Ukanda wa Kuiper

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ugawaji wa magimba ya ukanda wa Kuiper (nukta kijani)

Ukanda wa Kuiper (ing. Kuiper belt) ni eneo la mfumo wa jua letu nje ya obiti ya sayari Neptuni lililopo kwenye umbali wa vizio astronomia) kati ya 30 - 50 kutoka jua.

Ukanda huu una umbo la wingu wa mviringo wa magimba ya angani; mengi yao ni madogo machache makubwa kwa hiyo ukubwa kati ya vumbi na mawe hadi asteroidi na pia sayari kibete,

Ukanda wa Kuiper hufanana na ukanda wa asteroidi ulipo kati ya obiti za Mirihi (Mars) na Mshtarii (Jupiter) lakini ni kubwa zaidi. Upana wake ni mara 20 na unene wake mara 20-200.

Magimba ndani yake ni hasa aina mbalimbali za barafu kutokana na elementi zilizoonekana kama gesi katika mazingira ya dunia kama vile methani, amoni au maji. Wataalamu wanaamini leo ya kwamba chanzo cha magimba hasa ni mchakato wa kutokea kwa mfumo wa jua letu na kuzaliwa kwa sayari. Katika maeneo ya ndani ya mfumo wa jua mata ilijikusanya kutokana na graviti kuwa ama jua lenyewe au sayari. Hapa nje masi za magimba haizikutosha kuyavuta magimba mengine ili sayari kubwa itokee.

Hata hivyo kuna sayari kibete 3 zilizogunduliwa hadi sasa katika ukanda wa Kuiper ambazo ni Pluto, Haumea na Makemake.

Kuna pia nadharia ya kwamba miezi kadhaa katika mfumo wa jua letu ina asili yao katika ukanda wa Kuiper. Mifano ni Triton ya Neptuni na Phoebe ya Zohali. Miezi hii inaaminiwa ilijijenga katika ukanda wa Kuiper lakini ilivutwa ndani ya mfumo wa jua na kukamtwa na graviti ya sayari hizi.

Ukanda wa Kuiper uligunduliwa mwaka 1992 lakini iliwahi kutabiriwa na wataalamu mbalimbali pamoja na Gerard Kuiper.

Hadi sasa kuna magimba mnamo ya 1,000 yaliyogunduliwa kwa uhakika lakini inaaminiwa ya kwamba jumla ya magimba unaweza kufikia idadi ya malakhi au mamilioni.