Mshtarii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha ya Mshtarii iliyopigwa na chombo cha angani Cassini

Mshtarii (pia Mshiteri, Mushtarii au Mshatira[1] , kutokana na Kiarabu "المشتري" al-mshtari; na hata Jupita kutokana na Kiingereza Jupiter[2]) ni sayari ya tano toka kwenye jua katika Mfumo wa jua na sayari zake.

Ulinganishi wa ukubwa wa Dunia yetu (kushoto) na Mshtarii pamoja na "doa jekundu" inayozunguka katika angahewa ya Mshtarii

Mshtarii ni sayari kubwa kabisa ya jua letu. Maada yake inazidi mara mbili na nusu maada ya sayari zote nyingine pamoja.

Angahewa[hariri | hariri chanzo]

Uso wa sayari hauonekani kwa sababu angahewa nzito inafunika kila sehemu. Maada ya angahewa ni hasa hidrojeni na heli. Kutokana na uzito wa angahewa shinikizo ndani yake inaongezeka sana katika vilindi vyake na kusababisha gesi za angahewa kuingia katika hali ya giligili (majimaji) inayobadilika kuwa mango (imara) ndani zaidi. Zamani iliaminika ya kwamba sayari yenyewe ni ya gesi iliyoganda lakini siku hizi wataalamu wa astronomia huamini ya kwamba kuna kiini cha mwamba au metali.

Doa jekundu linaloonekana usoni mwa angahewa ni dhoruba ya tufani kubwa sana iliyotazamwa mara ya kwanza miaka 300 iliyopita wakati darubini za kwanza zilipopatikana. Duniani tufani zinapotea kwa kawaida baada ya wiki kadhaa lakini doa jekundu limeendelea bila kusimama.

Miezi[hariri | hariri chanzo]

Mshtarii ina miezi 63 zilizotambuliwa hadi mwaka 2005.

Miezi minne mikubwa ilitambuliwa mwaka 1610 na Galileo Galilei aliyekuwa kati ya wanaastronomia wa kwanza waliotumia darubini. Ndiyo Io, Europa, Ganimedi na Kallisto. Ukubwa wa Ganimedi unakaribia kipenyo cha Utaridi ukipita kile cha Pluto. Mwezi mdogo kabisa wa Mshtarii unajulikana kwa namba tu na una kipenyo cha km 1.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. kuhusu majina ya sayari zilizojulikana kwa Waswahili na hivyo kuwa na majina ya asilia linganisha Jan Knappert, Swahili Islamic poetry, Brill 1971, Vol 1 uk 96-97 - taz google booksearch [1]
  2. Umbo nyingine ni Sumbula inayotumiwa kwa kosa na vitabu kadhaa za shule pia na kamusi chache. Sumbula ni jina la la Kiswahili la nyota Alfa Virginis au en:Spica, si la sayari yoyote
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mshtarii kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano