Sayari kibete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Pluto inayozungukwa na mwezi wake Charon ilitazamiwa kuwa sayari ya tisa katika mfumo wa jua lakini 2006 imeshuhswa kuwa sayari kibete.

Sayari kibete (ing. dwarf planet) ni gimba la angani katika mfumo wa jua letu. Sayari kibete ni kitengo kipya katika mafundisho ya astronomia. Kilianzishwa mwaka 2006 baada ya kugundua magimba mbalimbali yanayozunguka jua letu ambayo ni makubwa kuliko asteoridi zilizojulikana hadi wakati ule lakini hazifai kuitwa "sayari" kamili. Azimio lilifanywa kwenye mkutano wa mwaka 2006 wa Umoja wa kimataifa wa wanaastronomia.

Sababu ya kuanzisha utaratibu mpya wa sayari kibete ilikuwa kutambuliwa kwa Eris mwaka 2005. Wataalamu walio wengi hawakuwa tayari kuikubali kama sayari ya kumi. Maana inaonekana ni kubwa kidogo kuliko Pluto kitengo kipya kilianzishwa.

Ufafanuzi wa sayari kibete[hariri | hariri chanzo]

Kufuatana na azimio la Umoja wa kimataifa wa wanaastronomia

sayari kibete ni gimba linalozunguka jua lenye ukubwa wa kutosha kujifanya umbo la tufe kwa njia ya graviti yake yenyewe lakini haikusafisha magimba mengine kutoka njia yake.

Tabia za Sayari kibete[hariri | hariri chanzo]

Tabia za sayari kibete ni hizi nne:

  • 1 ni gimba linalozunguka jua letu
  • 2 ukubwa wake unasababisha graviti ya kutosha ili kulazimisha mada yake kuchukua umbo kama mpira
  • 3 ukubwa wake haukutosha kufyeka mazingira ya njia yake ya kuzunguka jua kwa kuvuta kwake magimba madogo mengine
  • 4 si gimba linalozunguka sayari nyingine (=yaani si mwezi wa sayari)

Tabia za 1) na 2) ni sawa na sayari. Tabia kuu ya kufanana na sayari ni umbo la tufe. Umbo hili latokana na graviti ya gimba lenyewe kama masi yake au ukubwa wake unatosha kujifinyanga masi hii katika umbo la tufe. kama masi ni ndogo zaidi graviti ya gimba haitoshi kufikia umbo la tufe.

Tofauti muhimu ni tabia no. 3: Sayari kamili zina ukubwa na uvutano wa kutosha wa kuvuta magimba mengine madogo kwao; yaani katika njia ya dunia yetu au sayari nyingine hakuna vitu vidogo tena vinavyozunguka hapa pamoja na sayari. Yote yameshaanguka chini duniani kutokana na uvutano. Magimba yaliyobaki ni yale amabayo yanazunguka kama mwezi au kama bangili ya Zohari ambayo yana mwendo imara.

Tofauti nyingine muhimu ni no. 4: kuna magimba makubwa kushinda Pluto inayolingana na masharti ya 1-3 lakini huzunguka sayari za Mshtarii na Zohari kwa sababu ni miezi. Kwa mfano Ceres ni mwezi wa Zohari ina kipenyo cha 5,150 km. Io ina kipenyo cha 5,200 karibu sawa na Utaridi lakini ni mwezi wa Mshtarii haifai kuitwa sayari wala sayari kibete.

Orodha ya sayari kibete[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa kuna magimba 5 yanayotambuliwa kama sayari kibete katika mfumo wa jua letu:

Pluto iliyokuwa ilitajwa kama sayari ya jua letu tangu kutambuliwa mara ya kwanza mwaka 1930 lakini mwaka 2006 ilihamishwa kati ya sayari kibete.

Kuna ujwezekano wa kuwepo kwa sayari kibete nyingine katika mfumo wa jua lakini hadi sasa hakuna data za kutosha zinazoruhusu azimio kama gimba kubwa kina tabia zote za ufafanuzi wa sayari kibete.

Kuna uwezekano ya kwamba 4 Vesta, 2 Pallas na 10 Hygiea katika ukanda wa asteroidi zinaweza kutambuliwa siku moja kuwa sayari kibete.

Vilevile magimba kadhaa katika eneo nje ya obiti ya Neptuni kama vile Orcus, Quaoar, Sedna au Varuna yanatazamiwa kama wagombea kwa cheo cha sayari kibete.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sayari kibete kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.