Nenda kwa yaliyomo

Neva

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfumo wa neva wa binadamu
Muundo wa seli za neva aina neuroni

Neva (kutoka Kilatini nervus kupitia Kiingereza nerve, asili kutoka Kigiriki νεῦρον, nevron inayomaanisha "uzi", "kamba"), pia mishipa ya fahamu, ni kundi la seli za pekee mwilini zenye kazi ya kuwasilisha habari kati ya ubongo na sehemu za mwili.

Kazi ya neva[hariri | hariri chanzo]

Tukigusa kitu cha moto kwa kidole, tunaondoa mkono mara moja, wakati mwingine hata kabla ya kusikia bado maumivu makali na bila kutafakari muda mrefu. Sababu yake ni nini? Seli za kuhisi mkononi zimetambua joto kubwa ambalo ni hatari kwa ngozi, zimeashiria habari hii kwa seli za neva zinaounganishwa nazo na hizi zimepeleka habari ya hatari hadi ubongo.

Ubongo unafanya tathmini ya haraka na kuamuru musuli za mkono kusogeza kidole mbali na joto. Amri kutoka ubongo unapita tena seli za aina zilizoashiria habari kuhusu hatari ya joto hadi ubongo.

Seli hizi za pekee zenye uwezo wa kuwasilisha habari na amri kati ya ubongo na sehemu za mwili huitwa neva au mishipa ya fahamu.

Mfumo wa neva[hariri | hariri chanzo]

Kitovu cha mfumo wa neva ni ubongo, hapo linatoka fungu kuu la neva ambayo ni ugwemgongo na fungu hilo linaendelea kwenye nafasi iliyopo ndani ya mifupa ya uti wa mgongo inayokinga seli za neva hizo. Kutoka hapo fungu dogo zaidi zinatoka na kuelekea pande zote za mwili kama matawi au mizizi ya mti. Ubongo wenyewe umejengwa kwa seli za neva.

Neva zinapitia mwili mzima kwa umbo la nyuzi ndefu.

Katika mfumo wa neva kuna aina mbili za seli hasa:

  • neuroni (nyuroni, ing. neuron) zenye kazi ya kupitisha habari
  • glia ambazo zina kazi ya kupeleka damu na lishe kwa seli za neuroni halafu shughuli za kuratibu neuroni zisizotambulika bado kikamilifu.

Neuroni mara nyingi zina sehemu zinayotoka nje ya mwili wa seli yenyewe, hasa mihimili ya seli (ing. axon) inayoweza kuwa mirefu (baina ya 1 mm hadi 1 m kwa binadamu).

Halafu kuna matawi inayotoka kwenye mwili wa neuroni.

Mwishoni kuna vidole vinavyofikia kwenye vidole vya seli nyingine. Seli haziunganishwi moja kwa moja: kuna mapengo madogo kati ya seli zinazoitwa sinapsi[1].

Kupitisha misukumo ya umeme na kikemia[hariri | hariri chanzo]

Kupitisha msukumo kutoka neva moja kwenda nyingine: Natiri njano inaingia katika seli, kali (potasiamu) nyekundu inatoka na neurotransmita kibichi inapita sinapsi hadi vidole vya upande mwingine

Ndani ya seli misukumo ya habari inawasilishwa kwa mishtuko hafifu ya umeme hadi vidole vya matawi au mhimili. Kutoka hapa hadi vidole vya seli nyingine mbali ni ndogo sana na hapo alama za ahbari zinawasilishwa kwa njia ya kikemia; mara nyingi mawasiliano yanatokea kutoka mhimili kwenda matawi lakini kuna pia seli ambazo zinawasiliana mhimili-mhimili au tawi-tawi. Kwa misukumo ya kikemmia kwenye sinapsi kuna madawa yaliyo tayari kwenye vidole hivi ambavyo vinaachisha ioni kuelekea upande mwingine ya sinapsi zinazopokelewa pale na kusababisha mshtuko wa umeme unaopita ndani ya neuroni jirani. Kwa njia misukumo ya habari inapita haraka sana mwilini baina ubongo na sehemu za mwili.

Kati ya madawa muhimu yanayotumiwa na neuroni nyingi iko kolini asetili (acetylcholine, ACh), pia kuna mengine. Kwa jumla madawa haya huitwa neurotransmita (ing. neurotransmitter).

Maradhi ya neva[hariri | hariri chanzo]

Neva zinaweza kuathiriwa na maradhi. Kuna maradhi mbalimbali pamoja na

  • Jeraha - neva zinaweza kujeruhiwa kwa kukatwa au kutwangwa
  • sumu zinaweza kuathiri neva ambazo ni pamoja na alikoholi, risasi (metali), madawa ya kulevya
  • Ambukizo
  • Magonjwa kwa mfano usukari na ukoma.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Synapse - at neuroscience for kids

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neva kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.