Wikipedia:Makala kwa ufutaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta


Majadiliano ya awali yamehamishwa kwenye kurasa hizi:

Ongeza michango chini ya mstari wa mwisho!

Amilton of Christ

Makala ni tafsiri baya ya kompyuta tena nina mashaka kama anastahili makala. Mwandishi amesambaa makala juu yake kwenye wikipedia mbalimbali (de wameshamfuta, en bado iko kwa Kiingereza kibaya mno). Ilhali ni kweli mtu huyu yupo (vitabu vyake vyaonekana hapa: http://www.general-ebooks.com/author/97544770-amilton-de-cristo) hata jina lake si vile jinsi inavyoandikwa maana hali halisi aitwa "Amilton de Cristo". Haiwezi kubaki ilivyo, mimi sisikii wito wa kuisahihisha. Labda afutwe (hadi anapanusha crusade zake hadi Bongo..). Kipala (majadiliano) 06:57, 11 Septemba 2014 (UTC)

Kweli, shida za lugha zirekebishwe, lakini hata wikipedia ya Kiingereza ina makala kuhusu yake, kwa hiyo napendekeza ibaki. --Baba Tabita (majadiliano) 11:14, 11 Septemba 2014 (UTC)

Chocheeni Kuni‎??

Sina uhakika juu ya hali ya hakimiliki katika Tanzania kuhusu matini ya nyimbo. Nashauri mtu ajaribu kupata kibali chake, au kutoa maelezo hapo. Kipala (majadiliano) 16:38, 7 Mei 2015 (UTC)

Wikamusi

Makala ilivyo haifai. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 07:33, 6 Septemba 2015 (UTC)

Kizito Mihigo - IBAKI!

Tafsiri ya kompyuta, tena vibaya. Sina uhakika kama lemaa inafaa kweli au kama ni jaribio la kujitangaza tu. Isahihishwe au kufutwa. --Kipala (majadiliano) 08:38, 3 Oktoba 2015 (UTC)

Sasa , maandishi lazima lirekebishwe. si ifutwe Umutesi84 (majadiliano) 09:44, 3 Oktoba 2015 (UTC)
Baada ya marekebisho kadhaa, naona makala ibaki. Hata hivyo, marekebisho ya lugha n.k. yaendelee. --Baba Tabita (majadiliano) 07:17, 20 Oktoba 2015 (UTC)

PICHA SAWIRISHA

Inaonekana kama mwanzo wa riwaya; haifai kwa kamusi elezo, yaani ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 07:11, 20 Oktoba 2015 (UTC)

Facebook

Tafsiri baya , ama ya kompyuta au ya mhariri mvivu. Isibaki ilivyo. Ingawa lemma inapendwa sana, sioni faida ibaki kama haiborshwi. Kipala (majadiliano) 06:33, 26 Oktoba 2015 (UTC)