Kizio astronomia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mstari wa kijivu hudokeza umbali wa Dunia - Jua, ambao wastani wake ni takriban km milioni 150 umefafanuliwa kuwa kizio astronomia kimoja.

Kizio astronomia (ing. astronomical unit, kifupi "au"[1]) ni kipimo cha umbali katika elimuanga. Kinalingana na umbali wa wastani kati ya dunia na jua.

Urefu wake ni mita 149,597,870,691[2] au kwa kifupi takriban kilomita milioni 150. Umbali huu ni sawa na wastani wa umbali kutoka kitovu cha Dunia hadi kitovu cha Jua.

Vipimo vilivyo kawaida duniani kama kilomita vinaweza kutumiwa katika astronomia lakini vinaleta namba kubwa mno. Hivyo astronomia imebuni vipimo vyake vinavyorahisisha kutaja umbali wa magimba katika anga-nje. Mara nyingi astronomia hutumia kipimo cha mwakanuru kwa kupima umbali katika ulimwengu. Lakini kwa umbali za karibu zaidi jinsi ilivyo ndani ya mfumo wa Jua letu kizio astronomia kimechaguliwa.

63,241.077 vizio astronomia vinafanya mwakanuru 1.

Jina la sayari / gimba Umbali hadi jua
kwa vizio astronomia
Utaridi (Mercury) 0.39
Zuhura (Venus) 0.72
Dunia 1
Mirihi (Mars) 1.52
Mshtarii (Jupiter) 5.2
Zohari (Saturn) 9.58
Uranus 19.23
Neptuni 30
Ukanda wa Kuiper kuanzia 30
Pluto 39

Chombo cha angani kilichofika mbali hadi sasa ni "Voyager 1". Mwaka 2019 kilipita vizio astronomia 145 kutoka Jua, nje ya obiti ya Pluto na ukanda wa Kuiper.

Tanbihi

  1. Resolution B2 on the re-definition of the astronomical unit of length, mkutano mkuu wa UKIA 2012
  2. Resolution B2 on the re-definition of the astronomical unit of length, mkutano mkuu wa UKIA 2012

Viungo vya Nje