Wikipedia:Makala kwa ufutaji/Nyaraka 3

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Hii ni nyaraka ya makala Wikipedia:Makala kwa ufutaji tangu Januari 2014.

Kwa nyaraka za zamani zaidi angalia hapa.

Yaliyomo

Kundi la Lucy Lee na wengine[hariri chanzo]

Nyomi Banxxx, Tyra Banxxx Ariana Jollee, Cytherea, Daisy Marie,Tanner Mayes,Joanna Angel,Brandi Lyons,Alexis Love,Anksa Kara,Lucie Theodorova, vyote vinaletwa na mtumiaji asiyeandikisha na asiyejua Kiswahili; anaonekana ana hamu kubwa kuongeza idadi ingawa nimeshambana mara 2. Vyote vina maandishi "XYZ (amezaliwa ... katika..) ni ki-.... (nchi, kutajwa kwa makosa) pornographic mwigizaji." Mengine yana pia: "Yeye aliingia wazima sekta ya filamu ya mwaka ... katika umri wa miaka karibu .. ." Kama mtu ana hamu ya kuisahihisha - karibu. Kama la - zifutwe. Kipala (majadiliano) 20:40, 18 Novemba 2013 (UTC)

Hakuna marekebisho tangu Mzee Kipala ameshauri zifutwe miezi miwili iliyopitwa. Zimefutwa zote. --Baba Tabita (majadiliano) 11:03, 11 Januari 2014 (UTC)

Mchango wa wanafunzi wa kigeni wanaosoma kiswahili katika kukuza na kue ndeleza llugha ya kiswahili‎[hariri chanzo]

Si makala sina uhakika kama inaweza kujengwa kuwa makala. Kipala (majadiliano) 07:49, 4 Desemba 2013 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 11:06, 11 Januari 2014 (UTC)

Gaspa simon ngowi[hariri chanzo]

Gaspa Ngowi ni meneja uendeshaji wa startimes Tanzania, Pia ni PHD candidates toka chuo kikuu cha dar es salaam

Jinsi ya kunyua chuma[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai kwa kamusi. Kwa sasa, hasa ni ushauri kuhusu unyanyuaji vyuma (kwa Kiingereza "Weightlifting"). Bila marekebisho na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:08, 9 Desemba 2013 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 11:46, 11 Januari 2014 (UTC)

KUOKOKA NI NINI?[hariri chanzo]

Si makala bali ni uinjilisti. Hata kichwa hakifai kwa kamusi. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:10, 9 Desemba 2013 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 11:46, 11 Januari 2014 (UTC)

Romeo and Juliet[hariri chanzo]

Haina yaliyomo. Isipoingiziwa na habari ya igizo la Shakespeare, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 11:19, 11 Januari 2014 (UTC)

Makala imefutwa na Kipala saa 15:33, tarehe 11 Januari 2014 (UTC).

Taarifa za elimu wilaya ya same[hariri chanzo]

Yaliyomo ni swali si makala. Kwa vyovyote habari hizo ziingizwe katika makala ya Wilaya ya Same. Kwa hiyo makala hii ya sentensi moja tu ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 11:43, 11 Januari 2014 (UTC)

Makala imefutwa na Kipala saa 15:32, tarehe 11 Januari 2014 (UTC).

Vitabu bora 100 vya gazeti Le Monde[hariri chanzo]

Imenakilishwa kutoka Kiingereza tu bila kutafsiriwa. Isipotafsiriwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:55, 11 Januari 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 28 Januari. --Baba Tabita (majadiliano) 18:16, 30 Januari 2014 (UTC)

Lugha ya mazungumzo[hariri chanzo]

Ina sentensi moja tu isiyofaa kwa kamusi elezo. Isipoongezewa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 11:24, 11 Januari 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 28 Januari. --Baba Tabita (majadiliano) 18:16, 30 Januari 2014 (UTC)

Sung Jae-ki[hariri chanzo]

Makala haieleweki jinsi ilivyo. Ama isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 12:32, 11 Januari 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 28 Januari. --Baba Tabita (majadiliano) 18:16, 30 Januari 2014 (UTC)

Seo Jae-pil[hariri chanzo]

Vilevile makala hiyo haieleweki kwa ajili ya kutafsiriwa kikompyuta. Isiporekebishwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:05, 11 Januari 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 28 Januari. --Baba Tabita (majadiliano) 18:16, 30 Januari 2014 (UTC)

Park Jung-yang[hariri chanzo]

Vilevile makala hiyo haieleweki kwa ajili ya kutafsiriwa kikompyuta. Isiporekebishwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:05, 11 Januari 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 28 Januari. --Baba Tabita (majadiliano) 18:16, 30 Januari 2014 (UTC)

Madhara ya ugonjwa wa kaswende[hariri chanzo]

Ni swali la mtumiaji tu. Isipoandikwa upya pamoja habari zifaazo na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:59, 25 Januari 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 28 Januari. --Baba Tabita (majadiliano) 18:16, 30 Januari 2014 (UTC)

Mikoa ya Mara na Mwanza[hariri chanzo]

Kuna makala kuhusu Mkoa wa Mara na Mkoa wa Mwanza. Siyo lazima kuandika makala kuhusu mikoa miwili. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:59, 25 Januari 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 28 Januari. --Baba Tabita (majadiliano) 18:16, 30 Januari 2014 (UTC)

't Hoeveke[hariri chanzo]

Haifai ilivyo. --Baba Tabita (majadiliano) 15:00, 27 Januari 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 28 Januari. --Baba Tabita (majadiliano) 18:16, 30 Januari 2014 (UTC)

Electrical Installation.[hariri chanzo]

mchnago ni Kiingereza, haina habari ndani yake na ni fupi mno. Lakini ni mchango wa mchangiaji mpya aliyejiandikisha leo tu kwa hiyo nimemwandikia ana siku kadhaa ya kuiswahilisha. Kama la ifutwe.Kipala (majadiliano) 09:35, 5 Februari 2014 (UTC)

Imefutwa tarehe 19 Machi na MoiraMoira. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2014 (UTC)

Mwandishi imebaki[hariri chanzo]

ni fupi mno, inafaa kwa wikikamusi lakini si kwa wikipedia. Iongezwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 22:35, 5 Februari 2014 (UTC)

Imefutwa tarehe 19 Machi na MoiraMoira. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2014 (UTC)
Imeandikwa upya. iko. Kipala (majadiliano) 19:10, 26 Septemba 2018 (UTC)

Kigezo:Deletable file/doc[hariri chanzo]

Documentation subpage of a non-existing template. TintoMeches (majadiliano) 14:15, 8 Februari 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2014 (UTC)

Nyota ya mtu[hariri chanzo]

Kumeandikwa jina la mtu tu. Kama hata kichwa cha makala hakileti maana ya kuongeza habari, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 02:11, 11 Februari 2014 (UTC)

Imefutwa tarehe 8 Machi na Kipala. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2014 (UTC)

Misheni au CDC[hariri chanzo]

Kichwa cha makala hakifai (in mada mbili), na tena tusianzishe makala za mbegu kwa mtaa wowote tu. Ifutwe, --Baba Tabita (majadiliano) 02:27, 11 Februari 2014 (UTC)

Imefutwa tarehe 19 Machi na MoiraMoira. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2014 (UTC)

Polar Night[hariri chanzo]

Kichwa ni kwa Kiingereza, habari za makala ni kwa Kiswidi. Bila kutafsiriwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 02:28, 11 Februari 2014 (UTC)

Imefutwa tarehe 19 Machi na MoiraMoira. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2014 (UTC)

Chuchu thedon bling[hariri chanzo]

Makala inahusu mtu binafsi ambaye hana umaarufu wowote nchini Tanzania. Kifupi si mtu wa kuelezwa kwenye Wikipedia. Labda ajielezee mwenyewe kwenye ukurasa wake wa mtumiaji. Ifutwe!--MwanaharakatiLonga 06:48, 24 Februari 2014 (UTC)

Imefutwa tarehe 19 Machi na MoiraMoira. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2014 (UTC)

Mkinga aitwae lwembe[hariri chanzo]

Nahisi kuna maana katika habari lakini si makala kabisa. Labda iingizwe kama habari katika makala ya kieneo?? Au ifutwe. Kipala (majadiliano) 21:31, 7 Machi 2014 (UTC)

Imefutwa tarehe 19 Machi na MoiraMoira. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2014 (UTC)

Orodha ya watu maarufu wa Tanzania[hariri chanzo]

Makala haileti maana ilivyo. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:21, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:35, 1 Mei 2014 (UTC)

Sifongo[hariri chanzo]

Makala ilivyo ni fupi mno, tena haifai. Isiporekebishwa na kupanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:21, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:35, 1 Mei 2014 (UTC)

Ja Rule - IBAKI![hariri chanzo]

Makala haileti maana ilivyo. Isipoelezewa vizuri na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:21, 14 Aprili 2014 (UTC)

Salaam. Kesi hii nimeimaliza! Hakuna tena haja ya kuifuta. Nimeboresha makala kadiri ipasavyo. Wako, Muddyb!--MwanaharakatiLonga 14:57, 14 Aprili 2014 (UTC)
Asante sana kwa kuiokoa makala hiyo. Wasalaam, BT --Baba Tabita (majadiliano) 17:20, 14 Aprili 2014 (UTC)

Bwin[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai, hasa ni ombi la mtumiaji asiyesajiliwa. Ikiwa "Bwin" ni mada ambayo ingestahili makala katika kamusi elezo, basi makala iandikwe. La sivyo na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:33, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 10:02, 9 Mei 2014 (UTC)

Moderaterna‎ - IBAKI![hariri chanzo]

Sielewi maana ya makala ni nini. Inaonekana mwandishi hajui Kiswahli anataka kusambaza chama chake kwa njia ya google-translate au nini. Mtu aisahihishe au ifutwe. Kipala (majadiliano) 19:22, 22 Aprili 2014 (UTC)

Nimesanifisha makala ili kuhifadhi habari za chama cha serikali cha Uswidi. Bila shaka makala ipanuliwe lakini sasa angalao inaweza kubaki. --Baba Tabita (majadiliano) 10:25, 9 Mei 2014 (UTC)

Dunia Uwanja wa Fujo - IBAKI![hariri chanzo]

Makala haieleweki. Mwandishi ni mwanawikipedia mpya. Inawezekana anaandika juu ya riwaya fulani lakini hasemi hii ni riwaya iliyotungwa na nani, mwaka gani, wapi kwa hiyo habari za kimsingi hazipo. Inaonekana ni kama insha juu ya riwaya fulani. Naona isahihishwa sana au ifutwe. Afadhali mwandishi achangie hapo maana yake ni nini apate ushauri Kipala (majadiliano) 20:20, 23 Aprili 2014 (UTC)

Baada ya kusanifishwa kiasi na Mzee Kipala (asante sana!), makala ibaki ijapokuwa bado inahitaji marekebisho. --Baba Tabita (majadiliano) 10:13, 9 Mei 2014 (UTC)

Adult Film Database[hariri chanzo]

Mtumiaji asiyejiandikisha ‎87.97.134.188 hajui Kiswahili. Sioni sababu ya kuisahihisha. Analeta fujo Kipala (majadiliano) 10:30, 7 Mei 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 10:06, 9 Mei 2014 (UTC)

XVideos[hariri chanzo]

Mtumiaji asiyejiandikisha ‎87.97.134.188 hajui Kiswahili. Sioni sababu ya kuisahihisha. Analeta fujo Kipala (majadiliano) 10:30, 7 Mei 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 10:07, 9 Mei 2014 (UTC)

Malimbuko[hariri chanzo]

Labda jambo la maana, lakini haiwezi kubaki ilivyo. Inyoshwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 20:18, 2 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala na kupelekwa kwa wikamusi tarehe 5 Juni. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:53, 5 Juni 2014 (UTC)

Nembo ya chama cha chadema[hariri chanzo]

Ingawa mada ya makala hiyo ingestahili makala, lazima ipanuliwe, k.m. picha ya nembo, historia yake n.k. La sivyo na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:21, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 5 Juni. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:53, 5 Juni 2014 (UTC)

Frank e mayaya[hariri chanzo]

Haijaonyeshwa kama mtu huyu angestahili makala katika kamusi elezo. La sivyo (ama kama ukurasa umeandikwa kwa kosa la kumaanisha ukurasa wa mtumiaji), na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:33, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:10, 4 Juni 2014 (UTC)

Kutombana>redirect[hariri chanzo]

Makala haifai kwa kamusi elezo, labda ingefaa kwa wikamusi. Hapa ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:33, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:29, 4 Juni 2014 (UTC)
Imerudi kama redirect Kipala (majadiliano) 19:12, 26 Septemba 2018 (UTC)

Mwandishi,[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai, hata kwenye kichwa cha makala kuna kosa. Makala ya "Mwandishi" ilifutwa tayari kwa hiyo hata makala hii ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:47, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:29, 4 Juni 2014 (UTC)

Nusu irabu imerudishwa[hariri chanzo]

Ingawa mada hiyo ingestahili makala, haifai ilivyo. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:47, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala na kupelekwa kwa wikamusi tarehe 5 Juni. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:53, 5 Juni 2014 (UTC)

RJ kadutu[hariri chanzo]

Haijaonyeshwa kama mtu huyu angestahili makala katika kamusi elezo. La sivyo na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:47, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:29, 4 Juni 2014 (UTC)

Savior Bartholomew[hariri chanzo]

Haijaonyeshwa kwa nini mtu huyo astahili makala katika kamusi elezo. Kama asingekuwa mtu mashuhuri, na makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 20:10, 1 Mei 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:14, 4 Juni 2014 (UTC)

Bhange Sports Newz‎[hariri chanzo]

Nimemweleza mtumiaji mpya Majadiliano_ya_mtumiaji:Lucas_Bang'ala_(Bhange) kasoro za makala. asahihishe au ifutwe. Kipala (majadiliano) 17:37, 7 Mei 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:29, 4 Juni 2014 (UTC)

Elijah mumo‎[hariri chanzo]

Iende baada ya wiki 2. Nimemwandikia mwenyewe kwenye ukurasa wa majadilino ahamishe matini. Kipala (majadiliano) 04:47, 15 Mei 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:29, 4 Juni 2014 (UTC)

H.Kila`s property[hariri chanzo]

Imeletwa na mtumiaji mchanga kabisa - nimemwandikia. Kwa hiyo tusifute mara moja, tumwachie wiki 1. Kipala (majadiliano) 18:54, 21 Mei 2014 (UTC)

Imefutwa sasa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:11, 4 Juni 2014 (UTC)

Profesa wa kwanza Tanzania[hariri chanzo]

Imeletwa na mtumiaji mchanga kabisa - nimemwandikia. Kwa hiyo tusifute mara moja, tumwachie wiki 1. Kipala (majadiliano) 19:09, 21 Mei 2014 (UTC)

Imefutwa sasa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:12, 4 Juni 2014 (UTC)

Selemani mkonje[hariri chanzo]

Haijaonyeshwa kwa nini mtu huyo astahili makala katika kamusi elezo. Kama asingekuwa mtu mashuhuri, na makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:37, 4 Juni 2014 (UTC)

Imefutwa na Kipala tarehe 4 Juni. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 07:32, 6 Juni 2014 (UTC)

International Energy Agency[hariri chanzo]

Makala ilivyo haileti maana. Bila marekebisho na habari mpya na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:24, 5 Juni 2014 (UTC)

Imefutwa tarehe 12 Juni. Poleni kwa kutoandika maarifa hapa. --Baba Tabita (majadiliano) 21:11, 18 Juni 2014 (UTC)

Debora - IBAKI![hariri chanzo]

Si makala. Lemma ina maana. Labda kazi kwa Riccardo? Kipala (majadiliano) 21:54, 5 Juni 2014 (UTC)

Riccardo ameshaokoa makala. Asante!! Ibaki. Kipala (majadiliano) 08:06, 7 Juni 2014 (UTC)

Inno e Marcia Pontificale - IBAKI![hariri chanzo]

Makala fupi mno. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 21:41, 4 Julai 2014 (UTC)

Imepanuliwa vema na Kipala. Asante, mzee! --Baba Tabita (majadiliano) 06:46, 5 Julai 2014 (UTC)

Allah Peliharakan Sultan - IBAKI![hariri chanzo]

Makala fupi mno. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 21:41, 4 Julai 2014 (UTC)

Imepanuliwa vema na Kipala. Asante, mzee! --Baba Tabita (majadiliano) 06:47, 5 Julai 2014 (UTC)

Kuvia akili[hariri chanzo]

Ingawa mada ya makala ingestahili makala, lazima kuiandika vizuri. Isiporekebishwa na kupanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:33, 14 Aprili 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:25, 8 Agosti 2014 (UTC)

Tamausha[hariri chanzo]

Makala ilivyo haieleweki. Labda ingefaa kwa wikamusi. Bila maelezo mazuri zaidi, ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 07:52, 12 Mei 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:25, 8 Agosti 2014 (UTC)

Buu[hariri chanzo]

Makala ilivyo ni fupi mno; haijapanuliwa kwa muda mrefu sasa. Labda ingefaa kwa wikamusi siyo kwa kamusi elezo lakini. Isipopanuliwa hivi karibuni na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 05:07, 12 Juni 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:25, 8 Agosti 2014 (UTC)

Orodha ya Watu Mashuhuri Kenya[hariri chanzo]

Sina uhakika kama itafaa kuwa na orodha ya viungo tu. Labda ingekuwa bora kuingiza aya ndani ya makala ya Kenya. Mnaonaje? --Baba Tabita (majadiliano) 21:09, 18 Juni 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:24, 8 Agosti 2014 (UTC)

Serikali ya Tanzania[hariri chanzo]

Makala fupi mno. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 21:41, 4 Julai 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:11, 8 Agosti 2014 (UTC)

Nunarput utoqqarsuanngoravit[hariri chanzo]

Makala fupi mno. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 21:41, 4 Julai 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:22, 8 Agosti 2014 (UTC)

Vikwazo vya mawasiliano[hariri chanzo]

Makala fupi mno. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 21:41, 4 Julai 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:22, 8 Agosti 2014 (UTC)

Shavu la mguu[hariri chanzo]

Makala fupi mno. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 21:41, 4 Julai 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:22, 8 Agosti 2014 (UTC)

Tofauti ya maana na semantiki[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai, tena inatumia vigezo vibaya. Bila marekebisho na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 21:54, 4 Julai 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:23, 8 Agosti 2014 (UTC)

Wikipedia:B56 Bplus CP[hariri chanzo]

Haiwezi kubaki jinsi ilivyo (tazama: Majadiliano ya Wikipedia:B56 Bplus CP) kwa jina hilio pia nina wasiwasi kama ana umaarufu wowote. Labda Muddy aseme? Kipala (majadiliano) 13:32, 20 Juni 2014 (UTC)

Imehamishwa kwa ukurasa wa Cyprian Benedict Mwageni aliyeanza kuandika habari hizo kama ukurasa wake wa mtumiaji. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 23 Agosti 2014 (UTC)

Kino[hariri chanzo]

Makala ya Kiingereza; yaliyomo yalingana zaidi na wikikamusi. Kipala (majadiliano) 14:00, 7 Agosti 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 23 Agosti 2014 (UTC)

Malick bandawe[hariri chanzo]

Makala imeandikwa Kiingereza na haina viwango vya Kiwiki hata punje. Ninapendekeza ifutwe haraka iwezekanavyo!--MwanaharakatiLonga 13:47, 20 Agosti 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 23 Agosti 2014 (UTC)

Sickora Gerald[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai. Kwanza, imeandikwa na mhusika mwenyewe. Pili, siyo makala ya kamusi elezo bali ni sifa pamoja na uvutaji wa kununua muziki wake. Tatu, haijaonyeshwa kama mtu huyo angestahili kupata makala katika kamusi elezo, yaani, kama ni mtu mwenye umuhimu wa kutosha katika jamii ya Tanzania. Lazima kumwambia mwandishi ajieleze. La sivyo, makala na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:43, 29 Julai 2014 (UTC)

Nimeifuta Kipala (majadiliano) 10:54, 9 Desemba 2014 (UTC)

Sosholoji >redirect[hariri chanzo]

Makala ilivyo haileti maana. Hata kichwa cha makala ni kosa. Mada huitwa "sosiolojia" au "elimujamii". Makala hii na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 23 Agosti 2014 (UTC)

Imerejelewa kwa Sosholojia, makala iliyoandikwa na Riccardo Riccioni. Asante, mzee! --Baba Tabita (majadiliano) 09:47, 22 Desemba 2014 (UTC)

Orodha ya miji ya Kireno[hariri chanzo]

Makala haileti maana, ni orodha ya miji michache tu bila viungo wala maelezo zaidi. Machoni mwangu ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:56, 5 Oktoba 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 09:09, 26 Desemba 2014 (UTC)

Orodha ya wanasiasa wa EACU[hariri chanzo]

Makala haileti faida kwa kamusi elezo kwa vile inaonyesha jina moja tu. Tena kiungo chake ni chekundu, yaani makala yake haijaandikwa. Naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:58, 5 Oktoba 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 09:09, 26 Desemba 2014 (UTC)

Maghani IBAKI![hariri chanzo]

Kifupi mno. Ihamishwe wikikamusi au kufutwa tu au kuongezwa. Kipala (majadiliano) 21:22, 6 Oktoba 2014 (UTC)

Nimeongeza kiasi. --Baba Tabita (majadiliano) 13:57, 31 Oktoba 2014 (UTC)

Africa Safari Air[hariri chanzo]

Ni orodha ya miji tu; makala haijaeleza mambbo kuhusu ile kampuni ya ndege. Isipopanuliwa na makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:06, 31 Oktoba 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 09:11, 26 Desemba 2014 (UTC)

Utatuzi wa migogoro[hariri chanzo]

Makala ilivyo ni orodha ya matukio katika historia ya Afrika tu. Ama iunganishwe na makala ya Historia ya Afrika ama ipanuliwe kuleta maana vizuri. La sivyo na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 16:38, 7 Novemba 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 09:10, 26 Desemba 2014 (UTC)

Breath Takers[hariri chanzo]

Makala hii inahusu kundi la muziki ambalo si maarufu. Katika wikipedia ya Kiingereza makala ilikuwa imeshafutwa, angalia hapa. Naona na ifutwe na kwetu. --Baba Tabita (majadiliano) 14:38, 9 Novemba 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 09:10, 26 Desemba 2014 (UTC)

Chuma (maana)[hariri chanzo]

Haina viungo. Tena haileti maana kuingiza chuma kama kitenzi katika kamusi elezo. Naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:33, 16 Novemba 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 09:10, 26 Desemba 2014 (UTC)

Thumbnail[hariri chanzo]

Yote iko chini ya kichwa kisichofaa, halafu mpangilio... Ama mtu aipange ipasavyo mahali pake au ifutwe. Kipala (majadiliano) 07:40, 5 Desemba 2014 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 09:42, 22 Desemba 2014 (UTC)

Copyright[hariri chanzo]

Makala inarejesha kwa kiungo chekundu, yaani makala ya hakimiliki haijaandikwa. Isipoandikwa, na makala hiyo ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 18:37, 23 Novemba 2014 (UTC)

Imefutwa 22:45, 31 Januari 2015 tayari. --Baba Tabita (majadiliano) 08:21, 2 Februari 2015 (UTC)

Lugha ya mitaani[hariri chanzo]

Makala haileti maana. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 02:58, 9 Desemba 2014 (UTC)

Imefutwa 17:47, 24 Februari 2015 tayari na Sj. --Baba Tabita (majadiliano) 19:17, 25 Februari 2015 (UTC)

Harafa[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai kwa kamusi elezo ila labda kwa wikamusi. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:28, 18 Januari 2015 (UTC)

Imefutwa. Kipala (majadiliano) 04:15, 11 Machi 2015 (UTC)

ICSW[hariri chanzo]

Vifupisho virejee kwa makala ya jina refu kamili lakini visistahili kupata makala yenyewe. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:28, 18 Januari 2015 (UTC)

Imefutwa. Kipala (majadiliano) 04:16, 11 Machi 2015 (UTC)

IPR[hariri chanzo]

Vifupisho virejee kwa makala ya jina refu kamili lakini visistahili kupata makala yenyewe. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:28, 18 Januari 2015 (UTC)

Imefutwa. Kipala (majadiliano) 04:16, 11 Machi 2015 (UTC)

Mchongoano[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai kwa kamusi elezo ila labda kwa wikamusi. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:28, 18 Januari 2015 (UTC)

Imefutwa. Kipala (majadiliano) 04:18, 11 Machi 2015 (UTC)

AMCEN - IBAKI![hariri chanzo]

Vifupisho virejee kwa makala ya jina refu kamili lakini visistahili kupata makala yenyewe. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:40, 18 Januari 2015 (UTC)

Nimeipanua, ibakiKipala (majadiliano) 05:09, 11 Machi 2015 (UTC)

IFM[hariri chanzo]

Vifupisho virejee kwa makala ya jina refu kamili lakini visistahili kupata makala yenyewe. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:40, 18 Januari 2015 (UTC)

Imefutwa saa 23:04, tarehe 22 Februari 2015 na Kipala. --Baba Tabita (majadiliano) 19:20, 25 Februari 2015 (UTC)

ILC - IBAKI![hariri chanzo]

Vifupisho virejee kwa makala ya jina refu kamili lakini visistahili kupata makala yenyewe. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:40, 18 Januari 2015 (UTC)

imepanuliwa na kuhamishwa kwa jina ndefu. Kielekezo kibaki. Kipala (majadiliano) 15:10, 11 Machi 2015 (UTC)

Edmond Debeaumarché IBAKI[hariri chanzo]

Haina habari ndani yake itakayemsaidia mtu yeyote ila google translate mbaya. Iandikwe upya au kufutwa.Kipala (majadiliano) 07:34, 27 Januari 2015 (UTC)

Nimejaribu kuongeza habari zifaazo. Angalieni ukurasa wa Kiingereza kwa ajili ya kuboresha makala hii. Kwa sasa naona ibaki. --Baba Tabita (majadiliano) 08:40, 27 Januari 2015 (UTC)

Felix Christopher Mrema IBAKI[hariri chanzo]

Si Kiswahili, ni Kiingereza c/p. Tufute au mtu afanyie kazi (na kulinda baadaye?)Kipala (majadiliano) 16:30, 28 Januari 2015 (UTC)

Mgeni aliondoa Kiswahili na kuweka Kiingereza. Nimemwonya na kurudisha hali ya awali. Ibaki sasa. Kipala (majadiliano) 16:38, 28 Januari 2015 (UTC)

Jiografia ya Palestina - IBAKI![hariri chanzo]

Makala hii haina habari. Bila kujazwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 19:42, 31 Januari 2015 (UTC)

Makala ibaki sasa. Ndugu Riccardo amejaza makala vizuri sana - asante, mzee! --Baba Tabita (majadiliano) 08:19, 2 Februari 2015 (UTC)

Yungg rhymes[hariri chanzo]

Mwandishi amenakilisha makala ya Kiingereza tu bila kutafsiri kwa Kiswahili. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:46, 4 Februari 2015 (UTC)

Non-notable 14-year-old Youtube "rapper". Blocked on en-wp where he has many sockpuppets - see en:Wikipedia:Sockpuppet investigations/Dao2k. JohnCD (majadiliano) 20:58, 7 Februari 2015 (UTC)

Paradise Cay - IBAKI![hariri chanzo]

Yaliyomio ni uwongo sijui kama mzaha au mtihani kwetu. Si mji kisheria, ni eneo tu. Tufute au mtu afanyie kazi (na kulinda baadaye?)Kipala (majadiliano) 16:30, 28 Januari 2015 (UTC)

Nimeongeza sababu ya umaarufu wake, yaani ni mahali pa kufariki kwa Robin Williams. Nadhani ndiyo maana ya makala hiyo kuingizwa katika wikipedia ya Kiingereza. Sawa? --Baba Tabita (majadiliano) 06:41, 28 Aprili 2015 (UTC)

Felix C. Mrema Profile‎=[hariri chanzo]

mtumiaji amerudisha kuweka habari za Kiingereza chini ya lemma mpya. Ni Kiingereza tu. Kipala (majadiliano) 10:37, 30 Januari 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:12, 17 Aprili 2015 (UTC)

Simoni Mtakatifu[hariri chanzo]

Inaonekana mwandishi ametumia njia ya ujanja kwa kujitangaza. Inachekesha, hata hivyo si makala ya kamusi. Iende. Kipala (majadiliano) 20:03, 22 Februari 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:45, 28 Aprili 2015 (UTC)

Shukuru Kojaboy[hariri chanzo]

Sina uhakika kama kweli anastahili kuwa na makala. Wenyeji waseme. --Kipala (majadiliano) 07:53, 25 Februari 2015 (UTC)

Nimejaribu kupata habari zake mtandaoni lakini yuko kwenye Facebook na Twitter tu. Hata blogu yake imefutwa, na inaonekana hana umaarufu bado. Kwa hiyo nimeifuta makala. --Baba Tabita (majadiliano) 06:56, 28 Aprili 2015 (UTC)

Baskin-Robbins[hariri chanzo]

Inaonekana ni google-translate mbaya. Ama mpenzi wa aisikrimu hivi asahihishe yote au iende. Kipala (majadiliano) 11:19, 28 Februari 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:14, 17 Aprili 2015 (UTC)

Pierre Woodman[hariri chanzo]

Kiswahili si vibaya sana, mwandishi anaoekana hata hivyo hajui lugha. Tena 1 kati ya jitihada kusambaza majina ya watengenezaji wa filamu za ngono. Sijui... Kipala (majadiliano) 04:09, 11 Machi 2015 (UTC)

Hakuna marekebisho kwa wiki sita. Zote sentensi mbili zilikuwa na makosa; k.m. "film director" kwa Kiswahili siyo "mkurugenzi wa filamu". Haya, imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 07:03, 28 Aprili 2015 (UTC)

ADAM KARUMBETA[hariri chanzo]

Kuna haja ya kuisanifisha nakuongeza habari - kama hakunamwenye nafasi kwa hiyo ifutwe. Jinsi ilivyo ni zaidi rai juu yake kuliko habari zake. Kipala (majadiliano) 22:49, 11 Machi 2015 (UTC)

Hakuna maendeleo ya makala kwa wiki kadhaa. Tena, sikuweza kupata habari kuhusu mtu huyu mtandaoni nje ya makala hiyo. Haya, nimeifuta. --Baba Tabita (majadiliano) 07:07, 28 Aprili 2015 (UTC)

Samwel Yellah[hariri chanzo]

Nimesanifisha mbegu huu lakini sijui kama inastahili kubaki au la. Kipala (majadiliano) 18:31, 9 Aprili 2015 (UTC)

Hana umaarufu huyu kijana. Nimefuta makala. --Baba Tabita (majadiliano) 07:11, 28 Aprili 2015 (UTC)

Lusajo Chicharito Brown[hariri chanzo]

Sawa na hapo juu sijui kama anafaa kuwa na makala. Kipala (majadiliano) 18:33, 9 Aprili 2015 (UTC)

Nimefuta makala hiyo lakini kuhamisha yaliyokuwemo katika ukurasa wake wa mtumiaji. --Baba Tabita (majadiliano) 07:25, 28 Aprili 2015 (UTC)

Ponografia - IBAKI![hariri chanzo]

Bila shaka lemma ya kuvutia, lakini haina yaliyomo (ile nusu-sentensi imenakiliwa kutoka kamusi ya TUKI). Ipanuliwa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 10:24, 13 Aprili 2015 (UTC)

Nimeipanua tayari. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:58, 17 Aprili 2015 (UTC)

Kaimati[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai kwa kamusi elezo ila labda kwa wikamusi. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:28, 18 Januari 2015 (UTC)

Naona ibaki muda kidogo, nataka kuchungulia ni nini, maana naona jina latajwa mara kadhaa katika kurasa za upishiKipala (majadiliano) 04:17, 11 Machi 2015 (UTC)
Hakuna mabadiliko kwa miezi mitatu, ndiyo maana nimeifuta. --Baba Tabita (majadiliano) 19:34, 25 Juni 2015 (UTC)

ALYAFY PRODUCTION[hariri chanzo]

Kampuni hilo likistahili kupata makala, lazima kuingiza habari zake pamoja na marejeo na viungo vya nje. La sivyo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:40, 18 Januari 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:35, 25 Juni 2015 (UTC)

Black Leopard Fc(under 20)[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai, hata kichwa kina makosa ya uandishi. Bila kurekebishwa na kupanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:08, 17 Aprili 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:08, 24 Juni 2015 (UTC)

Center kwa ajili ya Utafiti na Maendeleo katika Sayansi ya Afya[hariri chanzo]

Ni tafsiri ya mashine, tena vibaya. Ama mtu anaifanyia kazi nyingi au ifutwe. Kipala (majadiliano) 19:46, 27 Aprili 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 07:06, 9 Juni 2015 (UTC)

Koloni ya Uingereza[hariri chanzo]

Matini haina yaliyomo yaliyo sahihi. Nadhani ilikuwa jaribio tu. Kipala (majadiliano) 18:28, 18 Mei 2015 (UTC)

Imeshafutwa na Kipala tarehe 19 Mei. --Baba Tabita (majadiliano) 07:03, 21 Mei 2015 (UTC)

Mtu wa hisia za ndani[hariri chanzo]

Haieleweki. Ikirejeshwa kwa makala nyenzake katika wikipedia ya Kiingereza, labda itawezekana kupanuliwa. La sivyo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 07:02, 21 Mei 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 07:06, 9 Juni 2015 (UTC)

Muddy kandonga[hariri chanzo]

Huyo kijana hana umaarufu wa kutosha kustahili makala yake katika kamusi elezo. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 07:05, 21 Mei 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:25, 2 Julai 2015 (UTC)

Ukawa[hariri chanzo]

Makala haina habari, haisemi ni kifupi cha nini, ni muungano wa akina nani, iko wapi, ina shabaha gani. Iongezwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 09:35, 6 Juni 2015 (UTC)

La C[hariri chanzo]

Makala haifai, ni fupi mno, tena imetafsiriwa kwa kutumia kompyuta, na Kiswahili chake ni kibovu wala haieleweki. Isiporekebishwa na kupanuliwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 19:27, 7 Juni 2015 (UTC)

Nimeifuta na kumwonya mwandishi Kipala (majadiliano) 16:46, 8 Juni 2015 (UTC)

Issaka Samsoni Messi[hariri chanzo]

Huyu mtu hana umaarufu wa kutosha, asipate makala ya kamusi. Jamani amezaliwa 2002 tu, na hakuna sehemu nyingine mtandaoni yenye habari zake. Makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 19:01, 24 Juni 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:25, 2 Julai 2015 (UTC)

Zawadi Mwagike[hariri chanzo]

Huyu mtu hana umaarufu wa kutosha, asipate makala ya kamusi. Hakuna sehemu nyingine mtandaoni yenye habari zake ila picha chache bila maelezo. Makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 19:05, 24 Juni 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:25, 2 Julai 2015 (UTC)

Kevin Gaspar Ndelwa[hariri chanzo]

Hana umaarufu (angalia Wikipedia:Umaarufu). Napendekeza makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:06, 28 Juni 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:25, 2 Julai 2015 (UTC)

Black Leopard FC Under20[hariri chanzo]

Kilabu hicho hakina umaarufu wa kutosha (angalia Wikipedia:Umaarufu). Tena, viungo vya nje havipo, na ukitafuta kwenye Google, hakuna matokeo ila kurasa za wikipedia hii. Ifutwe! --Baba Tabita (majadiliano) 13:11, 28 Juni 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:25, 2 Julai 2015 (UTC)

Omben Gerod Ngogo[hariri chanzo]

Hana umaarufu (angalia Wikipedia:Umaarufu). Napendekeza makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:47, 29 Juni 2015 (UTC)

naomba ifutwe makala hi
Imefutwa Kipala (majadiliano) 10:35, 30 Juni 2015 (UTC)

Yung Rhymes (Swahili)[hariri chanzo]

Salaam, wapendwa. Anayeilewa makala hiyo - tafadhali aiboreshe, akiona shida kama mimi, basi ninapendekeza ifutwe. Majanga tupu!--MwanaharakatiLonga 07:20, 9 Julai 2015 (UTC)

Nimeifuta. Hata katika wikipedia ya Kiingereza imefutwa kama uharabu, angalia https://en.wikipedia.org/wiki/Yung_Rhymes - basi, hata mtumiaji huyo aliyeianzia labda ni yule aliyezuiliwa katika wikipedia nyingine? Tumwangalie. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 08:56, 10 Julai 2015 (UTC)

Hot lady[hariri chanzo]

Sioni umaarufu wowote. Ni pia makala isiyofuata masharti ya kutaja vyazo. IFUTWE. Kipala (majadiliano) 23:28, 12 Agosti 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 20:08, 14 Agosti 2015 (UTC)

Amilton of Christ[hariri chanzo]

Makala ni tafsiri baya ya kompyuta tena nina mashaka kama anastahili makala. Mwandishi amesambaa makala juu yake kwenye wikipedia mbalimbali (de wameshamfuta, en bado iko kwa Kiingereza kibaya mno). Ilhali ni kweli mtu huyu yupo (vitabu vyake vyaonekana hapa: http://www.general-ebooks.com/author/97544770-amilton-de-cristo) hata jina lake si vile jinsi inavyoandikwa maana hali halisi aitwa "Amilton de Cristo". Haiwezi kubaki ilivyo, mimi sisikii wito wa kuisahihisha. Labda afutwe (hadi anapanusha crusade zake hadi Bongo..). Kipala (majadiliano) 06:57, 11 Septemba 2014 (UTC)

Kweli, shida za lugha zirekebishwe, lakini hata wikipedia ya Kiingereza ina makala kuhusu yake, kwa hiyo napendekeza ibaki. --Baba Tabita (majadiliano) 11:14, 11 Septemba 2014 (UTC)
Kwavile kwanza, hakuna marekebisho, na pili, hata katika wikipedia ya Kiingereza makala imefutwa, nimeifuta humo pia. --Baba Tabita (majadiliano) 07:19, 4 Januari 2016 (UTC)

Wikamusi[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 07:33, 6 Septemba 2015 (UTC)

Ilifutwa na Ndugu Kipala tarehe 19 Desemba 2015. --Baba Tabita (majadiliano) 15:17, 2 Januari 2016 (UTC)

Kizito Mihigo - IBAKI![hariri chanzo]

Tafsiri ya kompyuta, tena vibaya. Sina uhakika kama lemaa inafaa kweli au kama ni jaribio la kujitangaza tu. Isahihishwe au kufutwa. --Kipala (majadiliano) 08:38, 3 Oktoba 2015 (UTC)

Sasa , maandishi lazima lirekebishwe. si ifutwe Umutesi84 (majadiliano) 09:44, 3 Oktoba 2015 (UTC)
Baada ya marekebisho kadhaa, naona makala ibaki. Hata hivyo, marekebisho ya lugha n.k. yaendelee. --Baba Tabita (majadiliano) 07:17, 20 Oktoba 2015 (UTC)

Fikra za Mevlana[hariri chanzo]

Matini inaonekana umenakiliwa kutoka tovuti ya redio ya Uturuki. Hatuna makala bado kuhusu Mevlana yaani Jalal-ud-din Rumi lakini matini hii ni kipande tu kutoka makala za tovuti ya TRT. Pamoja na kunakiliwa haieleweki vema. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 09:26, 18 Desemba 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:19, 2 Januari 2016 (UTC)

Francis Sengo[hariri chanzo]

Sioni umuhimu wa mtu huyu. Nje ya wikipedia, napata blogu moja iliyoandika kuhusu harusi yake mwaka wa 2012, angalia hapa. Asipokuwa na umaarufu zaidi, nashauri makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:09, 18 Desemba 2015 (UTC)

Imefutwa Kipala (majadiliano) 06:56, 4 Januari 2016 (UTC)

Awadhi chang'a[hariri chanzo]

Mtumiaji mgeni alianzisha ukurasa huu akiweka habari juu yake mwenyewe. Nikimweleza utaratibu abaki na muda kidogo kuhamisha yaliyomo hadi kuufuta. Kipala (majadiliano) 13:23, 19 Desemba 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:19, 2 Januari 2016 (UTC)

Marco Masano[hariri chanzo]

Ameandika juu yake mwenyewe, yaliyomo yapo pia kwenye ukurasa wake Mtumiaji:Marco Masano. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 20:17, 1 Januari 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:19, 2 Januari 2016 (UTC)

Carlo Biotti[hariri chanzo]

Makala ilivyo haifai. Isiporekebishwa kufuatana na kanuni za wikipedia, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 19:44, 2 Januari 2016 (UTC)

Imefutwa Kipala (majadiliano) 06:57, 4 Januari 2016 (UTC)

Bernocchi[hariri chanzo]

Mwandishi yeye yule kama hapo juu, hajui Kiswahili. Anachezacheza tu. Kipala (majadiliano) 06:54, 4 Januari 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 07:16, 4 Januari 2016 (UTC)

Mariano Carsí[hariri chanzo]

Makala imeandikwa (au kunakiliwa) kwa Kifaransa na Kihispania. Bila kutafsiriwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:52, 3 Machi 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 08:59, 8 Aprili 2016 (UTC)

Tromsø - IBAKI![hariri chanzo]

Makala hii haina habari ya kutosha ili istahili kubaki ndani ya kamusi elezo. Isipopanuliwa, naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 08:53, 8 Aprili 2016 (UTC)

Baada ya maongezo aliyoingiza Ndg. Riccardo, makala ibaki. --Baba Tabita (majadiliano) 18:29, 8 Aprili 2016 (UTC)

Emilio Polli[hariri chanzo]

Yeye yule. Ifutwe au kuandikwa upya. Kipala (majadiliano) 07:02, 4 Januari 2016 (UTC)

Hakuna mabadiliko wala marekebisho kwa miezi mitatu; ikafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:46, 20 Aprili 2016 (UTC)

Don Giovanni[hariri chanzo]

Bila habari na makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:43, 20 Aprili 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 10:25, 11 Mei 2016 (UTC)

PICHA SAWIRISHA[hariri chanzo]

Inaonekana kama mwanzo wa riwaya; haifai kwa kamusi elezo, yaani ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 07:11, 20 Oktoba 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:22, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Facebook[hariri chanzo]

Tafsiri baya , ama ya kompyuta au ya mhariri mvivu. Isibaki ilivyo. Ingawa lemma inapendwa sana, sioni faida ibaki kama haiborshwi. Kipala (majadiliano) 06:33, 26 Oktoba 2015 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:24, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Msaada wa masomo ya elimu ya juu wa Jumuiya ya Madola[hariri chanzo]

Tafsiri ya kompyuta, tena ina viungo vyekundu vingi mno. Katika maoni yangu ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:48, 3 Januari 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:25, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Hungryalism[hariri chanzo]

Makala hii imetafsiriwa vibaya kutoka Kiingereza, hata kichwa cha makala ni Kiingereza. Tena, jamii zote ni viungo vyekundu. Isiporekebishwa na kupanuliwa naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:37, 6 Januari 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:26, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Lucky Star[hariri chanzo]

Sentensi moja tu, tena katika Kiswahili kibovu, na viungo viwili. Haitoshi kwa makala. Isiporekebishwa na kupanuliwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:18, 7 Januari 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:26, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Ulimwengu wa Sayansi[hariri chanzo]

Ingawa ni maandishi mazuri, ni insha zaidi ya makala ya kamusi elezo. Je, ibadilishwe kama makala kuhusu Ibn Firnas, au tufanyeje? Haiwezekani ibaki ilivyo. Bila mabadiliko, naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 19:29, 10 Januari 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:26, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Afya, Utalii na Uturuki[hariri chanzo]

Insha nyingine tena. Je, iunganishwe na makala kuhusu mji wa Canakkale, au ni mada tofauti? Bila mabadiliko, naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 19:29, 10 Januari 2016 (UTC)

Imefutwa, na maneno yake kuingizwa katika Majadiliano:Çanakkale. --Baba Tabita (majadiliano) 12:52, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Leo katika historia[hariri chanzo]

Lemma haifai. Habari za maana zipelekwe 23 Januari halafu makala kufutwa. Kipala (majadiliano) 19:45, 25 Januari 2016 (UTC)

Baada ya kuunganisha habari na makala ya 23 Januari na zinginezo, makala hiyo imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 20:09, 25 Januari 2016 (UTC)

Makala za mtumiaji:Trtswahili[hariri chanzo]

Michango yote imenakiliwa kutoka tovuti ya redio ya kimaaifa ya Uturuki. Sidhani kwamba mchangiaji ana nia mbaya lakini haelewi mfumo wa wikipedia. Makala zifutwe. Kipala (majadiliano) 20:04, 25 Januari 2016 (UTC)

Zimefutwa, ila maneno ya "Mji mkuu wa kiutamaduni wa Istanbul" yamehamishwa katika makala ya Makumbusho ya kutokutambuo uovu, kwa vile yanaeleza riwaya hiyo ya Orhan Pamuk. --Baba Tabita (majadiliano) 13:16, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Sarpsborg[hariri chanzo]

Makala hii haina habari ya kutosha ili istahili kubaki ndani ya kamusi elezo. Isipopanuliwa, naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 08:56, 8 Aprili 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:30, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Tønsberg[hariri chanzo]

Makala hii haina habari ya kutosha ili istahili kubaki ndani ya kamusi elezo. Isipopanuliwa, naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 08:56, 8 Aprili 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:30, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Stavanger[hariri chanzo]

Makala hii haina habari ya kutosha ili istahili kubaki ndani ya kamusi elezo. Isipopanuliwa, naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 08:56, 8 Aprili 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:30, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Vadsø - IBAKI![hariri chanzo]

Makala hii haina habari ya kutosha ili istahili kubaki ndani ya kamusi elezo. Isipopanuliwa, naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 08:56, 8 Aprili 2016 (UTC)

Mtumiaji:Riccardo Riccioni ameongeza kidogo. Bado ni makala fupi. --Baba Tabita (majadiliano) 13:30, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Teletubbies[hariri chanzo]

Makala hii haina habari ya kutosha ili istahili kubaki ndani ya kamusi elezo. Isipopanuliwa, naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:03, 8 Aprili 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:31, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Shaykh 'Abdullaah Swaalih Al-Farsy - IBAKI![hariri chanzo]

Makala hii inajitambulisha kuwa kopi-paste kutoka gazeti hali ambayo ni marufuku kwenye wikipedia. Bila shaka huyu mzee anastahili makala lakini jinsi ilivyo heri ifutwe. Yuko anayeishughulikia?Kipala (majadiliano) 10:49, 28 Aprili 2016 (UTC)

Isifutwe. Nimeiboresha. Pia nitarudi tena siku nyingine kuendelea kuiboresha na kuifanya iwe Kiwikipedia zaidi! Samahani kwa usumbufu uliojitokeza!--MwanaharakatiLonga 10:44, 15 Juni 2016 (UTC)

Historia ya hisabati[hariri chanzo]

Ni kopi-paste kutoka tovuti ya watchtower. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 08:54, 15 Juni 2016 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:33, 20 Oktoba 2016 (UTC)

Ariri Charles IMEFUTWA[hariri chanzo]

Makala ilianzishwa bila habari yoyote. Tena siwezi kugundua umaarufu wa mtu huyo. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:30, 23 Februari 2017 (UTC)

Nimeifuta Kipala (majadiliano) 12:07, 23 Februari 2017 (UTC)


Magimbi IBAKI ![hariri chanzo]

Jinsi ilivyo makala (ambayo ni fupi sana) haielezi magimbi ni chakula kutokana na mmea gani, au kama ni jina la kutaja vyakula vyenye asili mbalimbali. Nimekuta "en:yam" au "en:taro" (sw jimbi) kama maelezo kwa magimbi. Kimsingi mada ya kufaa lakini heri iende kuliko kutoeleweka

Šiprage‎ Inabaki[hariri chanzo]

Tafsiri ya kompyuta. mtu asahihishe au ifutwe. Kipala (majadiliano) 21:10, 19 Machi 2017 (UTC)

Imesahihishwa, asante Riccardo, inabakiKipala (majadiliano) 09:07, 23 Machi 2017 (UTC)

Ndoa katika uislam - IBAKI![hariri chanzo]

Makala yote ni kopi-paste kutoka HAPA, na ZAIDI HAPA. Ilhali ni mchango wa kwanza wa mchangiaji mpya naona tumwachie wiki 1 au mbili asahihishe kama anaelewa, Kama sivyo, ifutwe. Kipala (majadiliano) 13:27, 26 Oktoba 2016 (UTC)

Inaonekana kama mchangiaji amerekebisha makala nzima. Hongera! Kwa hiyo makala ibaki. --Baba Tabita (majadiliano) 21:09, 8 Desemba 2016 (UTC)
Bado makala dhaifu mno, bado dalili nyingi ya kunakiliwa kutoka ukurasa wa mahubiri. Nimejaribu kuingiza habari kadhaa za kimsingi kwa lugha ya kikamusi. Kipala (majadiliano) 12:06, 23 Februari 2017 (UTC)

Digital object identifier IMEFUTWA[hariri chanzo]

Ni Kiingereza tu, na ingekuwa vigumu sana kuitafsiri kwa sababu ya istilahi. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:10, 2 Aprili 2017 (UTC)

Imefutwa Kipala (majadiliano) 07:14, 5 Julai 2017 (UTC)

Digital Object Identifier IMEFUTWA[hariri chanzo]

Ni Kiingereza tu, na ingekuwa vigumu sana kuitafsiri kwa sababu ya istilahi. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:10, 2 Aprili 2017 (UTC)

Imefutwa Kipala (majadiliano) 07:14, 5 Julai 2017 (UTC)

Mayestron[hariri chanzo]

No evidence of notability. Cross-wiki promotion by various IP addresses. en:Mayestron was deleted 4 times, en:Mayestron (rapper) was deleted twice, fr:Mayestron was deleted 4 times. Also deleted: es:Mayestron, pt:Mayestron, uk:Mayestron, zh:Mayestron, etc. - ErikvanB (majadiliano) 15:32, 25 Mei 2017 (UTC)

Mayestron Ep One (Album)[hariri chanzo]

No evidence of notability. Cross-wiki promotion of the singer Mayestron by various IP addresses. en:Mayestron was deleted 4 times, en:Mayestron (rapper) was deleted twice, fr:Mayestron was deleted 4 times. Also deleted: es:Mayestron, pt:Mayestron, uk:Mayestron, zh:Mayestron, etc. - ErikvanB (majadiliano) 15:34, 25 Mei 2017 (UTC)

Nothing To Share (wimbo)[hariri chanzo]

No evidence of notability. Cross-wiki promotion of the singer Mayestron by various IP addresses. en:Mayestron was deleted 4 times, en:Mayestron (rapper) was deleted twice, fr:Mayestron was deleted 4 times. Also deleted: es:Mayestron, pt:Mayestron, uk:Mayestron, zh:Mayestron, etc. - ErikvanB (majadiliano) 15:37, 25 Mei 2017 (UTC)

Migogoro, Ujumbe‎, Kuhakiki‎[hariri chanzo]

Zote hafifu mno kwa kamusi elezo. Naona mchangiaji ni mgeni. Nimemwandikia hivi:

Bwana Kelvin, asante kwa michango ya Migogoro, Ujumbe‎  na Kuhakiki‎. Kwa bahati mbayo zote hazilingani bado na masharti ya makala katika kamusi elezo. Ukipenda zinafaa kuhamishwa kwa mradi wetu dada wikamusi ambako kuna maelezo ya maana ya maneno tu. Kama unapenda, naomba niulize au msimamizi mwingine, tutakusaidia. Kama unataka zibaki hapa wikipedia yenyewe ni lazima kuimarisha na kupanusha yaliyomo. angalia kwa mfano makala ya kama mfano kuhusu "Ujumbe".

Basi tusubiri kidogo. Kipala (majadiliano) 22:45, 15 Machi 2017 (UTC)

Ndiyo, mwanafunzi wangu huyo anapenda kuchangia namna ya Wikamusi. Nikiwahi narefusha mimi au nafuta moja kwa moja bila kufuata utaratibu mrefu... samahani kwa hilo! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:41, 16 Machi 2017 (UTC)
Makala za Migogoro na Kuhakiki zimefutwa. Makala ya Ujumbe inaweza kubaki ilivyorefushwa na Ndg. Riccardo. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 16:14, 2 Agosti 2017 (UTC)

Koloni ya Uingereza nchini kenya[hariri chanzo]

Makala inajaa makosa na habari zisizo kweli. Sioni kitu ndani yake kisichoelezwa tayari penginepo. Sioni sababu kuitunza. Kipala (majadiliano) 07:12, 5 Julai 2017 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 16:10, 2 Agosti 2017 (UTC)

Wikipedia:Jina la makala[hariri chanzo]

Mtumaiji mapya aliingiza matni ndefu mahali ambako si pake. Tena matini ni kama makala ya maoni ya gazeti, si kamusi elezo. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 18:24, 10 Julai 2017 (UTC)

Labda tuokoe sehemusehemu mahali pake. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:54, 11 Julai 2017 (UTC)
Kwa vile hakuna aliyeifanyia kazi kwa wiki tatu sasa, nimeifuta. --Baba Tabita (majadiliano) 16:07, 2 Agosti 2017 (UTC)

Mayestron (Mwimbaji)[hariri chanzo]

Tafsiri ya kompyuta, si nzuri, sioni haja ya kuisahihisha. Kipala (majadiliano) 17:21, 24 Julai 2017 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 16:02, 2 Agosti 2017 (UTC)

Hamis sempanga[hariri chanzo]

Inaonekana alitaka kuandika kwenye profile yake, lakini akachapisha ukurasa mpya. Luckimg2 (majadiliano) 14:23, 2 Agosti 2017 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:59, 2 Agosti 2017 (UTC)

Utawala wa sultani zanzibar - IBAKI kama marejeo![hariri chanzo]

Habari fupi zina makosa mengi tena kuhusu mada iliyopata makala tayari. Ilhali makala Usultani wa Zanzibar inahitaji kuboreshwa ile jaraibio fupi haina habari ndani yake zinazosaidia hapa. Kipala (majadiliano) 21:09, 14 Julai 2017 (UTC)

Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 16:02, 2 Agosti 2017 (UTC)
Baada ya kufuta nikaona bora irejee ile makala myingine Usultani wa Zanzibar, yaani ndivyo nilivyofanya sasa. --Baba Tabita (majadiliano) 16:03, 2 Agosti 2017 (UTC)