Nenda kwa yaliyomo

Eris

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Eris na mwezi wake

Eris (alama: ⯰;[1] pia (136199) Eris au 136199 Eris) ni sayari kibete kubwa inayojulikana katika mfumo wa Jua letu.

Picha inaonyesha mwendo wa Eris kwenye picha zilizopigwa kwa darubini ya anga ya Mt. Palomar. Eris ni ile nukta ndogo inayochezacheza upande wa kushoto juu ya mstari wa katikati ya picha. Mwendo unaoonekana ni mabadiliko ya mahali pa Eris angani katika muda wa masaa matatu. Nukta nyingine ni nyota tu zinazokaa mahali pamoja.

Tabia ze Eris

Njia yake ya kuzunguka jua ni nje ya njia ya Pluto. Eros inaonekana ina angalau mwezi mmoja unaoitwa Dysnomia. Makadirio ya kipenyo chake ni 2400 km ambacho ni kikubwa kidogo kuliko Pluto. Inazunguka jua katika muda wa miaka 556.7 ya dunia. Umbali wake na jua ni mara 97 umbali wa dunia yetu. Kutoka Eris hata jua letu laonekana kama nyota ndogo tu.

Kutambuliwa kwa Eris

Eris ilitambuliwa 2005 na wanaastronomia walioongozwa na Dr. Michael E. Brown kwenye paoneaanga Mount Palomar (Marekani). Walichungulia picha za anga zilizopigwa mwaka 2003 wakatambua nukta ya anga lililobadilika mahali.

Eris ni chanzo cha utaratibu wa "Sayari Kibete"

Kutambuliwa kwa Eris kulisababisha wanafalaki kuanzisha kitengo kipya cha "sayari kibete". Brown aliwahi kutangaza Eris kuwa sayari ya kumi ya jua letu. Lakini wataalamu wengine waliona uwezekano mkubwa ya kwamba magimba mengine ya kufanana na Eris yatapatikana karibuni. Maana ya neno "sayari" kwa kulingana na sayari za ndani ilihofiwa kutavurugika. Hivyo utaratibu wa sayari kibete ulianzishwa.

Hivyo Eris ilikuwa sababu ya kushushwa kwa cheo cha Pluto ambayo ni ndogo kuliko Eris.


Viungo vya Nje

Habari magazetini

  1. JPL/NASA (2015-04-22). "What is a Dwarf Planet?". Jet Propulsion Laboratory. Iliwekwa mnamo 2022-01-19.