Nyuzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pembe kali ya nyuzi 45°

Nyuzi (pia: digrii kutoka neno la Kiingereza) ni kizio cha kupimia pembe . Msingi wake ni mzunguko kamili wa duara unaogawiwa kwa sehemu 360. Kwa kawaida nyuzi moja huandikwa kama .

Nusuduara ina 180°. Pembemraba ina 90°. Jumla ya pembe ndani ya pembetatu ni 180°, ndani ya mstatili ni 360°.

Nyuzi inaweza kugawiwa tena kwa dakika na sekunde ya tao. Dakika ya tao ni sehemu ya 60 na sekunde ya tao ni sehemu ya 3600 ya nyuzi moja.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Asili ya hesabu hii huaminiwa kuwa katika Babeli ya Kale. Wababeli walihesabu mwaka kuwa na siku 360 na wakitazama nyota waliona ya kwamba kila siku zilihama takriban kiwango cha 1/360 cha duara.

Katika jiometria muundo huo ulielezwa kimsingi na mwanaastronomia Hipparchos wa Nikaia (190 KK120 KK).

Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyuzi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.