Gerard Kuiper

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Gerard Kuiper (1905 - 1973)

Gerard Peter Kuiper (Kiholanzi: Gerrit Pieter Kuiper; 7 Desemba 1905 – 23 Desemba 1973) alikuwa mwanaastronomia kutoka nchini Uholanzi aliyeendelea kuishi Marekani.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kuiper alizaliwa kwenye familia ya fundi cherahani katika kijiji cha Uholanzi ya kaskazini. Tangu 1924 alisoma astronomia kwenye Chuo Kikuu cha Leiden. Jan Oort alikuwa kati ya walimu wake. Baada ya kumaliza shahada ya uzamivu kwa tasnifu kuhusu nyota pacha mwaka 1933 akapata nafasi ya kazi kwenye kituo cha nyota cha Chuo Kikuu cha Kalifornia, Marekani. Baadaye aliuwa profesa kwenye Chuo Kikuu cha Chicago na Chuo Kikuu cha Arizona.


Kazi[hariri | hariri chanzo]

Utafiti wale ulihusu hasa mfumo wa Jua letu. Aliweza kuthebitisha kuwepo kwa dioksidi kabonia katika angahewa ya sayari Mirihi (Mars). Alitambua pia angahewa za miezi ya sayari kadhaa kama vile kwenye Titan (mwezi wa Mshtarii), Miranda (mwezi wa Uranus) na Nereid (mwezi wa Neptuni).

Alitabiri kuwepo kwa ukanda wa asteroidi nje ya obiti ya Neptuni iliyothebitishwa baadaye na kupokea jina la Ukanda wa Kuiper kwa heshima yake.

Other websites[hariri | hariri chanzo]