Zuhura

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Zuhura ikionekana kama nyota ya kwanza wakati wa jioni kando ya mwezi.

Zuhura (pia: Ng'andu; kwa Kiingereza Venus) ni sayari ya pili katika mfumo wa jua na sayari zake. Kati ya sayari zote za jua ndiyo inayofanana zaidi na dunia yetu.

Jina la sayari[hariri | hariri chanzo]

Sayari hii ina majina mawili kwa Kiswahili: Zuhura, kwa matamshi mengine pia "Zuhra", ni jina leye asili ya Kiarabu زُّهَرَة zuhara lenye maana asilia ya "mwenye kung'aa".

Ng'andu ni jina lenye asili ya Kibantu.

Tabia za sayari[hariri | hariri chanzo]

Kwenye anga la usiku inang'aa kushinda nyota zote isipokuwa mwezi. Kutokana na nguvu ya mwanga wake inaonekana mapema kati ya nyota za kwanza zinazoonekana jioni; vilevile huwa inaonekana kama nyota ya mwisho wakati wa pambazuko.

Zuhura ina umbali wa kati ya kilomita milioni 107.5-108.9 kutoka jua. Umbali kutoka dunia yetu hutegemea na mahali pa dunia na Zuhura kwenye mizingo yao ya kuzunguka jua: uko kati ya kilomita milioni 38.3-260.9.

Ukubwa wake na pia kemia yake zinafanana sana na dunia ikiwa kipenyo chake ni km 12,103.6 kwenye ikweta.

Haina mwezi wowote.

Mwaka wa Zuhura (ambao ni muda wa kutimiza obiti moja wa kuzunguka dunia) una siku 224.7 za kidunia.

Siku ya Zuhura (ambayo ni muda wa dura moja ya sayari yenyewe) ina siku 243 za kidunia.

Zuhura ni sayari yenye mzunguko kufuatana na mwendo wa saa.

Hali ya hewa ni ya joto sana, kwa wastani sentigredi 500. Hewa yake ni hasa ya kabonidaioksaidi inayosababisha mawingu mengi yanayozuia sura yake isionekane kwa darubini. Kutokana na halijoto kali hakuna maji.

Utafiti[hariri | hariri chanzo]

Warusi na Wamarekani walifaulu kupeleka vyombo vya angani mbalimbali hadi Zuhura, vingine vilipita na kupima hewa, vingine vilifika kwenye sura ya sayari na kutuma picha za mazingira hadi kuharibika kutokana na joto kali.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zuhura kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.