Nenda kwa yaliyomo

Majira ya baridi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tallinn, mji mkuu wa Estonia, ulivyofunikwa na theluji tarehe 1 Januari 2010.
Theluji kaskazini mwa dunia: Kuusamo, Ufini.
Theluji kusini mwa dunia: Tierra del Fuego, Argentina.

Majira ya baridi (pia: kipupwe; kwa Kiingereza Winter) ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kuliko majira mengine. Ni kinyume cha majira ya joto au chaka.

Pengine baridi inakuwa kali sana na kuendana na barafuto: ndiyo maana maeneo mengine ya dunia hayana wakazi wa kudumu, hasa bara la Antaktiki.

Yanafuata majira ya kupuputika majani (kwa Kiingereza Fall au Autumn) na kutangulia majira ya kuchipua (kwa Kiingereza Spring).

Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.

Majira hayo tofauti hupatikana zaidi katika ukanda wa tropiki.

Wanyama, mimea, binadamu na majira ya baridi[hariri | hariri chanzo]

Ili kuhimili ukali wa majira ya baridi, wanyama wengi wana njia mbalimbali za kimaumbile na kitabia.

  • Uhamaji ni mbinu mojawapo inayotumiwa hasa na ndege wakati wa baridi. Hata hivyo, ndege wengi hawahami. Baadhi ya vipepeo pia huhama msimu huu.
  • Wanyama wengine hulala ili kupunguza shughuli metaboli mwilini wakati wa majira ya baridi. Wanyama hao, kama vile vyura, nyoka, na popo huamka msimu huu unapomalizika.
  • Wanyama wengine huhifadhi chakula watakachokula wakati wa majira ya baridi.
  • Wanyama wengine wenye manyoya hukuza manyoya yao kama wakati wa baridi; hii inaboresha uwezo wa manyoya kuhifadhi joto.
  • Msimu huu huathiri pia tabia za wanyama. Kwa mfano panya kawaida huishi chini ya theluji.
  • Baadhi ya mimea ya kila mwaka haiwezi kuishi wakati wa baridi. Hata hivyo, mimea mingine ya kila mwaka inahitaji baridi kukamilisha mzunguko wa maisha yao. Baadhi ya mimea ya msimu hufaidika kwa kufunikwa na theluji wakati mimea mikubwa huacha sehemu ya juu kulala huku mizizi yake ikihifadhiwa na theluji.

Binadamu nao hufanya mambo mbalimbali ili kuweza kukabiliana na majira ya baridi.

  • Baadhi ya nyumba za majira ya joto, ambazo zilijengwa kwa ajili ya matumizi ya majira ya joto tu zinahitaji kutunzwa wakati wa majira ya baridi. Wakati wa msimu huu nyumba hizo hutunzwa kwa kufungwa, kuzima maji, umeme, na mistari ya simu, na kulinda vipengele mbalimbali kutokana na theluji kubwa.

Kwa mfano katika eneo la New England, nchini Marekani, familia nyingi tajiri zilizoishi humo wakati wa karne ya 19 zilikuwa na nyumba za majira ya joto milimani ili kuondoka mwanzoni mwa magonjwa kwa homa ya njano na magonjwa mengine ambayo mara nyingi yalijitokeza katika miezi ya majira ya joto.

  • Mabwawa ya samaki yanahitaji hatua kadhaa za ziada ili kuhakikisha kuwa samaki wanaishi vyema wakati wa baridi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Rosenthal, Norman E. (1998). Winter Blues. New York: The Guilford Press. ISBN 1-57230-395-6

Viungovyanje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Majira ya baridi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.