Pluto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhusu matumizi ya jina "Utaridi" kwa sayari hii tazama chini kwa "jina"

Pluto.
<Njia ya Pluto ya kuzunguka jua inakata njia ya Neptune - hali halisi njia ya Pluto ni duaradufu

Pluto (alama: ⯓[1] au ♇[2]) ni sayari kibete inayozunguka jua ng'ambo ya obiti ya Neptuni.

Masi yake ni hasa mwamba na barafu. Kipenyo chake ni km 2,390.

Katika mwendo wake inakata njia ya Neptune kwa sababu njia yake ina umbo la duaradufu kali.

Miezi

Pluto ina miezi mitano inayoitwa Charon, Styx, Nix, Kerberos na Hydra. Charon ni kama nusu ya ukubwa wa Pluto (kipenyo km 1200) na umbali wa wastani ni km 19,410. Styx, Nix, Kerberos na Hydra ni miezi midogo (vipenyo: km 10-25, 56x26, 31 na 43x33) yenye umbali wa km 42,600, 48,600, 57,700 na 64,700 kutoka Pluto.

Sayari au sayari kibete?

Pluto ilikuwa ikitambulika kama sayari ya tisa katika mfumo wa Jua toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006. Vipimo vipya vilileta wasiwasi juu ya swali: Je, sayari ni kitu gani?, hasa baada ya kugundua magimba ya ziada nje ya Pluto yanayokaribia ukubwa wake lakini hayafai kuitwa sayari.

Umoja wa kimataifa wa wanaastronomia uliondoa Pluto katika orodha ya sayari kwenye mkutano wake wa mwaka wa 2006. Badala yake wameiita sayari kibete. Hata hivyo baadhi ya wanaastronomia walipinga uamuzi huu.

Jina

Jina "Pluto" linamtaja mungu mtawala wa kuzimu katika mitholojia ya Roma ya Kale. Limechaguliwa kwa sayari hii kutokana na umbali wake na jua na giza kubwa liliko sawa na hali ya giza ambayo ni mfano wa kuzimu.

Vitabu kadhaa vinatumia jina la Kiswahili Utaridi[3] [4] [5] kwa kufuata kamusi ya KAST; lakini mabaharia Waswahili wametumia jina hili la "Utaridi" tangu miaka mingi kwa ajili ya sayari ya kwanza (ing. "Mercury").[6]

Marejeo

  1. JPL/NASA (2015-04-22). What is a Dwarf Planet?.
  2. John Lewis, ed. (2004). Physics and chemistry of the solar system (2 ed.). Elsevier. p. 64. 
  3. Wallah, W.B. & Mwamburi, J. Kiswahili mufti darasa la 8: Mwongozo wa mwalimu. Longhorn, 2009. ISBN 99966491066
  4. TESSA - Teacher Education in Sub Saharan Africa. Nishati na Mwendo: Kutoka Ardhini kenda kwenye nyota – kutumia Zana Kifani Archived 9 Aprili 2016 at the Wayback Machine.. Available at: www.tessafrica.net
  5. Waweru, M.; Makombo, H; Vonuoli, A.; Kashihiri, C.; Mwayani, J.Hutua za Kiswahili: Masomo ya Msingi 8. East African Educational Publishers ltd., 1ed, 290p., 2005. ISBN 9966-25-403-X
  6. KAST ni kamusi ya pekee inayotumia "Utaridi" kwa sayari hii. KKK/ESD ya TUKI inaonyesha Pluto. Linganisha ukurasa wa Majadiliano:Sayari

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pluto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.