Majadiliano ya mtumiaji:Kipala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Tazama pia kurasa za muda: Viungo vya mwili na makala 100!

Salamu bwana kipala nipe mwongozo kwenye ukurasa wa kuazisha makala mpya kuepukana na makosa yanayojitokeza humu (wiki) najua umenizuia bila kujua mimi nimekosea wapi,naomba mrejesho mpya mimi si mtu mbaya kuleta fujo.

Mimi Sharkgates!

Habari za leo Kipala?

Nashukuru kwa ujumbe wako ulionitumia lakini sielewi unamaanisha nini unaposema nimetumia lugha ya Kompyuta.

Mimi ni Mtanzania na Kiswahili ni lugha yangu ya kwanza. Siwezi kuandika jambo lisiloeleweka.

Naijua vizuri lugha yangu. Tafadhali nionyeshe palipo na kasoro katika makala ya Uzalendo niliyoandika.

Asante -- Sharkgates (majadiliano)

Ndugu asante kwa ujumbe. Ulitumia zana ya ContentTranslation iliyoandaliwa na WMF. Nilifanya pia majaribio ya kutunga makala. Kama ni tafsiri ya matini ya Kiingereza yenye sentensi sahili matokeo yake yanaweza kuwa chanzo kinachofaa. Kadri waandishi wa matini ya Kiingereza walitumia sentensi ngumu zaidi matokeo hayafai tena. Upande mwingine ni saikolojia yetu tunaotumia zana hili: napata matini ndefu kiasi ninayotazama kwenye kompyuta yangu, naona hapa na pale istilahi ambazo ni kosa na kuzisahihisha, lakini naweza kusahau kuangalia upya sentensi yote na kifungu chote. Zana hizi zinatuongoza kutafsiri neno-kwa-neno hata kama muundo wa sentensi na dhana ni tofauti katika lugha na utamaduni.
Tatizo hili lilitokea kwangu, ninaliona kwa wachangiaji wengine naona pia ktk uzalendo. Ulifaulu kuondoa istilahi nyingi zisizofaa (hapa hongera, tuna bado mabaya mengi katika makala nyingine zilizofika kwa kutumia google translate.. lkn hata kwako vitu kama "ufuasi wa taifa dini" vilipita) lakini sehemu za sentensi zako hazieleweki kirahisi ni ngumu bila kutaja habari ngumu.
Nukuu: "Neno la kiingereza wazalendo lilirasimishwa kwa mara ya kwanza katika Zama za Elizabeth..." - hakuna neno "wazalendo" ktk lugha ya Kiingereza
Nukuu: "Kwa ujumla dhana ya uraia wema na kujitolea kwa kundi la watu imerasimishwa duniani kote katika kipindi cha kihistoria." Kwangu haieleweki kabisa, nikaelewa baada ya kusoma Kiingereza chake. "Kipindi cha kihistoria" tofauti na vipindi gani vingine? Nikijua maana ya "historical period" kuwa tofauti na "prehistory" kwa Kiingereza napata picha, lakini ni sentensi gumu kidog hata kwa Kiingereza akieleza dhana sahili kwa njia gumu (naona alitaka kuepukana kusema kitu kuhusu kipindi ambako hatuna ushahidi). Jinsi ninavyoona wasomaji wetu wengi hawataitambua. Je, usingekubali ya kwamba sentensi kama "Watu waliojitolea kwa jumuiya walimoishi walisifiwa katika jamii zote za historia inayojulikana. Tabia hii ya kujitolea wa umma ilipanuliwa kadri watu waliendelea kuishi katika jamii kubwa zaidi kama vile miji, madola na hatimaye mataifa" inaweza kusaidia wasomaji wetu kushika dhana lilelile lililolengwa na mwandishi wa matini ya Kiingereza?

Basi namaliza hapa kwa sasa. Lkn asante kwa kutonyamaza! Na karibu sana kuchangia tena! Kipala (majadiliano) 06:56, 2 Mei 2018 (UTC)

Kumbukumbu ya Hifadhi ya Nyaraka

Majadiliano ya awali yamehamishwa kwenye kurasa za Hifadhi ya Nyaraka:

Mimi ni Millikan,Naahidi kufuata ulichonielekeza nimepata ujumbe wako.

Kiwavi

Kipala salaam. Unataka kufanya nini na ukurasa wa kiwavi? Matini uliyoyaweka hapa yanataka ukurasa wake. ChriKo (majadiliano) 09:52, 21 Januari 2017 (UTC)

Samahani ilitokea kwa kosa, niko Accra na intaneti ilikatika wakati nilipokuwa katikati kazini. Naondoa kwa sasa. Kipala (majadiliano) 10:18, 21 Januari 2017 (UTC)

Stammtische

Treffen der Wikipedianer (z.B. Stammtische) haben eine Übersichtsseite auf de:Wikipedia:Treffen der Wikipedianer. Als nächste Termine sehe ich da einen Stammtisch in Bremen am 26. Januar. Mit besten Grüßen, --Gereon K. (majadiliano) 11:36, 22 Januari 2017 (UTC)

Wir sprachen über de:Wikipedia:Bibliotheksrecherche ... --Gereon K. (majadiliano) 06:27, 25 Januari 2017 (UTC)

Barua pepe

Salaam, Umepata barua pepe yangu?--MwanaharakatiLonga 13:03, 23 Januari 2017 (UTC)

Salaam. Nitakuwepo online kutwa nzima. We tuma tu, nitakujibu! Hakuna shida, skype inafaa sana.--MwanaharakatiLonga 08:05, 25 Januari 2017 (UTC)
Hongera kwa WikiIndaba, lakini sijaelewa kwa nini umepogolea vile ukurasa wa Tarakilishi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:55, 28 Januari 2017 (UTC)
Asante kwa kuniambia, hii ilikuwa ajali, nimeisahihisha. Kipala (majadiliano) 06:09, 02 Mei 2018 (UTC)

RE:DCC Mlimani Park Orchestra

Salaam, Nitakupa muhtasari, baada ya watu kugundua kuna makala nyingi za bendi za Tanzania, ndiyo hivyo tena wanajaribu-jaribu. Lakini makala hizi zina umuhimu sana ziwepo humu kwa sababu ni za Waswahili na hii ndiyo Wikipedia yao!--MwanaharakatiLonga 06:55, 5 Februari 2017 (UTC)

Umuhimu si swali. Nauliza tu kama kulikuwa Jambo kuhusu bendi hii. Maana ghafla kufunguliwa mara 300 si kawaida. Kipala (majadiliano) 07:07, 5 Februari 2017 (UTC)
Hapakuwa na jambo! Mambo hutokea... Vipi kuhusu mradi wa Wikichanzo? Umefikia wapi?--MwanaharakatiLonga 09:22, 8 Februari 2017 (UTC)

Your feedback matters: Final reminder to take the global Wikimedia survey

(Sorry to write in English)

Translation

Hello, could you please translate Automatic refresh/Automatische Aktualisierung phrase to Kiswahili? Thanks -XQV- (majadiliano) 21:13, 1 Machi 2017 (UTC)

Kuhusu Mbute

Salaam mzee kipara natumai ni mzima wa afya. Ni sahihi kabisa ulicho ongeza kuhusu Mbute kwani kwa Tanzania kanda ya ziwa haswa hupenda chakula hichoEnock John (majadiliano) 12:28, 29 Mei 2017 (UTC)

WMCon 2017 Berlin

Ndugu, salaam. Nataka kukujulisha tu kwamba nimealikwa kuhudhuria Wikimedia Conference 2017, nami nikajisajili tayari. Sitahudhuria rasmi kwa ajili ya wikipedia yetu bali kama mwanakamati wa LangCom. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 20:55, 4 Machi 2017 (UTC)

Hata hivyo, mafanyikio mema!Kipala (majadiliano) 22:22, 4 Machi 2017 (UTC)

Ombi la MetaWiki

Salaam, Naomba munichangie msaada wa kukubali ombi langu la kupewa laptop kule Meta-Wiki. Kiungo hiki hapa. Wako,--MwanaharakatiLonga 13:14, 17 Machi 2017 (UTC)

Kuna email nilituma kati yangu mimi, Oliver na Asaf. Kama umeiona, tafadhali jibu ili tuwe wazi kwa huyo mbebaji wa ule mzigo. Pole sana. Najua hujapona jelaha la hospitali!--MwanaharakatiLonga 12:52, 24 Machi 2017 (UTC)

James Francis Mbatia

Habari? Could you please move this one to James Fransis Mbatia? According to the Parliament website, that's the proper spelling. Jon Harald Søby (majadiliano) 20:26, 30 Mei 2017 (UTC)

I guess it is not correct but rather a typo. On facebook he appears as James Francis. https://web.facebook.com/profile.php?id=100005600115588&hc_ref=SEARCH&fref=nf With Tanzanian orthographies you never know, so Francis is thinkable but not too much. I leave it as it is. As I cannot see him as Francis anywhere in the news, there is no need for redirect which we otherwise would do. Kipala (majadiliano) 22:06, 30 Mei 2017 (UTC)

Astrowiki

Kwa hali ya kazi tulipofikia angalia faili:Astrowiki_orodha_10000.pdf. Kipala (majadiliano) 14:53, 5 Juni 2017 (UTC)

Wilaya ya Kibiti

Salaam, mzee wangu. Inaonekana kama kata ya Kibiti imekuwa wilaya yenyewe, yaani siyo chini ya wilaya ya Rufiji tena. Kufuatana na tovuti rasmi, hiyo wilaya mpya ina kata kumi na sita. Ukiwa na nafasi, naomba ubadilishe kigezo cha Kata za Wilaya ya Rufiji na mabadiliko mengine yafaayo. Asante! Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 05:39, 11 Juni 2017 (UTC)

Naona umeanza kuifanyia kazi. Asante sana! --Baba Tabita (majadiliano) 18:11, 11 Juni 2017 (UTC)
Nilibahatika kupata orodha ya wakazi wa majimbo ya ucjaguzi lililotolewa na ofisi ya takwimu ya taifa - tovuti za wilaya kama mara nyingi hazikufanyaiwa kazi nje ya kuweka jina na picha ya mkuu, menginevyo kurasa zinajaa "Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur, adipisci veli....." Kipala (majadiliano) 18:17, 11 Juni 2017 (UTC)


Kurasa Za Mbele

Hali vipi, Kipala? Kuna mahali nilisoma kwamba sababu moja kuu mbona watu wengi hawatumii mtandao kwa lugha yao ya kiasili ni kwa sababu hawapati habari au hadithi zinazowafaa. Kwa mfano, Mozart, kwa sasa, yupo kwenye ukurasa wa kwanza. Mimi binafsi naipenda muziki yake, lakini itamsaidiaje mama mzee kutoka Morogoro kusoma kuhusu Mozart, badala ya kumhusu watu kama Salif Keita, ama Bi Kidude, ama Baraka Mwinshekhe? Mbona mama huyo asimwone mwanamuziki Saida Karoli kwenye landing page? Ama Daudi Kabaka? Mbona taarifa nyingi tunazopata ni za kuwahusu kina Queen Latifah? Ni ombi langu kwamba tuwe tunaweka taarifa zinazohusu Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye landing page. Shukran!

Asante kwa maoni. Nitamkumbusha MuddyB abadilishe makala hizi mara nyingi zaidi. Ni kweli ya kwamba hapa tumechelewa, maana tumeacha sasa makala hizihizi kwa miezi mingi. Sina imani kubwa ya kwamba Mama Mzee wa Morogoro atasoma sana intaneti; akisoma labda atafurahia pia kuona mambo ya kigeni. Hata hivyo nakubali kabisa inafaa daima kuwa na asilimia ya habari za Afrika ya MAshariki katika chaguo hili. Kipala (majadiliano) 07:05, 14 Julai 2017 (UTC)
Ahsante kwa majibu. Kazi kwetu basi! Luckimg2 (majadiliano) 07:53, 14 Julai 2017 (UTC)
Salaam tena wazee wangu,

Haya, pendekezeni kurasa, naimi nitaziweka. Muda sasa wa kufanya mabadiliko makubwa katika ukurasa wa mwanzo. Iajapokuwa siamini sana kama asemavyo mzee wangu kuhusu wazee kufungua intaneti hasa wa vijijini.--MwanaharakatiLonga 12:02, 14 Julai 2017 (UTC) Napendekeza tuandae orodha kwa njia hii:

  • makala 1-1 ya Afya/maradhi, historia, jiografia, Muziki, filamu, lugha/michezo, Afrika ya Mashariki, sayansi (orodha ya kurasa 8)
  • tuandae orodha hizi mfululizo, zibadilike ikiwezekana kila wiki, menginevyo angalau wiki 2

Mnanoaje? Kipala (majadiliano) 13:20, 14 Julai 2017 (UTC)

    • Sawa. Tuanze kuzijaza basi! Utaona nishaanza mbili tatu.--MwanaharakatiLonga 04:33, 15 Julai 2017 (UTC)

Asane nimeuona ujume wako naorsha sasa.

  • Ngoja niendeleze kama ulivyosema. Naomba pendekeza makala za historia, sayansi, michezo na kadhalika. Za muziki nimeweka 2 tayari..--MwanaharakatiLonga 06:44, 26 Julai 2017 (UTC)

Seduce Me

Kumbe! Ahsante! Hata hivyo, wimbo wenyewe sasa hivi huku TZ ni unasifika sana hakuna mfanowe.--MwanaharakatiLonga 03:13, 1 Septemba 2017 (UTC)

Makala za nyumbani

Salaam, Kipindi hiki nimeamua kuandika makala kuhusu masuala mbalimbali ya Tanzania. Hasa muziki, japo nimekuwa nikigusia na mengineyo kidogo kuhusu siasa, lakini mapenzi yangu hasa yapo katika muziki. Nina orodha ndefu mno na taarifa zake zipo ni jambo la kuziweka tu. Kama ulivyoona hivi karibuni nimepata kuingiza makala mengi sana. Haya, narudi polepole kama zamani. Tuombeane uzima tu.--MwanaharakatiLonga 03:33, 1 Septemba 2017 (UTC)

Majadiliano:Kupanda kwa halijoto duniani

Kipala salaam. Nakuuliza uangalie Majadiliano:Kupanda kwa halijoto duniani. Nafikiri matini haya siyo sadifu. Kwanza nilimwambia aandike kwa Kiswahili na kuchangia mawazo yake katika makala makuu. Akafuta matini yangu bila majadilliano. Halafu nikafuta matini yake nikiandika kwamba matini haya si sadifu. Sasa amerudisha matini yake, tena bila majadiliano. Nadhani kwamba tafadhali mchangiaji huyu apingwe. Hana hata akaunti. Unaonaje? ChriKo (majadiliano) 11:07, 11 Oktoba 2017 (UTC)

Michango ya mtumiaji Kwa 178.24.241.188 This IP address is currently globally blocked. The global block log entry is provided below for reference: 20:01, 7 Oktoba 2017: Tegel (meta.wikimedia.org) globally blocked 178.24.241.188 (inakwisha tarehe 21 Oktoba 2017 saa 20:01) (Cross-wiki spam) (local status)
alipakia yaleyale hata kwenye wiki nyingine. Nafuta hii kwenye ukurasa. Akirudi tumzuie hapa.Kipala (majadiliano) 12:06, 11 Oktoba 2017 (UTC)
Asante. ChriKo (majadiliano) 16:40, 11 Oktoba 2017 (UTC)

Nakala Citizen Tv

Angalia nakala yangu mpya Citizen TV na unisaidie kuisahihisha ..I invite you to correct and contribute in the article article I created.Citizen Tv Boy Addi (majadiliano) 09:53, 30 Novemba 2017 (UTC) Boy Addi (majadiliano) 09:53, 30 Novemba 2017 (UTC)

Asante, nimeweka kiungo cha interwiki, sasa unaona kiungo cha enwiki upande wa kushoto chini. Hii usisahau, maelezo unapata hapa Wikipedia:Mwongozo_(Viungo_vya_Wikipedia) (chini kwenye ukurasa). Nimehamisha pia jina kwa "Citizen TV" maana tahajia nhii ni kawaida, sivyo? Menginevyo ningeondoa orodha za vituo vya redio visivyohusika na Cititen TV na kuacha Citizen redio pekee. Mengine sina maana nasubiri habari utakazoweka, mwenyewe sina habari sana kuhusu Citizen TV, isipokuwa unaweza kuongeza zaidi kutoka enwiki. Kipala (majadiliano) 10:04, 30 Novemba 2017 (UTC)
   Usiondoe orodha za vituo vya redio.vyote viko chini ya Citizen TV ingawa katika lugha tofauti Boy Addi (majadiliano) 18:57, 30 Novemba 2017 (UTC)
Hii inapaswa kuleezwa katika matini. Kipala (majadiliano) 21:15, 30 Novemba 2017 (UTC)

Kigezo nyota

Mzee wangu salaam.
Ile kazi uliyonituma nimeikamilisha!
Naomba utazame: Majadiliano_ya_kigezo:Nyota kwa mfano zaidi.
Kilichotokea uliandika tofauti kati ya paramita za ndani na nje. Ulikuwa unachukua zile kubwa, badala ya ndogo. Ninamaanisha ili kigezo kitumike, sharti utumie yale maandishi madogo kuonesha paramita zake katika kigezo cha nje (katika makala). Mfano: "Kazi maarufu" ya nje (kazi maarufu) ya ndani ambayo ndiyo hasa inatakiwa iwekwe kwenye kigezo wakati wa kujaza taarifa!
Hadi baadaye, uwe salama mzee wangu. Ukinihitaji, just holla me up nakuja fasta tu!--MwanaharakatiLonga 05:49, 4 Desemba 2017 (UTC)

Wiki Loves Africa 2017

Hello and thank you for your message. I am trying to insert pictures from the Wiki Loves Africa contest 2017 (almost 18 000), in different languages. But unfortunately I do not understand yours.

Of course it would much be better if you, or other SW-contributors, would try to find interesting and relevant pictures to illustrate your own WP.

Best regards,

Ji-Elle (majadiliano) 11:03, 13 Desemba 2017 (UTC)

Eigentlich verstehe ich Deutsch viel besser als Swahili :-) Ji-Elle (majadiliano) 11:06, 13 Desemba 2017 (UTC)

'Oumuamua

Kipala salaam. Utaandika makala kuhusu 'Oumuamua? ChriKo (majadiliano) 07:00, 19 Desemba 2017 (UTC)

Ok, ukisema vile.. Kipala (majadiliano) 12:25, 19 Desemba 2017 (UTC)

Distributing Internet-in-a-Box in Southern Africa

We have delivered a few Internet's in a Box to Tanzania.

There is a request for more. We are wanting to put all of SW WP on the device.

Wondering if you can help with translating three sentences here Thanks?

James Heilman, MD (talk · contribs · email) 09:25, 24 Februari 2018 (UTC)

Sorry for the confusion. Needed to adjust a few things. Many thanks for your help :-) James Heilman, MD (talk · contribs · email) 09:25, 24 Februari 2018 (UTC)

Orodha ya volkeno

Ndugu, asante kwa kufafanua maana ya kisiwa cha wafu. Naomba utafsiri pia maneno ya Kijerumani katika orodha ya volkeno nchini Tanzania. Asante.

Sherehe!!!

Angalia hatua aliyoifikisha Ndugu Riccardo: Matukio ya hivi karibuni. Sherehe!!! --Baba Tabita (majadiliano) 10:01, 17 Machi 2018 (UTC)

Kupatwa kwa mwezi

Asante sana kipala nimefurahi sana kuona makala hii ikiwa imeshiba majibu ya maswali yangu. oba21.on (majadiliano) 17:20, 27 Julai 2018 (UTC)

Hongera kwa kushiba! Nafurahi kama makala hii inaweza kusaidia--Kipala (majadiliano) 18:08, 27 Julai 2018 (UTC)

Karata

Ndugu, kamusi zote nilizoangalia zinasema karata ni kutoka Kireno. Na kweli inaonekana historia ndiyo hiyo, na tahajia ka:d si rahisi kugeuka kuwa karata, tofauti na carta. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:05, 3 Agosti 2018 (UTC)

Asante, sijakuta maelezo kuwa "karata" inatoka Kireno (umeangalia kamusi zipi?). Lakini nikichungulia tena kamusi za kale za Kiswahili neno latajwa kote (Krapf, Madan). Sacleux anasema ni kutoka "lahaja za kaskazini". Kwa hiyo nakubali inawezekana neno lilifika kupitia Wareno.Kipala (majadiliano) 07:33, 3 Agosti 2018 (UTC)
Madan-Johnson, KK21, KKK. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:04, 3 Agosti 2018 (UTC)

To secrete

Kipala salaam. Je! Unajua tafsiri nzuri ya kitenzi "secrete" au "excrete"? Kamusi ya biolojia, fizikia na kemia ina "mnyeso" kwa "secretion", lakini hii inatoka kwa kitenzi gani? "Kunyesa" inamaanisha kulowa. "Kunya" inaonekana kutumika hasa kwa mavi na "kunyesha" pia (na kwa mvua). Nilidhani kwa muda kwamba "kuchoza" ilikuwa tafsiri nzuri, mpaka niligundua kuwa ina maana ya "secreting" kama kuficha kitu. ChriKo (majadiliano) 20:12, 29 Septemba 2018 (UTC)

Mnyeso inatokana na kunyesa. Angalia TUKI SED: nyes.a kt [sie] be wet, moisten. (tde) nyesea;(tdk) nyeseka; (tds) nyesesha. BTW kinyesi ni sawa na mavi. TUKI ESD excretion n.excrete vt -nya, toa takamwili Kipala (majadiliano) 20:48, 29 Septemba 2018 (UTC)
Ndiyo, hiyo yote ni kweli, lakini vitenzi hivi vyote vinahusu takataka (mavi, takamwili n.k.). Kinachotoka katika tezi si takataka. ChriKo (majadiliano) 14:32, 1 Oktoba 2018 (UTC)
Labda lete sentensi. "Kutoa" haitoshi? --Kipala (majadiliano) 14:38, 1 Oktoba 2018 (UTC)
Ndiyo, kama hakuna kitenzi bora, nitatumia "kutoa". Asante. ChriKo (majadiliano) 16:45, 1 Oktoba 2018 (UTC)

Koloni

Ndugu, sijui umatumia kamusi gani kupanga neno hilo katika ngeli i-zi. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:36, 10 Desemba 2018 (UTC)

Hali halisi nachanganyikiwa pamoja na kamusi zangu. TUKI Kiswahili-Kiingereza inanipa koloni* nm ma- [li-/ya-] colony. Lakini TUKI Kamusi ya Kiswahili Sanifu³ ina koloni nm [i-/zi-] nchi inayotawaliwa na nchi nyingine. Kipala (majadiliano) 10:51, 10 Desemba 2018 (UTC)
Inatokea. Mimi siku hizi nafuata zaidi KKK, ingawa naangalia nyingine pia. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:04, 10 Desemba 2018 (UTC)