Uranus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kuhusu matumizi ya jina Zohali kwa sayari hii tazama kipengele cha "Jina"

Uranus, bangili na miezi yake

Uranus ni sayari ya saba kutoka jua letu.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Ni sayari kubwa ya tatu ya mfumo wa jua hata kama mada yake ni hasa gesi iliyoganda. Jumla ya masi yake ni mara 14 ya dunia hivyo ni sayari nyepesi kulingana na ukubwa wake.

Ina miezi 27. Miezi mikubwa huitwa Miranda, Ariel, Umbriel, Titania na Oberon.

Uranus inaonekana kama nyota hafifu sana yenye mwangaza wa mag 5.6-6. Kutokana na kuwa hafifu vile na mwendo wake wa pole hakuna utamaduni wowote wa kale ulioitambua kuwa sayari. Ilitambuliwa mara ya kwanza kuwa sayari na tarehe 13 Machi 1781 na William Herschel.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Waswahili wa kale hawakujua sayari hii. Uranus ni jina la kimataifa lililoteuliwa katika karne ya 19 baada ya majadiliano marefu kati ya wanaastronomia wa Ulaya. Ni jina la mungu wa Ugiriki ya Kale Urano (Οὐρανός) aliyeaminiwa kuwa mungu wa anga. Lugha nyingi duniani zimepokea jina hili kwa sababu astronomia ya zamani haikujua sayari hii.

Vitabu kadhaa vinatumia jina la Kiswahili Zohali[1] [2] [3] kwa kufuata kamusi ya KAST; lakini hili ni jina la Kiswahili kwa sayari ya sita (Zohali - ing. "Saturn").[4]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Wallah, W.B. & Mwamburi, J. Kiswahili mufti darasa la 8: Mwongozo wa mwalimu. Longhorn, 2009. ISBN 99966491066
  2. TESSA - Teacher Education in Sub Saharan Africa. Nishati na Mwendo: Kutoka Ardhini kenda kwenye nyota – kutumia Zana Kifani. Available at: www.tessafrica.net
  3. Waweru, M.; Makombo, H; Vonuoli, A.; Kashihiri, C.; Mwayani, J.Hutua za Kiswahili: Masomo ya Msingi 8. East African Educational Publishers ltd., 1ed, 290p., 2005. ISBN 9966-25-403-X
  4. KAST ni kamusi ya pekee inayotumia "Zohali" kwa sayari hii. Kamusi za KKK/ESD ya TUKI na M-J SES zinaonyesha "Zohali" kwa sayari ya sita na "Uranus" kwa sayari hii. Linganisha ukurasa wa Majadiliano:Sayari
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uranus kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano