Majadiliano:Sayari

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Majina ya sayari za jua letu[hariri chanzo]

Kuhusu majina ya sayari kuna matatizo ya kuwa ni majina tofautitofauti zinazopatikana katika vitabu mbalimbali. waswahili wa kale walikuwa na elimu kubwa ya nyota wakiitumia kama mabaharia waliotegemea nyota kukuta njia yao baharini wakati wa usiku, pia kwa kupiga falaki (kutabiri nyota za mtu). Elimu hii hii pamoja na majina waliyotumia haikuingia katika kamusi za kwanza. Kamusi karibu zote hazina majina ya sayari zote, wala majina ya nyota na kundinyota zilizojulikana. Zamani hii ilikuwa elimu ya mabingwa zu. Lakini siku hizi habari za anga na vyomboanga zinafika mara kwa mara kwa watu wengi kupitia media na intaneti. Basi urithi wa utamaduni usipotee!

Jedwali hapo chini inaorodhesha majina niliyokuta. Inaonekana kuna mchanganyiko uliotokea juzi na matokeo yake yanaonekana hadi vitabu vya shule na sasa (2017) hata sasa katika kamusi mpya ya "Kiswahili kwa Karne ya 21".

Marejeo yamepangwa katika mfuatano wa ki-umri baada ya nguzo ya kwanza inayoonyesha majina jinsi yalivyo katika makala hii. Tangu toleo la nne (2019) Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI inaonyesha majina ya sayari kufuatana na mapokeo ya Kiswahili, wakati mwingine kwa kuongeza majina mengine kama visawe (vsw.). Matoleo ya awali hayakuwa na majina kwa sayari zote na kuonyeha majina yasiyo sahihi.

Makala hii Sacleux M-J SES [1] Jina la Kiarabu Jan Knappert 1993 + 1971 [2] Sebald [3] TUKI Kamusi ya
Kiswahili Sanifu4 (2019)[4]
TUKI KAST Tessafrica
Teaching materials [5]
Kamusi online
Utaridi -- -- [6] عطارد 'uTArid Utaridi Zebaki Utaridi, vsw. (Zebaki) Zebaki Zebaki Zebaki
Zuhura (Ng'andu) Zuhura, Nandu, Kiongozi cha mwezi Zuhura, Ng'anda زهرة zuhura Zuhura, Ng'andu, ua la mahaba Zuhura Zuhura, vsw. Ng'andu, Nandu Zuhura, Ng'andu Zuhura Zuhura, Ng'andu
Dunia (Ardhi) Dunia, ulimwengu Dunia, ulimwengu أرض arDH -- Dunia Dunia, vsw. Ulimwengu, Ardhi Dunia Dunia Dunia
Mirihi -- - [7] مريخ mrIkh Murihi Mars Mirihi Mirihi Mirihi --
Mshtarii Mashtira Mshtarii مشتري mshtarI Mshiteri, Mshatira Mshtarii Mshtarii, vsw. Mushtara, Jupita Sumbula Sumbula Mshtarii, Sumbula
Zohali Zohali Zahali زحل zahal Zohali Zohali Zohali vsw. Satuni Sarateni Sarateni Zohali, Zohari
Uranus -- -- أورانوس urAnUs -- Uranus Uranusi Zohali Zohari --
Neptun -- -- نبتون nibtUn -- Neptun Neptuni Kausi Kausi --
Pluto -- -- بلوتو blUtU -- Pluto -- Utaridi Utaridi Pluto
  1. Johnson, A Standard English Swahili Dictionary (ilikusanya msamiati katika miaka ya 1930-1939)
  2. Swahili Islamic Poetry: Introduction, The celebration of Mohammed's birthday, Swahili Islamic cosmology, pp 95f
    hasa hapo "The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations", katika jarida la The Indian Ocean Review, 6-1993, uk 5-7
  3. P. Oswald Sebald, Maajabu ya ulimwengu (Benedictine Publications Ndanda 1985); kitabu cha pekee ninachojua kinachojadili habari za nyota na sayari kwa Kiswahili nje ya milango mifupi kwenye vitabu vya shule ya msingi
  4. Kamusi ya Kiswahili Sanifu4 (TUKI, University of Dar es Salaam); Dar es Salaam 2019; ISBN 978 019 574616 7
  5. "Kutoka Ardhini kenda kwenye nyota" Misaada ya mwalimu iliyoandaliwa na Tessafrica - kama mfano wa lugha iliyo kawaida katika vitabu vya shule ya msingi TZ
  6. "sayari moja karibu na jua"
  7. "jina la sayari mojawapo"

Kufuatana na orodha hii ni wazi ya kwamba

  • Majina ya sayari zinazoonekana kwa macho yalijulikana kwa Waswahili tangu muda mrefu, na majina yana asili ya Kiaarabu.
  • Isipokuwa sayari ya pili (inayoonekana sana angani) ina pia jina lenye mzizi wa Kibantu "Ng'andu" (kung'aa)
  • Waswahili wa kale hawakuwa na majina kwa ajili ya sayari zisizoonekana kwa macho; hizi zilijulikana tu tangu kupatikana kwa mitambo ya darubini: Uranus (1781), Neptun (1846) na Pluto (1930) pamoja na sayari kibete nyingine. Hata Waarabu wenyewe hawana majina asilia wanatumia majina ya kimataifa yenye asili ya Kigiriki.
  • Kuhusu sayari ya kwanza jedwali inaonyesha ya kwamba hapa "Zebaki" kama tafsiri ya Kiingereza "Mercury" iliingizwa katika msamiati ingawa jina asilia "Utaridi" lipo. Jan Knappert aliyekusanya majina ya nyota na sayari anataja pia "Utaridi".
  • Kuhusu dunia au ardhi yetu napendekeza kutumia hasa "dunia" pamoja na ardhi. Neno "ulimwengu" tuache kwa jumla ya yote (cosmos, world, universe)
  • Tatizo linaanza kwenye sayari ya tano Mshtarii ambayo ni jina zuri la Kiswahili. Hapo ni KAST inayoingiza "Sumbula" .Lakini kufuatana na Knappert "Sumbula" ni jina la nyota ya "a Virginis" au "Spica", si sayari.
  • Kwa sayari ya sita kuna maumbo ya karibu ya jina Zohali - Zahali - Zohari tena hapa ni KAST inayoingiza "Sarateni" - kwa Kiarabu inamaanisha "kaa", pia ugonjwa wa kansa; kufuatana na Knappert hili ni jina la kundinyota ya "Cancer"; hapa ugonjwa na matamshi ya Kiing."Saturn" zimechanganyikiwa.
  • Kuhusu sayari "mpya" ambazo hazikujulikana kwa tamaduni za kale pamoja na utamaduni wa Waswahili kuna mchanganyiko mkubwa upande wa KAST na hao wanaoifuata.
    • Uranus inapewa jina la Zohali na Pluto jina la Utaridi. Hili ni kosa ambalo ni wazi. Ninahisi ya kwamba mtu alitumia orodha ya majina ya sayari bila utafiti wa etimolojia na kuyapakiza yale yaliyobaki juu ya sayari zilizokuwa na majina "ya kigeni". "Zohali" na "Utaridi" yote ni majina ya Kiswahili yenye asili ya Kiarabu yanayoeleweka kabisa. Hakuna njia kuyatumia kwa sayari ambazo hazikujulikana kwa Waarabu wenyewe wakati Kiswahili kilitokea.
    • Kwa Neptuni KAST inaingiza jina la "kausi". Lakini Kausi ni jina la Kiswahili kwa kundinyota ya "Sagittarius".

Kwa jumla naona tufuate utaratibu ufuatao:

  • A) Tutumie kwa majina ya sayari 6 za wanza makala yale ya kale yenye asili ya Kiarabu na tuheshimu utamaduni wa Waswahili. Tunonyeshe pia majina mengine yanayotumiwa, hii ni muhimu hasa kwa Utaridi - Zebaki.
  • B) Kwa sayari za nje tutumie majina yenye asili ya Kigiriki.
  • C) kwa jumla tuweke vielekezo, lakini tuonyeshe pia onyo kuhusu maumbo yaliyoingizwa katika vitabu vya shule vilivyofuata orodha ya KAST. (nimesahihisha mwaka 2017) Kipala (majadiliano) 20:32, 16 Mei 2017 (UTC)[jibu]
Miaka 5 baada ya utafiti huo, kamusi zinazidi kutolewa. Humo jina Kausi linazidi kutumika, yale makosa ya KAST hayafuatwi (kwa mfano Sarteni haihusishwi tena na Saturn bali na Uranus), isipokuwa Mercury inazidi kuitwa Zebaki. Napendekeza walau tuanze kutumia "Kausi". --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:02, 11 Desemba 2016 (UTC)[jibu]
Asante kwa kuuliza tena (samahani nikichelewa kuiona), umenihamasisha kuchungulia upya sasa nimepata msingi wa majina yale. Kausi inatokana na Kiarabu القوس al-qaus inamaanisha upinde yaani zodiaki inayoitwa kwa Kiingereza en:Sagittarius. Kausi ni jina la "buruji ya falaki" (kwa lugha ya Waswahili asilia wenyewe) yaani kundinyota za zodiaki inayoitwa "sagittarius" kwa Kilatini/Kiingereza. Kwa hiyo ni jina linalojulikana kabisa katika utamaduni wa Waswahili lakini si kwa sayari (ambayo haiwezekani kwa Neptuni). Kama watu wameitumia kwa sayari ya Neptuni ni kosa. Narejea J Knappert, fungu "In East Africa", makala AL-NUDJUM katika THE ENCYCLOPAEDIA OF ISLAM, LEIDEN BRILL 1997, VOLUME VIII NED — SAM, uk 105 nukuu hapo:
"Swahili astrologers concentrate first and foremost on the signs of the Zodiac, Buruji za Falaki, whose names are all from Arabic: Hamali, Aries - Mizani, Libra - Thauri, Taurus - Akarabu, Scorpio - Jauza, Gemini - Kausi, Sagittarius - Saratani, Cancer - Jadi, Capricornis - Asadi, Leo - Dalu, Aquarius - Sumbula, Virgo - Hutu, Pisces
... The Swahili names of the Planets are: Mercury, Utaridi; Venus, Zuhura; Mars, Mirihi; Jupiter, Mushitari; and Saturn, Zohali."
Naona kitabu cha rejeleo kuu ni J. Knappert (yeye yule), List of names for stars and constellations, in Swahili, xxxv/1 (Dar es Salaam, March 1965) . Basi nitajaribu kuipata. Sasa naelewa jinsi gani sehemu ya orodha ya sayari zimepata majina kama Kausi, Sumbula au Saratani: zimetungwa na watu ambao ama walisikia au kusoma majina ya zodiaki na kuyatumia majina ya kundinyota kwa sayari ili wakamilishe orodha - bila kutambua wanachochanganya. Kipala (majadiliano) 17:35, 14 Februari 2017 (UTC)[jibu]
Kuhusu Kausi na Kamusi - naweza kuangalia Kamusi Kuu ya Kiswahili kwa simu - hata hapa ni wazi si sayari mbali ile buruji ya falaki ikisema "Kausi - aina ya nyota ambayo hutumiwa na waganga wa kienyeji kupigia ramli, bao" Kipala (majadiliano) 18:30, 14 Februari 2017 (UTC)[jibu]
Ndugu, hongera kwa utafiti mkubwa wenye mafanikio. Ingefaa tuwashirikishe watu wa kamusi mbalimbali, hasa KKK. Ndani yake na ndani ya KK21 (nadhani hata katika KKS - toleo la 3) Kausi kwa maana ya Neptune inatajwa mwishoni, katika nyongeza kuhusu jua na mfumo wake. Mimi sina shida zaidi ukibadilisha tena. Lakini majina hayo mapya yasiyo sahihi yameanza kuzoelekeza kupitia hizo kamusi na vitabu vya shule. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:50, 15 Februari 2017 (UTC)[jibu]
Ndugu yangu natumaini karibuni tutapata nafasi ya kuonana ana kwa ana wakati utakaporudi. Niambie nitakuja siku yoyote wakati niko bado Dar. Hapa nimepata mawasiliano ya karibu na watu walioanzisha sasa na kuiandikisha mwezi wa Mei ASSAT (Astronomy and Space Science Association of Tanzania). Wanatumia ushauri wa mzee aliyestaafu katika BAKITA. Anakubali kabisa majina ya sayari za kwanza ninayotumia pamoja na Utaridi. anathebitisha pia kuwa Dr Jan Knappert alikuwa mtafiti muhimu wa utamaduni wa Waswahili, alimjua. Tangu nimepata matokeo ya kazi yake kuhusu majina ya nyota na sayari sina wasiwasi tena. Sasa ASSAT wameamua kupeleka taarifa kuhusu matatizo ya istilahi za astronomia kwa BAKITA na Taasisi ya Elimu (wanaosimamia vitabu vya shule wakitingisishwa na kashfa iliyojadiliwa bungeni kuwa vitabu vingi vya shule vina makosa). Ninajitahidi kupata sasa pia mawasiiano na TATAKI maana hii kamusi ya Karne ya 21 ina makosa mazito kuhusu sayari (hasahasa uk. 614 penye picha na maelezo yasiyo kweli kuhusu Pluto inayoitwa "Utaridi") Kipala (majadiliano) 17:56, 18 Mei 2017 (UTC)[jibu]

Ndani na nje?[hariri chanzo]

Ebu! Jina "sayari za nje" limetumika humo namna mbili tofauti: zile za mbali ndani ya mfumo wa jua na zile za nje yake. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:21, 8 Mei 2016 (UTC)[jibu]
Asante kwa kunidokeza. Tufanyeje? "Sayari za nje" kwa exoplanets tu? Kiingereza wanaweza kucheza kwa "outer planets" na "exoplanets", ambayo kietomolojia ni maana yaleyale lakini maneno tofauti yanayolenga sasa mamo tofauti. Hapu juu sijatumia maneno kwa umakini maana tukitofautisha "inner and outer planets" hata Mshtarii na Zohali ni "za nje". Naona si lazima kutumia ndani au nje kwenye mfumo wa jua,tunaweza kuongea pia kuhusu sayari za mwamba zilizopo karibu na jua na sayari za gesi zilizopo mbali na jua. Unonaje?Kipala (majadiliano) 11:04, 8 Mei 2016 (UTC)[jibu]
Napendekeza: za jirani, za mbali na za nje. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:32, 8 Mei 2016 (UTC)[jibu]
Namuunga mkono Ndugu Riccardo. --Baba Tabita (majadiliano) 16:30, 8 Mei 2016 (UTC)[jibu]