Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Anuary Rajabu

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:30, 19 Desemba 2020 (UTC)[jibu]

Kuhusu Uhariri[hariri chanzo]

Habari ndugu Anuary Rajabu Hongera sana kwa jitihada zako za kuhariri katika Wikipedia ya Kiswahili, jaribu kupitia sana ukurasa wa mabadiliko ya karibuni ili kuweza kuona baadhi ya makala zako na namna zinavyoendelea kuboreshwa, na utumie maboresho hayo katika makala zako nyingine. Amani sana kwako. Idd ningaIdd ninga (majadiliano) 22:58, 23 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Volkeno[hariri chanzo]

Ndugu naona tunaingiliana kwenye makala kuhusu Chamko ya volkeno. Sijamaliza bado. Ushauri ni: uangalie historia ya makala; kama imehaririwa dakika chache zilizopita, kuna uwezekano mhariri bado anaendelea.. Kwa hiyo heri kusibiri hadi kesho. Kipala (majadiliano) 20:05, 25 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Ooh Sawa kiongozi nimekuelwa Samahani kwa hilo, Nitafanya hivo. Anuary Rajabu (majadiliano) 22:17, 25 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Jina la Mtu[hariri chanzo]

Salamu Anuary Rajabu Unaweza kuangalia katika makala zako zenye majina ya watu na kuona baadhi ya mabadiliko hasa ya masahihisho ya jina, kwa kawaida unapoandika jina la mtu inafaa kabisa jina liandikwe kwa herufi kubwa badala ya ndogo, unaweza kuona namna majina ya makala zako yalivyobadilishwa, hongera kwa juhudi unazofanya, endelea kujifunza zaidi, Idd ninga (majadiliano)

Nimekuzuia siku 3[hariri chanzo]

Ndugu, uliondoa vigezo vya umaarufu, vyanz na futa kutoka ukurasa wa Melody Mbassa, bila maelezo yoyote. Hapa umeingilia katika kazi ya usimamizi wa wikipedia hii. Nimekuzuia sasa kwa siku 3, huwezi kuhariri kwa siku hizo. Unaweza kujieleza kwenye ukurasa huu hapa. Ukiweza kutaja sababu zinazoeleweka naweza kuondoa kizuizi.Kipala (majadiliano) 08:41, 28 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Naomba kusamehewa,nilikua sijui kuhusu hilo lakini kwa kuwa kiongozi wangu ameweza kunielekeza kuhusu hilo, sitoweza kufanya hivo tena kwani mie sio mjuzi sana katika uhariri wa makala. Hivo nimeweza kujifunza. Anuary Rajabu (majadiliano) 09:07, 28 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Asante kwa kujibu. Nimekufungua. Ila bado hujasema kwa nini uliondoa vigezo vile? Kipala (majadiliano) 18:57, 28 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Can you help me correct an article? Thank you![hariri chanzo]

Hello, @Anuary Rajabu:! I wrote an article on Andrea Benetti, a well-known Italian artist https://en.wikipedia.org/wiki/Andrea_Benetti_(artist). I used the automatic translator to make a draft https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:BarbaraLuciano13 . Could you help me correct the text and add the infobox with the photo at the beginning and the categories at the bottom? Unfortunately I don't know the language and I am not able to do it ... Thanks for what you can do, see you soon, --BarbaraLuciano13 (majadiliano) 09:11, 19 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Marekebisho[hariri chanzo]

Salamu Anuary, tazama katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Entisar_Elsaeed kuna sehemu umeandika kuwa Entisari ni mwanaharakati wa kutetea Wanawake, lakini katika makala hii ukasema kuwa Elsaeed na taasisi yake walilenga katika kuongeza unyanyasaji wa wanawake majumbani, nafikiri kuwa ulitaka kuandika kupunguza, sasa cha kufanya pitia makala yake ni kuifanyia marekebishom, tazama katika makala ya kiingereza nini kilichoandikwa,Amani sanaIdd ninga (majadiliano) 18:34, 9 Machi 2022 (UTC)[jibu]

sawa kiongozi nimeelewa nitafanya hivyo. Anuary Rajabu (majadiliano) 12:47, 10 Machi 2022 (UTC)[jibu]

Hongera[hariri chanzo]

Anuary naona siku hizi unaleta michango mingi yenye thamani. Naona umeshika vizuri fomati ya wikipedia. Nakupa Hongera! Kipala (majadiliano) 07:59, 16 Machi 2022 (UTC)[jibu]

Asante sana. Anuary Rajabu (majadiliano) 11:34, 16 Machi 2022 (UTC)[jibu]
Pamoja na pongezi, naomba uangalie makala zenyewe: kweli tunahitaji kutetea ushoga? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:13, 29 Machi 2022 (UTC)[jibu]
Asante kwa kufanyia doria makala nyingi. Mimi nimezidiwa. Ila naomba uondoe tanbihi za Wikipedia ya Kiingereza na hasa jamii nyingi mno. Unakuta makala ya mwanamuziki wa Nigeria ina jamii:Sanaa ya Afrika! kama si Jamii:Afrika! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:14, 4 Mei 2022 (UTC)[jibu]
Asante sana, nitajitahidi kufanya hivyo. Amani iwe nasi sote. Anuary Rajabu (majadiliano) 14:31, 4 Mei 2022 (UTC)[jibu]

JAMII za Muziki Aziingiliani na michezo[hariri chanzo]

Amani kwako ndugu, kuwa makini wakati unachagua jamii ya kuweka kwenye makala,acha kuunganisha jamii ya muziki na makala za mchezo wa Mpira wa miguu. Justine Msechu (majadiliano) 19:41, 14 Mei 2022 (UTC)[jibu]

Asante kwa ukumbusho nadhani ni suala la kujisahau tu katika ukopiji wa jamii wakati wa kuchapisha makala, hivo nitazipitia makala zangu zote ili kurekebisha makosa hayo. Amani iwe nasi sote. Anuary Rajabu (majadiliano) 19:54, 14 Mei 2022 (UTC)[jibu]

Feminism and Folklore 2022 - Local prize winners[hariri chanzo]

Please help translate to your language

Congratulations for winning a local prize in Feminism and Folklore 2022 writing competition. Thank you for your contribution and documenting your local folk culture on Wikipedia. Please fill in your preferences before 15th of June 2022 to receive your prize. Requesting you to fill this form before the deadline to avoid disappointments.

Feel free to contact us if you need any assistance or further queries.

Best wishes,

FNF 2022 International Team

Stay connected  

MediaWiki message delivery (majadiliano) 07:50, 22 Mei 2022 (UTC)[jibu]

Reminder to provide information - Feminism and Folklore 2022[hariri chanzo]

Dear User

The Google form to submit information of winners during the 2022 edition of Feminism and Folklore 2022 end on 10th of June 2022. Please be informed that you will loose your prize once the deadline for sending information ends. We humbly urge you to kindly fill the form using this link as soon as possible.

Feel free to contact us on mail or talkpage if you have any difficulties.

Thank you for understanding!

Regards

International Team

Feminism and Folklore 2022

MediaWiki message delivery (majadiliano) 12:38, 5 Juni 2022 (UTC)[jibu]

Mipira ya samaki[hariri chanzo]

Salamu Anuary. Ukichangia makala unafuata mabadiliko katika makala haya na kusoma majadiliano yake? Niliweka maoni yangu na swali kwenye Majadiliano:Mipira ya samaki (angalia hapo chini). Bado ninangoja jibu lako.

Mipira wa samaki ni tafsiri isiyofaa kwa "fish balls". Maana ya mpira kwanza ni "rubber", kwa hivyo ikiwa maana yake ni "ball" hiyo ball ni aina ya rubber au labda ya plastiki. Kwa ujumla, "food ball" ni tonge kwa Kiswahili, au kitonge ikiwa ni dogo. "Meat ball" ni kababu, kwa hivyo labda tutumie hii kwa "fish ball" pia. Mnapendelea neno gani? ChriKo (majadiliano) 06:00, 22 Juni 2022 (UTC)[jibu]

Asante sana Chriko kwa ukumbusho wako mzuri, hakika kweli Mipira ya samaki sio tafsiri thabiti ya "fish ball", hivyo katika kuchangia kwangu uhariri wa makala hiyo sikuweza kupitia huo ujumbe wako ulioacha. Anuary Rajabu (majadiliano) 02:16, 23 Juni 2022 (UTC)[jibu]

Tena jamii[hariri chanzo]

Asante kwa kutekeleza masahihisho. Sasa mfano wa Alfred Dan Moussa. Umemweka kwa "Wanahabari wa Cote d'Ivoire" PIA "Watu wa Cote d'Ivoire". Hii ya pili ni bure. "Wanahabari wa Cote d'Ivoire" umeanzisha kama jamii mpya, sasa unahitaji kufungua ukurasa wake (bofya jina jekundu tu) na ndani yake unaandika (katika mabano mraba) "Watu wa Cote Cote d'Ivoire" halafu pia jamii husika ya wanahabari. Uitafute tu, utakuta jina tofauti kidogo "Jamii:Waandishi wa habari". Kipala (majadiliano) 20:52, 26 Julai 2022 (UTC)[jibu]

Ahsante sana kwa ukumbusho wako mzuri, lakini makala hii sikuianzisha mimi, hivo mie nimefanya masahihisho tu katika makala.
Pia katika suala la kuongeza, kupunguza na masahihisho ya jamii niliogopa kuingilia majukumu ndio maana niliacha kama nilivyokuta, kwani nafahamu hilo ni jukumu la mkabidhi. Anuary Rajabu (majadiliano) 05:02, 27 Julai 2022 (UTC)[jibu]

Ndugu, hongera kwa juhudi zako. Ila unapotaka kuchangia ukurasa fulani, usianze na moja. Kwa mfano huo hapo juu ulikata viungo na maandishi mazuri. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:07, 31 Julai 2022 (UTC)[jibu]

ukarasa huo ulikua hauna vyanzo na pia baadhi ya maudhui yalikua hayaendani na makala ya kiingereza, hivo ndio nilikua najaribu kuongeza vyanzo kwa kuanza kuandika upya, lakini baadhi ya vitu kama jamii na picha nimerejesha kama awali ilivyokua.
Unaweza kuupitia sasa hivi ukaona. Anuary Rajabu (majadiliano) 06:16, 31 Julai 2022 (UTC)[jibu]
Sawasawa, ila kumbuka si lazima ukurasa wa Kiswahili ufanane na ule wa Kiingereza! Kwa mfano kwa Kiswahili nadhani hatusemi sana "mtangazaji mwanamke" bali ni "mwanamke mtangazaji" au "mtangazaji wa kike". Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:52, 31 Julai 2022 (UTC)[jibu]
Ahsante sana kwa kunipatia uelewa ambao nilikua sina hapo awali, hivo nitayafanyia kazi yote haya kuhakikisha kuwa makala zinakua bora zaidi. Anuary Rajabu (majadiliano) 07:00, 31 Julai 2022 (UTC)[jibu]


Kukaribisha watumiaji wapya[hariri chanzo]

Habari nimeona umefanya kazi sana kuwakaribisha waliojiandikisha, asante sana!! Ila sasa naona umeanza kukaribisha pia URL. Sitaki kukuzuia, ukiwa nba muda mwingi endelea tu. Ila tu faida yake si kubwa sana. Maana wengi wanaingia kwa URL tofautitofauti zinazoweza kubadilika. Hapo ni sababu kwa kawaida hatuifanyi. Ila ni chaguo lako. 2003:CE:6730:1F01:2C97:DBF6:8B7:A19 12:47, 16 Agosti 2022 (UTC)[jibu]

Kumbe safari hii nilingia pia kwa URL fulani  ! Kipala (majadiliano) 12:49, 16 Agosti 2022 (UTC)[jibu]
Asante sana kwa kunikumbusha na kunielekeza hapa nimeelewa. Anuary Rajabu (majadiliano) 19:34, 16 Agosti 2022 (UTC)[jibu]

Kuongeza jamii[hariri chanzo]

Habari, naona umeongeza jamii kwenye makala zilizokosa jamii za maana (zote zilipangwa chini ya "amani" pekee, ambayo haisiaidii kitu. Ila umeweka "mbegu za watu" ambayo haisaidii vilevile (ningependa kuifuta lakini ziko nyingi mno tayari, heri tuache kuitumia). Maana kusudi la jamii ni kuainisha makala na kupanga makala ambazo mada zinafanana.

Njia bora ni kuona kama makala iko kwenye enwiki na kuchagua jamii za huko; hii inahitaji muda kidogo maana unahitaji kupeleleza kwanza kama jamii iko kwa Kiswahili, halafu utaitumia, au unaanza jamii mpya. Kwa vyote tazama Msaada:Jamii. Kipala (majadiliano) 10:42, 20 Agosti 2022 (UTC)[jibu]

Asante ndugu Kipala kwa kunielekeza kile ambacho nilikua sikifahamu hapo awali, lakini sasa nimefahamu hivyo sitofanya hivyo tena na nitajaribu kuzipitia makala zote ambazo niliziwekea jamii hiyo na wakati mwingine takua mdadisi kwanza kabla ya kuweka jamii husika. Anuary Rajabu (majadiliano) 15:24, 20 Agosti 2022 (UTC)[jibu]
Asante kwa jibu zuri. Sitaki kukusumbua nafurahi kamba unajifunza haraka na kuboresha wikipedia yetu. Kipala (majadiliano) 19:24, 20 Agosti 2022 (UTC)[jibu]
Asante sana. Anuary Rajabu (majadiliano) 19:29, 20 Agosti 2022 (UTC)[jibu]

Tafadhali uwe macho makala zilizotafsiriwa kwa kompyuta[hariri chanzo]

Habari naona ulijitahidi kusahihisha makala kadhaa ambazo niliangalia baadaye na kuzipendekeza kwa ufutaji (k.v. Itifaki ya Mitandao ya Kijamii iliyosambazwa, Ufahamu wa mazingira. Ukiona matini ni vigumu nashukuru ukihakikisha kama ni tafsiri ya kompyuta. Wengine kama Mwambashi901 hawaonyeshi interwiki; mara nyingi ni rahisi kutambua makala ya enwiki waliyojaribu kutafsri, kwa kumwaga jina la makala katika google translate (maana huko walichukua jina). Mimi hutumia google translate kutafsiri sehemu ya kwanza kutoka enwiki kwenda sw, halafu nalinganisha kwenye ukurasa wa word pande zote kandokando (natumia jeswali).

Nikiona A) matini imepokelewa neno kwa neno kutoka google, na B) Kiswahili kina kasoro, makosa au hakieleweki, ninaamua kama naweza kuisahihisha (au kama ninapenda kutumia muda wangu kwa jambo hili) halafu C) ama ninasahihisha au D) ninabandika kigezo cha {{futa}} na kuandikisha makala katika orodha ya Wikipedia:Makala kwa ufutaji (kwa kubofya link yake), ambako mwingine ataiangalia na kuamua.

Kwa jumla uone Msaada:Tafsiri_ya_kompyuta. Nitashukuru ukiweza kusaidia kutambua makala zenye lugha na tafsiri mbaya. Tumepata idadi kubwa ya makala kupitia google translate na tokeo lake ni kweli hatari kwa ajili ya wikipedia hiyo. Kipala (majadiliano) 07:16, 8 Septemba 2022 (UTC)[jibu]

Asante sana kwa maelekezo yako na nimekuelewa vizuri sana, hivyo kuanzia sasa tajitahidi niwe napitia vema makala hasa za watumiaji wapya ambao ndio wanaanza kachangia katika Wikipedia ya kiswahili na pia baadhi ya watumiaji wengine ambapo makala zao zinakua na dalili ya kutungwa na kompyuta na makosa mengine mbalimbali.
Lakini pia naomba kujua je, nikikutana na makala yenye dalili ya kutungwa na kompyuta nina ruhusiwa pia kuweka alama ya "Tafsiri ya Kompyuta" au hiyo inaruhusiwa kwa "Wakabidhi" tu? Anuary Rajabu (majadiliano) 12:03, 8 Septemba 2022 (UTC)[jibu]
ukiona dalili weka alama tu. Pia pendekezo la "futa". Maazimo ya baadaye yatachukuliwa na wakabidhi. Kipala (majadiliano) 12:20, 8 Septemba 2022 (UTC)[jibu]
Sawa asante sana nimeelewa nitajitahidi kuwa nafanya hivyo. Anuary Rajabu (majadiliano) 15:57, 8 Septemba 2022 (UTC)[jibu]

Dead links[hariri chanzo]

Habari, asante kwa kusafisha dead links. Kwa jumla si vibaya tukichungulia kama hiyo link imehamishwa kabla ya kufuta tu. Wakati mwingine inasadia kutafuta kwa google jina la makala inayotajwa . ---- Pamoja na hayo je umeshapiga kura ukurasa wa Jumuiya? Kipala (majadiliano) 13:47, 9 Novemba 2022 (UTC)[jibu]

Asante sana kwa kuniewesha kwani hapo awali nilijua hazina maana yoyote, sasa nimeelewa. Ndio kura nimeshapiga tayari kwenye ukurasa wa Jumuiya. Anuary Rajabu (majadiliano) 13:57, 9 Novemba 2022 (UTC)[jibu]
Samahani kwa kuingilia majadiliano hayo, mimi pia najitahidi kuondoa dead links, kumbe ni afadhali tuziache? Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:58, 11 Novemba 2022 (UTC)[jibu]
Bila ya samahani, hakika asante sana kwa kuchangia, kwa mujibu wa ndugu @Kipala ni afadhali tuziache au kabla ya kuifuta ni bora kuichungulia kwanza kama haijahamishwa Anuary Rajabu (majadiliano) 14:17, 11 Novemba 2022 (UTC)[jibu]
Ushauri wangu ni: kama ziko bure, tuzifute tu. Lakini mimi naona mara kadhaa marejeo yaleyale yanapatikana kwa anwani tofauti, nikitafuta jina la faili katika google. Inachukua muda zaidi kuchungulia, kwa hiyo kila mmoja anapaswa kuamua mwenyewe. Kipala (majadiliano) 19:06, 11 Novemba 2022 (UTC)[jibu]
Sawa sawa hapo nimeelewa na hata ndugu @Riccardo Riccioni natumaini nayeye ameelewa labda kama analo la kuongezea. Anuary Rajabu (majadiliano) 19:24, 11 Novemba 2022 (UTC)[jibu]

Sending regards and few questions to ask...[hariri chanzo]

Hello, if I may I will shift to Kiswahili. Ni kwamba asante kwa ukaribisho Mzuri kutoka juu na pia ya kuongeza asante hata kwa university wikimedians kwa kunipa nafasi ya kujiunga katika platform hii ya wikipedia... Niko ma swali, mona ni kwamba inakuaje kama nitahitaji kuweka picha na hio picha haipo kwenye platform yeyote ya wikipedia but only inapatikana kwenye mtandao mara nyingine kwenye tovuti kuu husina inayoshikiria hati miliki. Na pili nimeweza kuweka picha pamoja na taarifa kwa kiufupi kama inavoonekana kwenye makala za watu au makampuni. Ni hayo tu, Shukran sana na nitakua pamoja na nyie. Denis R. John 196.249.97.46 19:29, 27 Novemba 2022 (UTC)[jibu]

Salaam ndugu,
Asante sana kwa swali lako zuri na karibu sana kwenye Wikipedia ya kiswahili, hivyo kwa mujibu wa taratibu za Wikipedia huzingatia sana faragha za mtu binafsi, kwahivyo huruhusiwi kuchukua picha ya kitu au mtu au media yeyote kutoka kwenye nyenzo zingine au mitandao ya kijamii na kuweza kuitumia kwenye makala za wikipedia bila ya ridhaa ya mmiliki husika.
Na ili kuweza kutumia picha husika kwenye makala za wikipedia, kwanza kabisa inakupasa kuipakia kwenye jukwaa la Wikimedia Commons kwa kuzingatia taratibu zote za faragha za mmiliki wa picha au media husika au kama picha au media hiyo uliipiga au kuandaa wewe mwenyewe pia bila ya kupitia huko kwenye nyenzo zingine au mitandao ya kijamii.
Asante,amani kwako. Anuary Rajabu (majadiliano) 12:34, 30 Novemba 2022 (UTC)[jibu]

Translations for Wikimania 2023[hariri chanzo]

Hi Anuary Rajabu,

You are receiving this notification because you have listed yourself as a volunteer for Wikimania 2023 either on Meta or on Wikimania wiki. We already have a few pages related to Wikimania 2023 available for translation on Wikimania wiki. Your help with translating these pages in your languages would be highly appreciated. Currently the following pages are available for translation:

If you do not want to reiceive further notifications about pages related to Wikimania 2023, which are available for translation, you may remove your name from this list.

Thanks for your help! --Ameisenigel (talk)

This message was delivered through [[<tvar name="mass-delivery">Special:MyLanguage/Global message delivery</tvar>|Global message delivery]] --MediaWiki message delivery (majadiliano) 14:14, 28 Desemba 2022 (UTC)[jibu]

Translations for Wikimania 2023[hariri chanzo]

Hi Anuary Rajabu,

You are receiving this notification because you have listed yourself as a volunteer for Wikimania 2023 either on Meta or on Wikimania wiki or because you have subscribed on Meta. We already have a few pages related to Wikimania 2023 available for translation on Wikimania wiki. Your help with translating the following pages in your languages would be highly appreciated:

If you do not want to reiceive further notifications about pages related to Wikimania 2023, which are available for translation, you may remove your name from this list.

Thanks for your help! --Ameisenigel (talk)

This message was delivered through Global message delivery --MediaWiki message delivery (majadiliano) 14:50, 22 Januari 2023 (UTC)[jibu]

Habari SISTY MUSHISA (majadiliano) 11:26, 17 Februari 2023 (UTC)[jibu]

Translations for Wikimania 2023[hariri chanzo]

Hi Anuary Rajabu,

You are receiving this notification because you have listed yourself as a volunteer for Wikimania 2023 either on Meta or on Wikimania wiki or because you have subscribed on Meta. Your help with translating the following pages on Wikimania wiki in your languages would be highly appreciated:

If you do not want to reiceive further notifications about pages related to Wikimania 2023, which are available for translation, you may remove your name from this list.

Thanks for your help! --Ameisenigel (talk)

This message was delivered through Global message delivery --MediaWiki message delivery (majadiliano) 09:40, 4 Machi 2023 (UTC)[jibu]

Makala kuhusu Analog Pussy[hariri chanzo]

Ndugu nmeona pitio lako katika makala hii  https://sw.wikipedia.org/wiki/Analog_Pussy,na ningependa kujua je kundi la muziki lenye kufanya kazi za muziki sindo kundi la wanamuziki?,ningependa kujua juu ya hilo ili makosa kama hayo yasijirudie. Amami sana Husseyn Issa (majadiliano) 19:33, 14 Aprili 2023 (UTC)[jibu]
Yote ni sahihi lakini tukisema kundi la wanamuziki, hapo naona inakua inaleta maana nzuri zaidi kwa sababu inajumuisha muunganiko wa watu fulani kwenye kazi ya muziki, kuliko tukisema kundi la muziki (ambapo hapa mwingine anaweza kufafanua kama mjumuisho wa aina fulani za muziki n.k) Anuary Rajabu (majadiliano) 20:29, 14 Aprili 2023 (UTC)[jibu]
Sawa sawa Husseyn Issa (majadiliano) 22:04, 14 Aprili 2023 (UTC)[jibu]


Feminism and Folklore 2023 - Local prize winners[hariri chanzo]

Please help translate to your language

Congratulations on your remarkable achievement of winning a local prize in the Feminism and Folklore 2023 writing competition! We greatly appreciate your valuable contribution and the effort you put into documenting your local Folk culture and Women on Wikipedia. To ensure you receive your prize, please take a moment to complete the preferences form before the 1st of July 2023. You can access the form by clicking here. We kindly request you to submit the form before the deadline to avoid any potential disappointments.

If you have any questions or require further assistance, please do not hesitate to contact us via talkpage or Email. We are more than happy to help.

Best wishes,

FNF 2023 International Team

Stay connected  

--Tiven2240 (majadiliano) 13:30, 10 Juni 2023 (UTC)[jibu]

Organizer Tools Office Hours & Event Discovery Project[hariri chanzo]

(Lire ce message en français); (Ver este mensaje en español); (Angalia ujumbe huu kwa Kiswahili); (إقرأ هذه الرسالة بالعربي) Please help translate to your language .

The Campaigns team at the Wikimedia Foundation has some updates to share with you, which are:

We invite you to attend our upcoming community office hours to learn about organizer tools, including the Event registration tool (which has new and upcoming features). The office hours are on the following dates, and you can join one or both of them:

  • Saturday, October 7 at 12:00 UTC (Register here)
    • Languages available: Arabic, English, French, Swahili
  • Tuesday, October 10 at 18:00 UTC (Register here).
    • Languages available: Arabic, English, French, Portuguese, Spanish, Swahili

We have launched a new project: Event Discovery. This project aims to make it easier for editors to learn about campaign events. We need your help to understand how you would like to discover events on the wikis, so that we can create a useful solution. Please share your feedback on our project talk page.

Thank you, and we hope to see you at the upcoming office hours!

MediaWiki message delivery (talk) 19:54, 24 Septemba 2023 (UTC)[jibu]

You are receiving this message because you subscribed to this list

Affiliations Committee News (January-March 2024)[hariri chanzo]

Group photo of the 2023 EduWiki Conference in Belgrade, organized by Wikipedia & Education User Group

You can find this newsletter translated into additional languages on Meta-wiki. Please help translate to your language

Quarterly newsletter sharing news and events about the work of Wikimedia's Affiliations Committee.

MediaWiki message delivery (majadiliano) 12:56, 18 Aprili 2024 (UTC)[jibu]

Ukumbusho kuhusu kupiga kura sasa ili kuchagua washiriki wa U4C ya awamu ya kwanza[hariri chanzo]

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language

Ndugu Mwanawikimedia,

Unapokea ujumbe huu kwa sababu hapo kabla uliwahi kushiriki katika mchakato wa UCoC.

Huu ni ukumbusho kwamba kipindi cha kupiga kura kwa Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) kitamalizika tarehe 9 Mei 2024. Soma maelezo kwenye ukurasa wa kupiga kura kwenye Meta- wiki ili kupata maelezo zaidi kuhusu upigaji kura na ustahiki wa mpiga kura.

Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) ni kikundi cha kimataifa kilichojitolea kutoa utekelezaji sawa na thabiti wa UCoC. Wanajamii walialikwa kutuma maombi yao kwa U4C. Kwa maelezo zaidi na majukumu ya U4C, tafadhali pitia Mkataba wa U4C.

Tafadhali washirikishe ujumbe wanajumuiya wenzako ili nao waweze kushiriki.

Kwa niaba ya timu ya mradi wa UCoC,

RamzyM (WMF) 22:54, 2 Mei 2024 (UTC)[jibu]