Kipanya (kompyuta)
Kipanya cha kompyuta (pia: puku) ni kifaa cha kuingizia data katika tarakilishi.
Kipanya hushikwa kwa mkono na kusukumwa mezani. Mwendo wake husababisha mshale wa kasa (kielekezi) kutembea kwenye kiwamba.
Mtumiaji hulenga kwa mshale huko anapochagua kotoa amri kwa kubofya kitufe cha kipanya. Tendo hili lasababisha amri inayoonekana kama alama au mchoro kwenye skrini kutekelezwa na programu ya kompyuta.