Makemake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Artist's conception of Makemake, by Ann Feild (Space Telescope Science Institute)

Makemake (tamka "ma-ke-ma-ke"; jina rasmi 136472 Makemake) ni sayari kibete inayozunguka jua letu katika umbali mkubwa kwenye ukanda wa Kuiper.


Iligunduliwa tarehe 31 Machi 2005 na wanaastronomia Michael E. Brown, Chad Trujillo na David Rabinowitz kwenye kituo cha nyota Palomar.

Jina

Jina lilichaguliwa kutokana na mungu mwuumbaji aliyeitwa "Makemake" katika dini asilia ya Kisiwa cha Pasaka. Kuna mapatano katika Umoja wa kimataifa ya astronomia kutumia majina ya miungu ya dini mbalimbali kwa magimba yanayoendelea kugunduliwa katika ukanda wa Kuiper. Asili ya jina iko katika lugha ya Kipolinesia na katiki dini yao ni mwuumbaji wa binadamu na mungu wa rutba. Makemake aliabudiwa katika ibada kwa umbo la ndege wa bahari. Ishara yak ilikuwa mwanaume mwenye kichwa cha ndege.[1]

Muundo na tabia

Hakuna habari nyingi za uhakika kutokana na umbali na kwa sababu hadi sasa hakuna chombo cha angani kilichopita karibu nayo. Lakini Makemake inaonekana ni hasa mwamba na barafu ilhali katika ubaridi mbali na jua barafu huwa ngumu kama mwamba.

Marejeo

  1. Fourth dwarf planet named Makemake, tovuti ya Ukia, 19 Julai 2008, iliangaliwa Julai 2017

Viungo vya Nje

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makemake kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.