Chocheeni Kuni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Hali Ngumu"
Wimbo wa Mrisho Mpoto
Umetolewa 2 Aprili, 2014
Umerekodiwa 2014
Aina ya wimbo Muziki wa asili
Lugha Kiswahili
Urefu 5:32
Studio Soround Sound Studio
Mtunzi Mpoto
Mtayarishaji Allan Mapigo

Chocheeni kuni ni jina la wimbo wa aina ya muziki wa dansi ya asili uliyoimbwa na mwimbaji Mrisho Mpoto kutoka nchini Tanzania. Wimbo ulitoka mwaka wa 2014. Ni muendelezo wa mashairi yenye utata, yaani, utunzi wa hali ya juu katika kufumba maneno mazito dhidi ya siasa za Tanzania.

Mashairi ya wimbo[hariri | hariri chanzo]

KIITIKIO:
Chocheeni kuni mbichi moto ukolee
Ugali uive mnachotaka kitokee
Alikeni mamluki, wakija wangojee
Mikeka waweke, wanachotaka kitokee
Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea , chochea , chochea oooo
Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea , chochea , chochea, chochea…

UBETI WA KWANZA:
Watanzania, mwenda kwao siku zote haogopi giza
Acheni nirudi nyumbani safari imenishinda, nauli zenu nitarudisha.
Mtu anatapika nyongo yake, anailamba tena anaangaliwa
Ni sawa na tawi kavu linapoanguka watu wakapiga kelele, ayaaaa
Katika misimu minne kwa mwaka, tuongeze msimu mwingine wa kujiridhisha
Raha ya jamvi siku zote ni viraka viraka,
Na dungu, linamficha mlinzi wa ndege wakati wa mvua tu
Eti ooo, imenyesha juzi tu, maji sio mengi, nisubirini kule
Ilishindikana vipi kuyapima maji kwa mti, ndio mkawaambia watu wavuke
Mjomba, binadamu ni kama ganda la kitabu,
Mpaka umfungue maandishi, ndio uweze kumuelewa
Eti lilotokea mbali tufanye limepita, na haliwezi kumdhuru mwingine
Kweli! Inayotaka kunyesha huwa haisubiri mawingu
Mimi, sidhani kama kujiponya kwa mambo mazito
Tunahitaji cheti kilichogongwa muhuri wa moto
Au mtaalamu wa magonjwa ya akili, zaidi ya kutumia neno sahau tu
Unawaulizaje watu magongo ya nini, wakati umesema kuna nyoka?
Mjomba, wewe si uliwapaka wanja, ngoja wao wakupake pilipili
Halafu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga

KIITIKIO:
Chocheeni kuni mbichi moto ukolee
Ugali uive mnachotaka kitokee
Alikeni mamluki, wakija wangojee
Mikeka waweke, wanachotaka kitokee
Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea , chochea , chochea oooo
Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea , chochea , chochea, chochea…

UBETI WA PILI:
Mngekuwa mnajua anachokula nyuki, msingethubutu kusema asali ni tamu
Niwashukuru, kwa kufikiri mjini ni hifadhi yenu
Halikuwa wazo baya kwa wakati ule
Maana mlionyesha ukomavu kutoka kwenye shingo kwenda chini na sio juu
Mbona hamkumfikiria aliyekuwa ndani kafungiwa kwa nje?
Usingizi hapati anawaza jinsi ya kutoka
Nikisema uwezo wa watu kufikiri na mahitaji unatofautiana,
mtaanza kusema nina dharau na matusi
Lakini kumbukeni ulimi unauma kuliko meno
Mnawezaje kumfikiria aliyekuwa ndani,
kajifungia mwenyewe, funguo anazo mwenyewe,
Kalala fo fo fo, asijue hata idadi ya misumari iliyoshikilia mlango wake
Kulipamba jeneza, hakumfanyi aliyekufa kufufuka nyinyi
Kama kusema nimeshasema sana, mwishowe nitakuwa kama mwanasiasa
Hawajitokezi mpaka kuwe na maafa

Natoa katoni ishirini za sabuni ya unga, aliyekwambia wale wachafu nani?
Kasafisheni kwanza nyoyo zenu ndio mrudi kwa wananchi
Ndugu zangu, tawi kavu, kuanguka wala sio ajabu
Wakati wao wanatenganisha mavi ya panya kwenye unga
Ninyi chicheeni kuni zilizoloa, maji yapate moto ugali usongwe
wakiwauliza, waambieni huu ni utani hehehe, Hapa kwetu tuna makabila 120, tunataniana
Waliopo hatuwataki, wanaotaka hatuwaamini
Maneno siku zote yanauma na yanachefua ukijua maana yake
Kwa mfano neno la kitoto, mtoto kumwambia mtoto tunasema watoto wanacheza
Neno la kitoto, mtoto kumwambia mkubwa tunasema mtoto anakuwa
Mtoto akisema babaa, ile ndege yangu,
Baba hata kama huna baiskeli, utamwambia ikitua nitakuletea, ndio utaratibu
Lakini maneno ya kitoto, mtu mzima kumwambia mtu mzima mwenzie, kuna walakini
Mimi safari imenishinda, na sitaki tena kuulizwa kwanini

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]