauti. Pia unaweza kuonyeshea filamu zenye mafundisho mazuri, kama kuonyesha filamu zenye elimu ya jeografia na sayansi ya mifugo na kilimo, kuonyesha sehemu muhimu za nchi yetu, kuonyesha athari za nchi ambazo ndiyo sehemu kuu zinazotuletea fedha za kigeni katika nchi yetu, na kuonyesha picha za maendeleo katika sekta mbali mbali za nchi yetu, pia kuonyeshea mila na tamaduni za taifa letu la Tanzania na mataifa mengine mbali mbali duniani na kadhalika.

Michezo[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta zimeandaliwa ndani yake programu mbali mbali zenye michezo tofauti, ambayo inaweza kutumika na watu mbali mbali kutofautiana na umri wao, na ambayo inajulikana kama moja ya kazi za kukuza kipaji na kuchangamsha akili, na ni sehemu moja wapo ya kuburudisha nafsi.

Ufundi[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta zinaweza kutumika kwa ajili ya kufanyia kazi za ufundi, kama kuchora ramani ya nyumba na mazingira ya nje ya nyumba, kutengenezea picha kwa kuibadilisha na kuiremba na kuifanya ionekane katika sura nyengine ambayo ni tofauti na ile ya asili.

Mawasiliano[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta inaweza kutumika kwa ajili ya kufanyia mawasiliano kupitia mtandao wa (Internet) ambao leo hii ndiyo umeshika nafasi kubwa sana ya mawasiliano kuliko kitu chengine ulimwenguni, kama kuwasiliana kwa kutumiana ujumbe wa barua pepe (E-mail) ambayo ni rahisi na inafika haraka kuliko barua za kupitia posta, pia kwa kutumia barua pepe hakuna haja ya kufikiria sehemu aliko mtu America au bara hindi au sehemu nyengine duniani, kuwasiliana kwa maneno ya maandishi (Chat), pia kuwasiliana kwa maneno ya sauti na kuonekana picha (video chat.)

Usafirishaji[hariri | hariri chanzo]

Kwa kutumia kompyuta unaweza kuendeshea kazi za usafirishaji katika vituo vikuu vya usafirishaji, kama usafiri wa ardhini (mabasi, metro na treni), usafiri wa majini (meli), na usafiri wa angani (ndege).

Matumizi ya kiwandani[hariri | hariri chanzo]

Kama kuendeshea mashine viwandani kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbali mbali, kama kutengenezea magari, kuzalishia umeme na kutengenezea bidhaa nyengine za kawaida kama nguo mazulia na kadhalika.

Matumizi ya benki[hariri | hariri chanzo]

Kama ilivyokuwa ada na kawaida hivi sasa kutumia kompyuta kwa ajili ya kuendeshea kazi za benki,kwa ajili kurahisisha kazi za mahesabu.

Kufanyia matibabu[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta zimekuwa na matumizi makubwa na muhimu sana katika kufanyia uchunguzi na matibabu hospitalini, kama kuchunguza na kuelekeza dawa ya kutibu ugonjwa uliyoonekana, pia kupimia na kujaribia mimba na kutoa maelekezo kuhusiana na siku na tarehe ya kujifungua.

Kazi za Kompyuta[hariri | hariri chanzo]

Kuhifadhi vitu (Data)[hariri | hariri chanzo]

Kama ilivyotanguliwa kusemwa hapo awali kuwa kompyuta ni chombo pekee chenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu, na mpaka hivi sasa bado hakijapatikana chombo chengine chenye uwezo mkubwa wa kuhifadhia vitu zaidi ya kompyuta.

Kuonyeshea matokeo ya vitu (Data na Information)[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na kuendelea elimu ya teknolojia imeweza kuturahisishia kazi zetu nyingi ambazo tulikuwa tunazifanya kupitia vyombo mbalimbali. Kila chombo kilikuwa na kazi yake maalumu, tofauti na kompyuta ambapo mtu anaweza kuanzisha au kutengeneza kitu na wakati huohuo anaweza kukionyesha kwa kutumia kompyuta yenyewe, yaani kuonyesha ufanisi na sura nzuri ya kitu kilichofanyika.

Kompyuta imegawanyika katika sehemu kuu mbili[hariri | hariri chanzo]

Sehemu zinazoshikika (Hardware)[hariri | hariri chanzo]

Sehemu zinazoshikika (Hardware), ni aina zote za vifaa vya kompyuta, navyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu.

Vifaa vya kuingizia vitu (Input devices)[hariri | hariri chanzo]

 1. Baobonye (pia: kibodi (keyboard)
 2. Puku] au Kipanya (Mouse)
 3. Skana (Scanner)
 4. Mikrofoni (Microphone)
 5. Kamera (Camera)
Baobonya / Kibodi (keyboard)[hariri | hariri chanzo]

Kibodi inatumika kwa ajili ya kuingizia herufi, namba, alama na michoro, nayo imegawanyika katika sehemu kuu nne, nazo ni kama ifuatavyo: Funguo za kuandikia (Typewriter keys), funguo za kuhama (Movement keys), funguo za namba pamoja na michoro mingine (Numeric keys) na funguo za kazi Function keys).

Jedwali linaloonyesha funguo na kazi zake[hariri | hariri chanzo]

Jina la funguo Kazi yake Home Inatumika kwa ajili ya kuhamia mwanzo wa mstari End Inatumika kwa ajili ya kuhamia mwisho wa mstari.

Inatumika kwa ajili ya kuhamia juu ya mstari.

Inatumika kwa ajili ya kuhamia upande wa kushoto mwa mstari.

Inatumika kwa ajili ya kuhamia upande wa kulia mwa mstari.

Inatumika kwa ajili ya kuhamia chini ya mstari. Pg Up Inatumika kwa ajili ya kuhamia juu ya mstari. Pg Dn Inatumika kwa ajili ya kuhamia chini ya mstari. Num lock Inatumika kwa ajili ya kufunga na kufungulia namba na michoro. Caps lock Inatumika kwa ajili ya kufunga na kufungulia. Enter Inatumika kwa ajili ya kutekeleza amri, au kuanzisha fungu la maneno kwenye ukurasa.. Del “Delete” Inatumika kwa ajili ya kufuta herufi ya mbele yake.

“Back space" Inatumika kwa ajili ya kufuta herufi ya nyuma yake. Space “Space bar” Inatumika kwa ajili ya kuweka masafa kati ya maneno. Esc “Escape” Inatumika kwa ajili ya kuacha kutekeleza amri. Tab Inatumika kwa ajili ya kuwacha masafa maalumu tofauti na ya kawaida (Normal).

Ctrl “Control” inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu. Alt inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu. Shift inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu. Alt-Shift Inatumika kwa ajili ya kubadilishia lugha. Ctrl-Shift Inatumika kwa ajili ya kubadilishia mwelekeo ndani ya ukurasa (kulia au kushoto) Print screen Inatumika kwa ajili ya kupiga picha kitu chochote kwenye kompyuta.

Ctrl-Alt-Del Inatumika kwa ajili ya kuwasha upya kompyuta.

Kipanya (Mouse)[hariri | hariri chanzo]

Kuna vitufe viwili kwenye kila mausi, kitufe cha upande wa kushoto (Left click) kinatumika kufungulia windozi, programu na kuchagulia maandishi, maneno na picha, na kitufe cha upande wa kulia (Right click) kinatumika kufungulia orodha ya mapendekezo ya kazi.

Skana (scanner)[hariri | hariri chanzo]

Skana inatumika kwa ajili ya kuingizia picha ndani ya kompyuta. Na kitu chochote kile kinachoingia ndani ya kompyuta kwa njia ya skana kinapewa sifa ya picha.

Mikrofoni (microphone)[hariri | hariri chanzo]

Makrofoni inatumika kwa ajili ya kuingizia sauti ndani ya kompyuta.

Kamera (camera)[hariri | hariri chanzo]

Kamera inatumika kwa ajili ya kupigia picha na kuingiza ndani ya kompyuta.

Vifaa vya kutolea vitu (Output devices)[hariri | hariri chanzo]

Skrini (screen)[hariri | hariri chanzo]

Skrini inatumika kwa ajili ya kuonyeshea matokeo ya vitu vilivyofanyika ndani ya kompyuta.

Kipaza sauti (speaker)[hariri | hariri chanzo]

Kipaza sauti kinatumika kwa ajili ya kutolea sauti kutoka ndani ya kompyuta.

Printa (printer)[hariri | hariri chanzo]

Printa inatumika kwa ajili ya kutolea vitu vya maandishi au picha kwenye kompyuta kwa njia ya karatasi (kuchapisha).

Plota (ploter)[hariri | hariri chanzo]

Plota ni chombo kinachotumika kwa ajili ya kutolea vitu, ambacho kinafanana na printa katika ufanisi wake wa kazi, lakini umbile lake ni kubwa kuliko printa, na kinatumika kwa ajili ya kuchapishia picha na michoro ya kiufundi, pia kinaweza kutumika kwa ajili ya kuchapisha maandishi kama herufi namba na alama.

Sehemu zisizoshikika (Software)[hariri | hariri chanzo]

Kompyuta haiwezi kufanya kazi mpaka kipatikane kitu kinachoitwa software, ambacho kinawakilisha programu zinazoendesha kompyuta. Programu hizo zimegawanyika katika sehemu kuu mbili:

1. Programu za kuendeshea kompyuta (operating systems): programu hizo zinaitwa Windows, na kuna aina nyingi za Windows kulingana na toleo lake na ubora wake, kwani siku zinavyozidi kwenda mbele ndipo tunapozidi kupokea programu nyingine za Windows zenye ubora zaidi kuliko zile za awali.

2. Programu za kufanyia kazi (application systems), nazo ni: Microsoft Office na Graphics design; programu hizo daima zinafanya kazi ndani ya windows, ambazo zinatumika kwa ajili ya kazi mbalimbali za uandishi na hesabu, na kazi nyinginezo za kuunda na kutengeneza picha n.k.

Vifaa vya kuendeshea vifaa vya kuingizia na kutolea vitu:[hariri | hariri chanzo]

Vifaa hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho C.P.U. (kifupi cha Central Processing Unit), ambacho ni kiini cha kompyuta na ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vyote vya kompyuta na kutoa maelekezo yote.

C.P.U. ni sehemu kuu ya nguvu ya kompyuta, au kitovu cha kompyuta. Kazi za C.P.U. ni:

Kutawala (Control)[hariri | hariri chanzo]

Ndani ya madhabodi (Motherboard) kinapatikana kifaa kinachoitwa Bios (kifupi cha Basic Input Output System), ambacho ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vya kuingizia na kutolea vitu. Ni vigumu kufuta au kurekebisha vitu vilivyomo ndani ya kifaa hicho kwani vinazingatiwa ni vitu vya kusomea tu na si kwa kazi nyingine.

Akili na mahesabu (arithmetic logical)[hariri | hariri chanzo]

Kazi za mahesabu ni kazi zote zinazofanywa na hesabu, kama vile kutoa, kujumlisha, kuzidisha na kugawanya. Na za akili

Windows XP[hariri | hariri chanzo]

Windows Xp inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa Windows za kisasa zenye kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko zile za zamani, kama Windows 95, Windows 98 na Windows Millenium.

Sifa za windows XP[hariri | hariri chanzo]

 1. Wepesi wa kuanza na kumaliza kutumia.
 2. Uwezo wa kutumia lugha mbili mfano kingereza na kiarabu, pia uwezo wa kubadilisha lugha hizo na kuweka nyengine.
 3. Kufungua kurasa kwa haraka.
 4. Uwezo wa kuendesha programu zaidi ya moja katika wakati mmoja.(Multitasking)
 5. Uwezo wa kuhifadhi vitufe (files) vilivyofutwa katika recycle bin.
 6. Uwezo wa kufanya kazi katika mdahalishi (Network) kwa haraka.
 7. Uwezo wa kubadilishana vitu (Data) kati ya programu tofauti.
 8. Kutumia majina marefu zaidi ya herufi 255 katika jina la faili moja.
 9. Haraka na wepesi katika utekelezaji.
 10. Vifaa vya kisasa vinavyowezesha kufanya kazi katika net.
 11. Uwezo wa kutambua idadi nyingi ya vyombo vilivyounganishwa ndani ya kumpyuta.
 12. kuwepo kwa picha nyingi zenye kuvutia kwa ajili ya kupamba skirini (Backgrounds).

Kuanza kutumia Windows[hariri | hariri chanzo]

Kabla hujaanza kutumia Windows unatakiwa kufanya mambo yafuatayo:

 • 1. Kuhakikisha waya wa umeme umeshaunganishwa kwenye kompyuta yako.
 • 2. Kufungua kompyuta kwa kutumia sehemu inayoitwa power.
 • 3. Kusubiri mpaka idhihiri sehemu inayoitwa desktop.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]