Kupatwa kwa jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kupatwa kwa jua tar. 29 Machi 2006

Kupita kwa kivuli cha mwezi duniani wakati wa kupatwa kwa jua. Watu katike eneo kubwa la giza waliona kupatwa kwa jua kisehemu. Nukta nyeusi yaonyesha sehemu ambako jua lilipatwa kabisa.
"Central duration" inataja muda wa kupatwa kabisa kwenye kitovu cha kivuli; namba katika kona ya juu huonyesha saa za tar. 29 Machi kupatwa kulipotokea.

Kupatwa kwa Jua (ing. solar eclipse) ni hali ya Jua kutoonekana (au kuonekana kisehemu tu) angani wakati wa mchana kwa muda fulani hata pasipo na mawingu. Kunatokea wakati mwezi unapita kati ya jua na dunia na kufunika jua. Tokeo lake ni kupungua kwa jua hadi kutoonekana tena na kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu.

Kunatofautishwa kati ya „Kupatwa kisehemu“ (ing. partial eclipse) na „Kupatwa kabisa“ (ing. total eclipse). Kupatwa kwa Jua kunatokea kila mwaka, angalau mara mbili hadi mara tano. Lakini kupatwa kabisa kwa Jua haiwezi kutokea zaidi kuliko mara mbili kwa mwaka.[1][2].

Misingi ya kupatwa kwa jua[hariri | hariri chanzo]

Kupatwa kwa jua.PNG

Kupatwa kwa jua kunatokea kama Dunia, Mwezi na Jua zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya Dunia na Jua. Katika hali hiyo kuna kivuli cha Mwezi kwenye uso wa Dunia. Kivuli hiki hakifuniki Dunia yote. Ni kama mlia kwenye uso wa Dunia. Nje ya mlia huu Jua linaonekana kisehemu au bila upungufu.

Hali ya kupatwa kabisa kwa jua inatazamiwa kila mara kwenye mstari mwembamba kwenye uso wa Dunia tena giza kabisa kwa muda mfupi. Mstari huu ni njia ya kitovu cha kivuli cha mwezi. Nje ya njia hii kupatwa kwa jua kunaonekana kisehemu tu. Mbali na njia ya kivuli hiki jua linaonekana kama kawaida.

Aina za kupatwa kwa jua[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa jua.

  • kupatwa kabisa: jua lapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii yaonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli.
  • kupatwa kipete: mwezi huonekana mdogo kuloko jua. Kwa hiyo duara ya kung'aa ya jua ni kubwa kuliko duara ya mwezi na mwanga wa jua waonekana kama pete.
  • kupatwa kwa jua kisehemu: Katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu huona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali na kitovu cha kivuli. Wakitazama jua kwa filta kwa mfano kioo kilichopakwa dohani katika moshi ya mshumaa huwa wanaona sehemu ya duara ya jua imefunikwa.

Mpito wa sayari[hariri | hariri chanzo]

angalia Mpito wa Zuhura

Wakati sayari inapita kati ya Jua na Dunia inafunika sehemu ya Jua. Tofauti haionekani kwa macho lakini inaweza kutazamiwa kwa kutumia darubini. Kuna sayari mbili zinazoweza kupita mbele ya Jua kwa macho ya mtazamaji duniani, ni Utaridi (Mercury) na Zuhura (Venus).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Littmann, Mark; Fred Espenak, Ken Willcox (2008). Totality: Eclipses of the Sun. Oxford University Press, 18–19. ISBN 0199532095. 
  2. Kupatwa kwa jua kulitokea mara tano katika mwaka 1935 NASA (6 September, 2009). "Five Millennium Catalog of Solar Eclipses", NASA Eclipse Web Site, Fred Espenak, Project and Website Manager. Retrieved on 26 January 2010. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Usalama wa mcho wakati wa kuangalia[hariri | hariri chanzo]