Hipparchos wa Nikaia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hipparchos

Hipparchos (kwa Kigiriki Ἵππαρχος; takr. 190 KK hadi takr. 120 KK) alikuwa mtaalamu wa astronomia, jiografia na hisabati wa Ugiriki ya Kale.

Alizaliwa mjini Nikaia (leo: Iznik katika Uturuki) akafariki kwenye kisiwa cha Rhodos.

Hutazamwa kama mwanaastronomia muhimu kabisa wa nyakati za kale.

Aliorodhesha nyota 800 na kuzichora katika ramani ya anga. Alibuni mfumo wa kutofautisha nyota kwa uangavu unaoonekana.

Aliweza kukadiria na kutabiri kupatwa kwa jua .

Katika hisabati alianzisha mbinu za kijiometria, kwa mfano mgawanyo wa duara kuwa na nyuzi 360.