Darubini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Darubini ya mkononi[1]
Darubini kubwa ya lenzi[2][3]
Darubini redio kubwa


Darubini (kutoka Kiajemi دوربين dorbin) ni kifaa cha kutazamia vitu ambavyo ni mbali. Kutegemeana na kusidi lake kuna aina mbalimbali:

  • darubini ndogo za mkononi ni vyombo vinavyotumiwa na wapenda mazingira asilia, wavindaji, polisi na jeshi.

Darubini kubwa hupatikana mara nyingi katika vituo vya astronomia kuna hasa aina mbili

  • darubini maonzi kubwa hutumiwa na wanaastronomia kwa kutazama magimba ya angani kama jua, mwezi, nyota, sayari au kometi.
  • darubini redio hutumiwa pia na wanaastronomia zikikusanya mishale ya sumakuumeme zinazofaa kutupa picha za violwa vya mbali sana zisizoonekana kwa njia ya nuru ya kawaida. Zinafaa pia kuonyesha tabia za violwa vya angani vya karibu zaidi zisizoonekani wka njia ya nuru.

Darubini maonzi hutumia ama lenzi pekee au kiakisi pamoja na lenzi.

Historia ya darubini[hariri | hariri chanzo]

Darubini ya kwanza inayojulikana ilitengenezwa mwaka 1608 na Mholanzi Hans Lipperhey aliyekuwa fundi miwani. Mfano wake ulichukuliwa na kuboreshwa na mwanaastronomia Mwitalia Galileo Galilei aliyeanza kuitumia mwaka 1610 kwa kuangalia nyota. Aligundua mara moja miezi ya sayari Mshtarii. Aina nyingine ya darubini ilielezwa na Mjerumani Johannes Kepler mwaka 1611.

Muundo tofauti uligunduliwa na padre Nicolaus Zucchius mwaka 1616 iliyotumia kiakisi parabola kwa kukusanya mishale ya nuru.

Katia karne zilizofuata vyombo hivi viliendelea kuboreshwa. Mtambo mpya ulipatikana katika karne ya 20 kwa kutumia mnururisho wa sumakuumeme kutoka kwa nyota iliyoendelezwa kuwa darubini redio.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: