Kujizungusha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mhimili wa Dunia)
Dunia inajizungusha, na pia inazunguka Jua

Kujizungusha ni tendo la gimba kuenda mwendo wa kufanya duara kwenye mhimili wake mwenyewe.[1] Mwendo wa kufanya duara kwenye mhimili ulioko nje ya kiolwa huitwa mzunguko.

Mhimili wa kujizungusha[hariri | hariri chanzo]

Mstari nyekundu ni mhimili wa kujizungusha

Mhimili wa kujizungusha ni mstari mnyoofu wa kudhaniwa ambako gimba linajizungusha. Katika mfano wa gurudumu mhimili wa kujizungusha ni sawa na ekseli.

Kwa magimba ya angani kama Dunia mhimili wa kujizungusha ni mstari wa kudhaniwa unaopita kwenye ncha mbili za kaskazini na kusini ukipita kitovu cha masi yake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia. TUKI. 1990. uk. 178. ISBN 9976 911 09 2. 
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kujizungusha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.