Afeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
1. Sayari kwenye afeli yake 2. Sayari kwenye periheli yake 3. Jua

Afeli (ing. aphelion) ni mahali katika obiti ya sayari au magimba mengine ya angani ambako ni mbali zaidi na jua. Jina latokana na kigiriki από na Ήλιο apo (mbali) na "helio" (jua).

Kinyume chake ni periheli inayomaanisha sehemu ya obiti iliyo karibu kabisa na jua.

Majina haya hutumiwa kama obiti ina umbo la duaradufu, yasingekuwa na maana kama obiti ingekuwa duara kamili lakini hii haitokei hali halisi.